Haiwezekani Wasabato kuhubiri neno la Mungu bila kutaja Kanisa Katoliki? Au ni mafunuo? au mbinu za kupata na kutunza wafuasi?

Hakuna anayeshindana na msabato ila msabato ndiye anayeshindana na RC

Pia hebu niangalizie kwenye Biblia kama kuna mafungu yanayozungumzia:

Kurudi wa Yesu Kristo miaka ya 1,800 kama William Miller alivyodai

Habari ya Hukumu ya upelelezi

Habari za Bwana wetu Yesu Kristo kuhmia chumba cha patakatifu pa patakatifu kutokea chumba cha patakatifu akiwa huko kwenye hekalu la mbinguni

Habari za amri ya Sabato kuwa na mng'aro mkubwa zaidi ya amri nyingine
 
😀😀Inavyoonekana adui mkubwa wa Wasabato sio shetani bali ni RC.Sijawahi kuona Wasabato wakiwashambulia Moravian,Anglican,Lutheran,AIC,n.k japo wote wanasali siku ya Jumapili,wote wanabatiza watoto wadogo,wote wanabatiza kwa maji ya kunyunyiza,wote wanaamini fundisho la utatu mtakatifu,wote wanakula sakramenti,wote wanasherehekea sikukuu ya krismasi na pasaka n.k
 
Nakuona umeamua kupambania mifumo ya Roman Catholic,na ikiwa mtazamo wako umekuwa fixed humo,hauta elewa labda papa aje akuthibitishie mwenyewe kuwa yeye pamoja na taasisi yao/zao ni wakala wa Shetani.
Huu sio uwanja wa mashindano/mapambano ya kidini/kiimani [dhehebu],Bali ni sehemu ya kuelimishana kwa aliye/walio tayari kujifunza pamoja.
Nimekupa vyanzo vya maandiko [vifungu vya biblia]vinavyothibitisha ukweli,[ninahisi hukusoma],tambua kuwa HOJA hujibiwa kwa HOJA na si kubishana tu bila vielelezo, Msingi wa huu mjadala upo kwenye maandiko matakatifu [biblia tunayoiamini sote].
Hivyo kama ambavyo nimekupa vyanzo vya maandiko [vifungu vya biblia] kuthibitisha ukweli wa hoja,ndivyo unavyopaswa kufanya kuthibitisha ukweli wa hoja yako pia.
Nakushauri,soma kwanza vyanzo vya maandiko nilivyokupa, kisha urudi na hoja yenye vielelezo vya biblia pia.
KARIBU.
 
Kwa hiyo wewe unaijua mifumo/misingi ya kikatoliki, kuliko wakatoliki wenyewe. Kwa hiyo nyie kwenye masomo yenu kuna kasegment cha kuidiscuss ukatoliki?

Sijaona reference ya andiko lolote zaidi ya chai.
 
Kwa hiyo wewe unaijua mifumo/misingi ya kikatoliki, kuliko wakatoliki wenyewe. Kwa hiyo nyie kwenye masomo yenu kuna kasegment cha kuidiscuss ukatoliki?

Sijaona reference ya andiko lolote zaidi ya chai.
Kunywa hiyo chai huenda itakusaidia.
 
Mimi nina bahati kupata vibinti vya namna hio ila vinanishinda tu kuniambia niende kanisani kwao najikuta nakula na kupita
😂😂😂🤣😅😆na ndo maana ukienda kwenye hayo makanisa utakuta vibinti vingi vimezalishwa na havina ramani.
Vinajifanyaga havijali hata ukikipiga chini
 
Mkuu umetoa vyanzo vya maandiko na uko sahihi ila ulipokosea kama ilivyo Wasabato wenzako ni tafsiri mliyoitoa ni potofu.
 
Ni sawa na waislam kuwaona wakristo hamnazo kwa kumuabudu mwanadamu "Yesu" kutwa kucha na mihadhara ya kuukashifu ukristo na biblia.
Hata hao ni hivyo hivyo kwa wakatoliki.
 
Mkuu wanaoifananisha taasisi ya RC mnyama wa kutisha na taasisi ya Wasabato yaani SDA na siyo Biblia

Wasabato wamesoma Vitabu vya Daniel na ufunuo na kuamua kuwa na hiyo tafsiri ambayo kwao wanaona ni sahihi

Ujitahidi kuacha kuungaunga mada
 
Mkuu hebu fafanua hayo mafundisho ya uongo kuhusu wafu?
 
Mungu ninae mzungumzia mimi hajaletwa na mzungu hata kitabu ninacho tumia kufanyika rejea hakijaletwa na mzungu... Labda... Narudia tena hapa labdaa hizi simu tunazotumia kujadaliana humu mtandaoni...

Pia hoja zako zinamkata Mungu, katikati ya hoja zako na hitimisho unamkubali tena... Sasa kipi ni kipi?

Chakukushauri ongeza maarifa kuhusu Imani kwanza.. na unapoyatafuta iweke huru fikra yako kujifunza.. wala usiwe na mawazo ya kupinga, maana ukiwa na mawazo hayo kamwe hutojua kweli.

Kuna kipindi niliwahi kukutana na changamoto Fulani katika maisha nikajawa na mawazo kama yako... Lakini badae nikamrejea Mungu akaniokania, ingawa Kuna wakati alinidhihirishia uwepo wake kwa njia ngumu kidogo lakini kupia hiyo njia ngumu ambayo kibinadamu inaumiza sana na kukatisha tamaa alinikumbusha kitu cha kujifunza hapa duniani... Na ninavyo zidi kukitunia kina msaada sana katika maisha yangu.

N:B Naomba kwa Mungu Roho mtakatifu awe msaada kwako.
 
Nimeeleza kwamba Mungu yupo mkuu..

Ila Ninapinga namna hayo maandiko ya vitabu jinsi yanavyomuelezea....

Mungu ninaemuamini mimi sio huyo wa kwenye vitabu ...
 
Point
 
Reactions: K11
Kwani huko mbinguni mkienda wenyewe kinawauma nini?
Hatuwazuii,nendeni tu!
 
Mkuu hebu fafanua hayo mafundisho ya uongo kuhusu wafu?
Wanafundisha wafu wako pagatory... Hakunaga kitu kama hiki kwakuwa mfu hajui neno lolote kulingana na Biblia. Mtu anapokufa pumzi inamrudia aliyeiumba na mwili ambao hauna uhai tena unakuwa kaburini had ufufuo wa mwisho Uwe ufufuo wa kwanza kwa watakatifu au ufufuo wa pili kwa waliotenda mabaya.

Kufanya ibada za wafu eti kumuombea marehemu ni makosa kwa vile hesabu ya mtu na Mungu wake inakamilika pale anapokufa hakuna namna ya kuboresha tena kile ambacho mtu hakukikamilisha kabla ya mauti yake.
 
Kanisa katoliki kachagua kuplay role ya kitimoto.

Hapa duniani hakuna kiumbe kinasimangwa kama huyo jamaa,ila ndiyo kwanza anazidi kunona na kutoa mafuta.

Ndiyo RC sasa.
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…