Haja Ya Kuwepo Wawakilishi Wa Zanzibar Kwenye Balozi..

Haja Ya Kuwepo Wawakilishi Wa Zanzibar Kwenye Balozi..

under_age,mtu wa pwani,...

jamani acheni acheni jamani...yaani mnataka watu million 1 mgawane nusu kwa nusu na watu milioni 30?

kuhusu wa-zenj kufanya kazi huku Bara, hiyo ni win-win situation. wangeweza kuwa jobless huko ZNZ, au wakambilia Kenya etc. wakati wanatoa utaalamu wao Bara, mapato wanaweza kupeleka Zenj.

hata wapemba waliojazana huku Bara wakiuza maduka. hiyo nayo ni win-win situation. mwanzo tulikuwa na wachaga hawapendi kukopesha lakini sasa hivi tuna afueni baada ya kuja wapemba. hao wangebakia pemba wangekuwa jobless.

kweli kabisa ukichukua percentage wise waZenj wameelimika kuliko Wabara wote. Lakini ukichukua waZenj ukalinganisha say na Wahaya au Wachaga basi hapo ni hadithi nyingine kabisa.

MAFUTA:

Hili suala la mafuta mimi nashauri muachiwe. Lakini tuelewane kuhusu uchimbaji wa mafuta off-shore.

Fununu ni kwamba, mkondo wa bahari kati ya Zenj na Tanganyika ni mwembamba kiasi kwamba kutakuwa na utata ktk utekelezaji wa SHERIA za KIMATAIFA za matumizi ya RASILIMALI zilizoko BAHARINI.

Kwani Zenj wakigundua DHAHABU kuna kipengele kimeeleza kwamba tunapaswa kugawana 50/50?
 
Kwa ujinga wangu, wanzibari wanatuzidi sana sisi wa bara kwa habari ya uelewa wa kisiasa.

This is very strong point mkuu wangu, isipokuwa kuhusiana na hii ishu bado wa-Tanzania, tunajaribu kukimbia kivuli chetu thinking kwamba itatokea miujiza na kuurekebisha our fragile muungano, maana in the big picture malalamiko yanayotolewa kila wakati na pande zote mbili huwa sio the real ishu, the real ishu ni kama do we need this muungano thing anyways? na hii ishu ni kwa both bara na visiwani,

Sasa mpaka siku moja tutakapoamua kuweka manyanga chini, na kusema ukweli wa tatizo letu, tutaendelea kushikana mashati na none ishus on muungano, kama this one!
 
Hata mimi najiuliza kama CHADEMA wakiingia na kuchukua dola na sera ya majimbo- swala la Zanzibar kama nchi itakuwaje? Je serikali za Zenj itapenda kugawa mikoa yake 5 ktk majimbo? say Pemba jimbo 1 na Unguja Majimbo mawili

Hakuna nchi inayoitwa Zanzibar duniani ispokuwa kuna Tanzania ambayo ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama ni kugawa majimbo basi Zanzibar itakatwa katwa kama sehemu nyingine yeyote ya Tanzania. Baada ya Marekani kuungana umeisha sikia nchi inayoitwa Colorado au Texas. Lakini, kuna jimbo la Colorado na Texas. Kwahiyo, visiwani kutakuwa na majimbo kama Kagera na Arusha.

Watu wanasahau kuwa 1964 ni nchi mbili ziliungana- ni vema watu wakakumbushwa- sii vema leo 2007 kuchukulia Visiwani kama jimbo au Mkoa!

1964 ni miaka 43 imepita na ni zaidi ya vizazi (generation) viwili na wengi wetu humu tulikuwa hatujazaliwa. Huu ni wakati tofauti kabisa. Maamuzi yoyote yatakayofanyika yatazingatia mahitaji ya wakati huu.

Maoni yangu ni kwamba sioni sababu ya special treatment ikiwa hizi ni nchi mbili zilizoungana zikiwa na idadi tofauti ya watu lakini mahitaji sawa. msongamano wa watu Zanzibar ni 1/35 ya msongamano wa watu Bara. Why special treatment to them?
 
