Haji Juma Omar: Mishahara Midogo kwa Walimu inachangia wengi wao kuishi kwa madeni

Haji Juma Omar: Mishahara Midogo kwa Walimu inachangia wengi wao kuishi kwa madeni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar, Haji Juma Omar amesema changamoto ya ulipaji wa mshahara mdogo kwa baadhi ya Walimu Zanzibar imesababisha kuwaingiza katika madeni makubwa na kusababisha kutafuta kazi nyingine za kuwaingizia vipato ili kuweza kujikimu.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa 9 wa Chama cha Walimu Zanzibar katika Ukumbi wa Taasisi ya Utalii Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja, amesema kutokana na maslahi ya Walimu kuwa ya chini kada hiyo imekuwa haiwavutii Wanafunzi wanaohitimu masomo yao na badala yake kuchagua taaluma nyingine kujifunza vyuo vikuu hali ambayo inaweka hatari hapo baadaye kwa kada hiyo kukosa walimu wa kutosha na kuteteresha hali ya utoaji wa elimu.

Omar ameomba kuongeza maslahi ya Walimu ili kuwavutia wanafunzi wengi kujifunza kada hiyo. Sambamba na hilo Omar amesema kumekuwa na matatizo kwa wajiri wa shule binafsi kuwanyanyasa kutofata sheria zilizopo za uwajiri walimu kutokuwapa mikataba na hata kushindwa kuwapelekea fedha katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
Hapo tatizo sio serikali bali walimu wenyewe.

Sasa unakuta mwalimu analazimishwa na mkurugenzi wa halmashauri tu anavalishwa kofia na fulana ya chama eti kwenda kukata viuno kushangilia mafanikio ya serikali na kwamba serikali imewafanyia kila kitu hawana deni nayo.

Sasa kama wahusika wameridhika na mshahara wanaolipwa unadhani serikali itakuwa na kiherehere cha kuwapa zaidi ya kile walichoridhika nacho?

Walimu kwa umoja wao kupitia viongozi wao wapaze sauti zao waboreshewe maslahi yao ili wasidhalilike na kudharauliwa mitaani kwa kuishi maisha duni.

Kuna kipindi nikiwa nasoma O'level pale home tulikuwa na duka la bidhaa mchanganyiko aise binafsi nilikuwa nawaandika walimu majina kwenye daftari vitu walivyokopa wakitegemea kulipa mwisho wa mwezi hadi nawaonea huruma.

Wengine walikuwa na madeni makubwa hayalipiki kwa kulimbikiza hadi wanakwepa duka wanaenda kuanzisha mkopo mwingine duka lingine.
 
Back
Top Bottom