Choveki,
Siyo kwamba wanaweza kufanya referendum na kupindua matokeo kama walivyomnyang'anya Seif urais wa Zanzibar? Mimi sioni tatizo ya CCM kupata simple majority bara, not even Unguja.Kazi iko Pemba huko.Labda Muungano uendelee Tanganyika na Unguja, Pemba wende zao ati yakhee!
Au hata watu wa Unguja hawataki muungano nao?
Now this is where Nyerere's vision becomes a reality.Wkijitenga Zanzibar kesho itakuwa Unguja na Pemba wanajitenga.Keshokutwa Kwaani sijui na Michenzani wanataka kuwa na rais na jamhuri zao, mwishowe kila baba mwenye wake wawili naye anatangaza jamhuri lol!
Ninachotaka kuwaambia wanaJF ni kuwa muungano si kulazimishana au ubabe, ukweli utakuja onekana siku moja. Sisi muungano wetu una kasoro nyingi na fukuto ni kubwa sana, tunachofanya ni ku delay kuuvunja, ila utakuja vunjika tu.
Nyumba yoyote iliyojengwa kwenye foundation ya hewani, ni lazima ije anguka tu siku moja, lakini iliyojengwa mwambani hudumu milele!
Mtu wa pwani......
niliwahi sikia kuwa TANGANYIKA walikuwa hawana KITI KTK UMOJA WA MATAIFA,nasikia baada ya muungano wakafanya mazingaombwe na kuwapokonya kiti chetu wa-ZANZIBAR na kukitumia wao,ingawa sina uhakika wa hili.naamini JF wapo wanaolijua hili,hebu tuwekeeni data.
Kitila,
nakuunga mkono...watanganyika hawadadisi kabisa haki zao ndani ya Muungano. Kwa mfano:-
..kwanini Tanzania Bara inalipa mishahara ya SMZ wakati waalimu wetu wanacheleweshewa malipo?
..kwanini SMZ haichangii ktk gharama za uendeshaji wa vyombo vya Muungano?
..kwanini wabunge wa Zanzibar wanachukua posho, wanashiriki na kupiga kura, ktk vikao vinavyojadili masuala ya Tanzania Bara?
..kwanini wazanzibari wanaendelea kuajiriwa/kuteuliwa ktk nafasi zisizo za Muungano?
..kwanini watanzania bara wanalazimika kutumia passport kuingia wanapokwenda Zanzibar, lakini Wazanzibari wanaingia Tanzania Bara kama msalani?
..kwanini wazanzibar wanaruhusiwa kupiga kura ktk chaguzi zetu lakini sisi haturuhusiwi kupiga kura ktk chaguzi zao?
..kwanini machangudoa kutoka Bara wanafukuzwa Zanzibar, lakini mashoga toka Zanzibar hawafukuzwi wanapoweka makazi huku Bara?
Choveki,
Siyo kwamba wanaweza kufanya referendum na kupindua matokeo kama walivyomnyang'anya Seif urais wa Zanzibar? Mimi sioni tatizo ya CCM kupata simple majority bara, not even Unguja.Kazi iko Pemba huko.Labda Muungano uendelee Tanganyika na Unguja, Pemba wende zao ati yakhee!
Au hata watu wa Unguja hawataki muungano nao?
Now this is where Nyerere's vision becomes a reality.Wkijitenga Zanzibar kesho itakuwa Unguja na Pemba wanajitenga.Keshokutwa Kwaani sijui na Michenzani wanataka kuwa na rais na jamhuri zao, mwishowe kila baba mwenye wake wawili naye anatangaza jamhuri lol!
Nijuavyo mimi tokea kuundwa kwa Bunge la Muungano hadi mwanzoni mwa miaka ya tisini, 'SHERIA YOYOTE INAYOHUSU MAMBO YA MUUNGANO, ILIHITAJI TWO THIRD YA WAJUMBE KUTOKA ZANZIBAR NA TWO THIRD YA WAJUMBE KUTOKA BARA'ili ipite. Lakini sasa SHERIA YOYOTE YA MUUNGANO INAHITAJI TWO THIRD YA WAJUMBE WOTE WA BUNGEili ipite.
Kama wajumbe wote wa sasa ni 320, na wajumbe kutoka Zanzibar hawazidi hata 70, je hata Wazanzibar wakiikataa sheria ndani ya Bunge si itapita tu coz hawa Wabara tayari wao wapo two third ya wajumbe wote wa Bunge. Muungano gani huu zaidi ya mauzauza!
wenye kujua zaidi forums hapa tupeni ukweli plz
A day will come
Chukua tano zako mkuu
The two countries were unified to form the United Republic of Tanganyika and Zanzibar on 26 April 1964, later changing its name to the United Republic of Tanzania on 1 November 1964, and have since been represented as one member.
Ndio sisi wengine tunaamini kwenye muungano wenye serikali tatu.
Wewe Bwana. Sasa nini kinagomba hapo. Kwani Ubalozi ni wa Tanganyika?yani kwenye balozi wawepo wajumbe wa serikali ya mapinduzi na serikali ya tanganyika balozi ndio anakua wa serikali ya muungano.
Mimi binafsi sioni kabisa sababu ya kukumbatia huu muungano Serikali ya mapinduzi ifanye tu ku declare kua wao ni serikali huru na wanavunja muungano rasimi.sasa sijui wanashindwa nini?