Lakini historia inaonesha kama kinyume vile... Nchi nyingi duniani hazitengani bali zinaungana katika kutatua matatizo... .SteveD.

SteveD, Nchi nyingi zinatengana, halafu kunaanzishwa Jumuia kama za Afrika MAshariki, SADC, EEC, nk.

Ninachisema ni kuwa ukiangalia historia nchi kama Marekani ndiyo ambayo imebakia na hii ni kwa sababu muungano wao upo clear, kila kitu kinaeleweka na hakuna ukandamizaji, unapokwenda State nyingine lazima ufate sheria za huko period, na ndiyo maana kuna State zinazoruhushu hukumu ya kifo na nyengine haziruhusu, pia kuna nyingine zinaruhusu ushoga na State nyingine haziruhusu, kuna State ambazo wanawake hawarushusiwi kuvaa "thong", na hukumu yake ni jela nk.

Nchi kama Ethiopia na Eritrea, muungano wao ulikuwa wa kusuasua kama wetu, mwisho wake ukafa. Pia kama Senegambia (senegali na Gambia), wala haukudumu. Kuna nchi kama Guinea Bissau na Visiwa vya Cape Verde nazo zishasambaratishana na kila nchi imeenda kivyake, hawa kwa kiasi kikubwa ni kama Bara na visiwani, muungano ulikuwa wa kibabe na kulazimishana. Angalia Jugoslavia je imeishia wapi?, hapa zimetoka nchi zaidi ya nne tayari na bado kunachemka! Kuna hiyo nchi ikiitwa Czechekoslovakia, sasa kuna Czeko na Slovakia na ni nchi mbili tofauti. Soviet Union ndo wala usiseme, zimetoka nchi zaidi ya kumi na tano, na bado zitaongezeka! Hiyo Russia yenyewe bado kunachemka na akina Chechnya (Yaani Russia itamegeka tena). Sudan kwenyewe unakuonaje? nao watasambaratika tu! Hebu angalieni UK yenyewe kunachemka, wa scotland, wa wales na wa Irish wala hawataki kuitwa waBritish, na wenyewe wanasema wanatafuta uhuru wao wa kweli, mambo yanavyokwenda nao hauna miaka mingi utavunjika tu je seuze huu wetu maboksi wa Tanganyika na Zanzibar ambao umejaa kejeli, kashfa, ubinafsi na Udini? Mifano bado ni mingi ila naishia hapa.

Ninachotaka kuwaambia wanaJF ni kuwa muungano si kulazimishana au ubabe, ukweli utakuja onekana siku moja. Sisi muungano wetu una kasoro nyingi na fukuto ni kubwa sana, tunachofanya ni ku delay kuuvunja, ila utakuja vunjika tu.
 
under_age,mtu wa pwani,...

jamani acheni acheni jamani...yaani mnataka watu million 1 mgawane nusu kwa nusu na watu milioni 30?

kuhusu wa-zenj kufanya kazi huku Bara, hiyo ni win-win situation. wangeweza kuwa jobless huko ZNZ, au wakambilia Kenya etc. wakati wanatoa utaalamu wao Bara, mapato wanaweza kupeleka Zenj.

hata wapemba waliojazana huku Bara wakiuza maduka. hiyo nayo ni win-win situation. mwanzo tulikuwa na wachaga hawapendi kukopesha lakini sasa hivi tuna afueni baada ya kuja wapemba. hao wangebakia pemba wangekuwa jobless.

kweli kabisa ukichukua percentage wise waZenj wameelimika kuliko Wabara wote. Lakini ukichukua waZenj ukalinganisha say na Wahaya au Wachaga basi hapo ni hadithi nyingine kabisa.

MAFUTA:

Hili suala la mafuta mimi nashauri muachiwe. Lakini tuelewane kuhusu uchimbaji wa mafuta off-shore.

Fununu ni kwamba, mkondo wa bahari kati ya Zenj na Tanganyika ni mwembamba kiasi kwamba kutakuwa na utata ktk utekelezaji wa SHERIA za KIMATAIFA za matumizi ya RASILIMALI zilizoko BAHARINI.

