Dah kumbe mtu na c MUNGU.elewa fungu hilo vzur.Kulikuwa na sheria 2 zinazokinzana SHERIA YA MUNGU NA YA MAAGIZO AMBAYO MUNGU ALIMWAMBIA MUSA AWAANDIKIE AWEKE PEMBENI MWA SANDAKU LA AGANO.Yesu alipokuja aliondoa sheria ya musa ikabaki ya MUNGU ambamo ndan yake imo sabatho.
Kol 2:16-17
Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
Narudia, kuabudu ijumaa sijui jumamosi au jamapili hakumpeleki mtu kwa Mungu kama matendo yake binafsi hayamlingani BWANA.
Kinachowapofusha wasabato ni mapokeo ya imani yenu yanayojikita kwenye siku badala ya kuwekea mkazo wokovu.
Kwenye madhehebu yote kuna wazinzi, washirikina, waongo, wezi, wasengenyaji et al, je! hao wenye matendo hayo kwa vile wanaabudu siku ya jumamosi inatosha wao kurithi uzima wa milele?
Nakuthibitishia bila mashaka, kwenye kila dhehebu kuna baadhi ya watu wataurithi uzima wa milele kwa maana uzima wa milele hauko katika siku wala majira flani.
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Kwa nyongeza dini ya kweli ndiyo hii;
Yak 1:27
Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Vifungu vya kurejelea vyote viko agano jipya ambalo ndilo linalobeba hatma ya kizazi hiki.