Kwani Zenj wakigundua DHAHABU kuna kipengele kimeeleza kwamba tunapaswa kugawana 50/50?

bigi snake (jokakuu) , u r very right na ndio maana nasema solution ya muungano huu ni serikali tatu. kwani ukiangalia kiundani hiyo population inayowekwa kama ni kigezo basi ndiyo inayoimaliza zanzibar. pia pale tunapoiona serikali imebeba jina la muungano lakini deep inside tanganyika ndie anaicontroll hiyo the so called serikali ya muungano. naomba niulize hivi mawaziri wa tanzania wanatokea upande gani wa muungano?(sielewi naomba nieleweshwe). sipendi kuona tunafarikiana kiasi hiki lakini naamini kuikomboa zanzibar ndio kuikomboa tanganyika na vise versa. njia moja ya kuiweka tanganyika isitegemewe na zanzibar kama wanavyodai sasa basi ni kuipatia tanganyika serikali yake.my apologies kwa nilipotumia jazba ,i admit kwamba mimi ni mtu ninaepanda jazba haraka . i still respect all tanzanian ,isipokuwa wale wanaokuja na malumbano ya kukejeli.
ni mtanzania mwenzenu under age
 
hili poleni, hatutaki kulisikia, na ndio maana CHADEMA hawana chao zanzibar.

Pole wewe; Kitakachoamua CHADEMA kwenda ikulu si kura milioni 2 za wazanzibar bali kura milioni 35 za watanzania. Ni wajang'ombe lakini katika hili naunga mkono muungano wa serikali tatu. Ama sivyo twende majimbo. Provinsi ya Pemba, Province ya Unguja, Province ya Ziwa, Province ya Magharibi, Province ya Kaskazini, Province ya Mashariki, Province ya Kusini, Province ya Kati, Province ya Dar es salaam. Kila serikali iwe na mamlaka yake. Balozi awe mmoja. Kama provinsi itaona faida kupeleka afisa katika ubalozi wa nchi fulani kutokana na maslahi ya provinsi hiyo basi watapeleka. Sio masuala ya kupeleka mapunda mtoni hata kama hayana kiu!

Asha
 
bigi snake (jokakuu) , u r very right na ndio maana nasema solution ya muungano huu ni serikali tatu. kwani ukiangalia kiundani hiyo population inayowekwa kama ni kigezo basi ndiyo inayoimaliza zanzibar. pia pale tunapoiona serikali imebeba jina la muungano lakini deep inside tanganyika ndie anaicontroll hiyo the so called serikali ya muungano. naomba niulize hivi mawaziri wa tanzania wanatokea upande gani wa muungano?(sielewi naomba nieleweshwe). sipendi kuona tunafarikiana kiasi hiki lakini naamini kuikomboa zanzibar ndio kuikomboa tanganyika na vise versa. njia moja ya kuiweka tanganyika isitegemewe na zanzibar kama wanavyodai sasa basi ni kuipatia tanganyika serikali yake.my apologies kwa nilipotumia jazba ,i admit kwamba mimi ni mtu ninaepanda jazba haraka . i still respect all tanzanian ,isipokuwa wale wanaokuja na malumbano ya kukejeli.
ni mtanzania mwenzenu under age

Makubaliano ya muungano ya pitiwe tena wananchi wa pande zote mbili waambiwe nini cha kutegemea kutoka pande zote mbili, kusema kweli ukiniuliza mimi nini kilichofikiwa mpaka wakaunganisha tanganyika na zanzibar sijui.
Solution hapa ni serikali moja au serikali tatu lakini kwenye swala la serikali tatu gharama za serikali ya muungano zitagawanywa nusu kwa nusu? Sasa hapo napo nina uhakika lazima malalamiko yatatokea tu.
 
kwa kuanzia tanganyika haijachangia hata shilingi kwa maana serikali ya tanganyika haipo.

pili wazanzibari wengi wanafanya kazi ndani ya serikali ya muungano ambayo kimtindo inaonekana kuipendelea tanganyika na kwa hiyo tanganyika kunufaika na wataalamu wetu.

tatu zanzibar ktk mapato ya taifa wao wanapewa asilimia 4. something kwa mantiki nyengine zinaenda kwenye muungano ambayo zanzibar imo na intakiwa inufaike ila kimsingi hamna maendeleo yyte kwetu.

wizara zote za muungano na idara zake ziko tanganyika kiasi ambacho tanganyika inajiimarisha zaidi kuliko zanzibar, si kiajira kimiundo mbinu, kimajengo, kiuchumi na mengineo.

stay tune tunakuja mengi tumeyapeleka na ss tunasisitiza mazungumzo ndio njia salama ya kutatua kero za muungao ikishindikana tugawane mbanjo

Nani kakudanganya Tanganyika haipo? ipo, inaitwa Tanzania Bara. Kama Tanganyika isingekuwepo pasingekuwepo mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano. Kuna taasisi zipo zinaitwa ni za bara pekee. Hazina mamlaka ya kufanya kazi Zanzibar. Hivyo hivyo kwa baadhi ya sheria mf. Sheria ya Vyombo vya Habari ni ya bara pekee, Zanzibar kuna sheria yake.

Asilimia 4 tu? huu ni unyonyaji. Nadhani Zanzibar ingepewa walau asilimia 6-8. Kwa kigezo cha watu. Kama wazanzibar wako milioni 2; wa bara wako milioni 35. Asilimia 10 ingekuwa 3.5 milioni hivyo milioni 2 stahili yao ni asilimia 6 sana sana 8. Ungeongezea zaidi umewanyonya walio wengi. Kwani mchango wa Zanzibar katika pato la Taifa ni kiasi gani? Karafuu na biashara si vimelala umebaki utalii tu?

Dawa ni Serikali Tatu- hapo kila mtu atakuwa na mapato yake na atalazimika kuchangia kiasi serikali kuu! Tutakuwa na mji mkuu ambao ni sehemu inayojitegemea kama ilivyo Washington kule Marekani. Kama serikali tatu hazitakiwi basi tubakishe Tanganyika na Zanzibar Zote kwenye historia tu; tuunde majimbo au provinsi. Mbona Afrika Kusini wamefanya hivyo? hata Nigeria nao imewasaidia kupunguza vita vya kugombea rasilimali. Tuache historia ibaki simulizi, kadiri tunavyolinda hii historia yenye mashaka kwa vitendo ndio tunazidi kutengeneza ufa katika taifa. Kama Tanganyika wanasherekea uhuru wa nchi ambayo imebaki kwenye tafsiri ya kishria tu, basi Zanzibar nayo ife mapinduzi yasherekewe kwenye historia tu. Tuunde provinsi mpya, kwa katiba mpya ambayo tutakubaliana jamani

Asha
 
Kwa ujinga wangu, wanzibari wanatuzidi sana sisi wa bara kwa habari ya uelewa wa kisiasa.

This is very strong point mkuu wangu, isipokuwa kuhusiana na hii ishu bado wa-Tanzania, tunajaribu kukimbia kivuli chetu thinking kwamba itatokea miujiza na kuurekebisha our fragile muungano, maana in the big picture malalamiko yanayotolewa kila wakati na pande zote mbili huwa sio the real ishu, the real ishu ni kama do we need this muungano thing anyways? na hii ishu ni kwa both bara na visiwani,

Sasa mpaka siku moja tutakapoamua kuweka manyanga chini, na kusema ukweli wa tatizo letu, tutaendelea kushikana mashati na none ishus on muungano, kama this one!

Mwalimu Nyerere si aje achukue vipande vya muungano wake wa serikali mbili unatotetewa na CCM na kwenda nao akhera? Mvumilivu hula mbovu! Mimba ya muungano imeshatunga usaha..

Asha
 
Mtu wa pwani......

niliwahi sikia kuwa TANGANYIKA walikuwa hawana KITI KTK UMOJA WA MATAIFA,nasikia baada ya muungano wakafanya mazingaombwe na kuwapokonya kiti chetu wa-ZANZIBAR na kukitumia wao,ingawa sina uhakika wa hili.naamini JF wapo wanaolijua hili,hebu tuwekeeni data.
 
Kwa ujinga wangu, wanzibari wanatuzidi sana sisi wa bara kwa habari ya uelewa wa kisiasa.

Mzee ES......

kule zenji ukiwaona watu wapo kool sana,lakini wanakusubiri siku ya KURA tu ndio utawajua wazenji wakoje.

mkuu inasemakana hata JKN hakuwahi hata usiku moja kulala zenji,huko pemba ndio kbs alikuwa anaenda na baada ya masaa machache anatimua.

1+1=3
 
Ninachotaka kuwaambia wanaJF ni kuwa muungano si kulazimishana au ubabe, ukweli utakuja onekana siku moja. Sisi muungano wetu una kasoro nyingi na fukuto ni kubwa sana, tunachofanya ni ku delay kuuvunja, ila utakuja vunjika tu.

Nyumba yoyote iliyojengwa kwenye foundation ya hewani, ni lazima ije anguka tu siku moja, lakini iliyojengwa mwambani hudumu milele!
 
Kilichobaki ni swali la wakati tu. Wakati utakapotimia muungano utakwisha. Ni kujidanganya kama mbuni anavyofunika kichwa chake akidhani haonekani. Kila kero moja ya muungano itakavyopatiwa ufumbuzi, nyingine itajitokeza. Itafikia mahali watu watasema tosha.
Zanzibar ina kila haki ya kupewa uhuru wake kama muungano hawautaki.
 
kalamu....

unajua suala hapa sio kuvununjika kwa muungano,unajua point kubwa ni lazima vipengele vifanyiwe marekebisho na kila mtu ajue mipaka yake.wananchi wapewe haki ya kujua utakua muungano wa aina gani,kwani tulianza na vipengele 4 nasikia lakini leo hii NEEMA ikiibuka znz basi inaingizwa kwenye muunganona sasa imekuwa vipngele zaidi ya 30 duh sio utani.

sijui leo hii al-marhum mzee abeidi amani karume akipewa dakika 1 afufuke akija duniani atasema nini kuhusu muungano.
 
Kwa ujinga wangu, wanzibari wanatuzidi sana sisi wa bara kwa habari ya uelewa wa kisiasa.

Mzee ES......

kule zenji ukiwaona watu wapo kool sana,lakini wanakusubiri siku ya KURA tu ndio utawajua wazenji wakoje.

mkuu inasemakana hata JKN hakuwahi hata usiku moja kulala zenji,huko pemba ndio kbs alikuwa anaenda na baada ya masaa machache anatimua.

1+1=3
unaweza ukawa right, kwani kuna kipindi cha uandikishaji mara moja nilitembelea tanzania bara na nilishangazwa nilipoona waandikishaji kura wanasinzia na hawana wa kumuandikisha na badili yake nikarejesha memory yangu zanzibar ambapo siku ya uandikishaji wapiga kura basi foleni zinasababisha baadhi ya barabara kufungwa na katika uandikishaji huo unashangazwa zaidi pale unapomuona mtoto wa miaka 14 na yeye yuko kwenye foleni anajizidisha umri almuradi tu apige kura. ila suali la kujiuliza. je wazenji hawa wana uelewa wa kisiasa kama hoja ilivyokuja hapo juu au wana ushabiki wa kisiasa?. nadhani siku wazenji watakayokuwa kitu kimoja hapo ndio watakuwa na uelewa wa kisiasa . kwani kwa sasa zanzibar kunahitajika "umoja" kulikoni u "cuf" na u "ccm".
 
Makubaliano ya muungano ya pitiwe tena wananchi wa pande zote mbili waambiwe nini cha kutegemea kutoka pande zote mbili, kusema kweli ukiniuliza mimi nini kilichofikiwa mpaka wakaunganisha tanganyika na zanzibar sijui.
Solution hapa ni serikali moja au serikali tatu lakini kwenye swala la serikali tatu gharama za serikali ya muungano zitagawanywa nusu kwa nusu? Sasa hapo napo nina uhakika lazima malalamiko yatatokea tu.

good point!je kama serikali 1 haikuwork out tutaelekea wapi?.nadhani kusuluhisha matatizo ya serikali 3 yakiibuka ni rahisi sana kulikoni serikali moja.nakubaliana na wewe ni gharama ila at least kutakuwa hakuna kunyoosheana vidole .sijui usijiunge na nani? sijui almasi tugawane ,au kwanini zanzibar wana balozi 5? na mengine mengi yanayosumbua vichwa vya watanzania.
 
Next election kuwe na referendum nchi nzima kuhusu muungano.This way tukipata simple majority both sides kwamba watu wanataka muungano muungano uendelee.Tukikosa simple majority muungano uvunjwe na Zanzibar iwe nchi.Kama kweli muungano ni wa watu hatuwezi kushindwa kupata 50% ya kura both sides ku support muungano.Ama sivyo tunaogopa nini kufanya referendum? Hii itakuwa na effect ya kumaliza for good kelele za legitimacy za muungano on the one hand or kuwapa watu uhuru wao on the other.
 
pundit.
hilo unaloongelea ndio only solution. na kama muungano utakubalika katika hiyo referendum pia kuwe na waraka ulio wazi kuhusu muungano kusiwe na kubabaishana mara leo unaambiwa hichi hakipo kwenye muungano ,ukilala ukiamka unaambiwa tayari kimeingizwa kwenye muungano jana na mheshimiwa kikwete au mkapa au karume.anyway lets hope 4 the best.
 
under_age,mtu wa pwani,...

..tulipoungana na miaka ya mwanzo ya muungano pande zote[bara && zenj] zilikuwa na hali nzuri ya kiuchumi. bara tulianzisha viwanda na zenj ilikuwa inatesa na karafuu.

..soko la karafuu lilipoanguka ndipo zenj ikaanza kuwa na hali mbaya. huku bara tuliua viwanda vyetu kwa kutumbukiza siasa kwenye manegement.

..siyo haki kusema kwamba Tanzania Bara, au Zenj, haiendelei kutokana na kuwa kwenye muungano. kuna kipindi nchi hizi zilistawi ndani ya muungano.

..SMZ wangekuwa wajanja wangejielekeza ktk kuanzisha viwanda. kuna soko kubwa sana Tanzania Bara, na Kenya wamekuwa wakifaidika nalo kwa muda mrefu.

..Biashara ya import-export toka Dubai ina faida kidogo sana kwa mwananchi wa kawaida wa Zenj.

..Bila Industrialization Zenj haitokaa kuona faida za huu Muungano.
 
Next election kuwe na referendum nchi nzima kuhusu muungano.......Hii itakuwa na effect ya kumaliza for good kelele za legitimacy za muungano on the one hand or kuwapa watu uhuru wao on the other.

Nakubaliana nawe kwa asilimia mia moja. Tatizo ni kuwa wengi tunajuwa jibu la hiyo referandum. CCM wanajua jibu, Serikali ya mapindizi kule Zanzibar wanajua jibu na pia Serikali ya muungano wanajua jibu- yaani matokeo ya hiyo referundum na ndiyo maana hata siku moja haitafanyika.

Si wana JF tunakumbuka Rwanda na Burundi walivyoingizwa kinyemela kwenye EAC?, wananchi wengi waliomba referundum, serikali ilikuwa inalifahamu vizuri jibu ya hiyo referundum na matokeo yake wakatumia ubabe wao na sasa ati Rwanda na Burundi ni member!

Ninachotaka kusema ni kuwa Serikali haiwezi kujifunga goli la wazi hivyo, jibu linafahamika na ndiyo maana referandum ya muungano haitofanyika kamwe, labda tupate rais kichwa maji sana katika awamu zijazo ndo anaweza kuchukua hiyo risk ya kupigia kura huu muungano wa maboksi!

Mkitaka mjue jinsi ambavyo pande zote zilivyouchoka muungano nyie angalieni tu hapa jinsi ambavyo watu wanatoleana macho!
 
Back
Top Bottom