Haji Manara: Ahmed Ally ni shabiki kindakindaki wa Yanga

Haji Manara: Ahmed Ally ni shabiki kindakindaki wa Yanga

Katika muendelezo wa tambo mbali mbali za Simba na Yanga pindi ukiotewa pale ambapo pana mshono hakika nawe lazima ukajipange kuja kurudisha mashambilizi.

Picha ya zamani ya Ahmed Ally akiwa ameshika kombe la Yanga sasa imetumiwa vizuri na Manara kwenye kuwaaminisha wananchi kuwa Ahmed naye pia ni mpenzi wa Yanga japo yupo Simba kwenye kujitafuta

Manara ameandika “Nakiri kwamba hata mimi wakati najitafuta, niliibukia kuwa Mfuasi feki wa Madunduka, na ilifika mahali nikawa nawacharura mno Yanga hadi mimi mwenyewe ilikuwa inanikera, lakini ndio kujitafuta huko, ningefanyaje ndugu zangu? Na bila kufanya hivyo GSM wangenionaje? Ile Siku waliyoniambia rudi home sasa, ooohh ilikuwa siku kubwa sana kwangu, SITASAHAU

Basi bhana Wakulungwa, ndio story ya huyu kijana mkazi wa Tambuka Reli, kelele na kebehi zote anazosema dhidi yetu, ichukuliwe ni kwenye kujitafuta na kujipapatua tu, huyu anaumwa na Yanga yake, hali hata Chakula siku Wananchi wakiwa wanacheza, Kigosi na Jimmy Mafufu waliwahi kuniambia walikuwa wanampa hadi hirizi kuvaa, siku ya mechi ya Yanga.

Miaka ya nyuma ilikuwa kila asubuhi anaenda Jangwani kubusu na kupiga picha na Makombe yetu, na akifika tu anaamkia, Shikamoo Makombe[emoji12] na Wazee wetu pale klabuni walikuwa wanampenda kwa ule usafi wake wa kusafisha kila siku Makombe yetu, hadi Jiki alikuwa anayaoshea.[emoji2957]

Kwa hiyo msameheni Wanayanga, anajitafuta tu, ni kijana wetu mzuri na ana msaada mkubwa kwetu, Mtu wa maana sana na ni familia kabisa, Soon Mtanielewa Wananchi”

View attachment 2942262
Amalizie kabisa kuwa GSM ni Simba damu damu.
 
Ushabiki wa Simba na yanga kwa Tanzania ni zaidi ya dini,

Unaweza kubadili dini lakini sio kushambulia timu nyingine, Mara nyingi Kama mapenzi wa Simba nimekuwa sipendezwi na baadhi ya Mambo au natumia pale tunapopoteza lakini sijawahi kuwaza nihame timu, angalia hili jukwaa wale unaowaona mashabiki kindakikindaki umewahi kusikia wanasema wamehama timu, ni wasanii Kama Manara ndio wanaweza kusema wanahama timu.
Ndio maana ugomvi wa jemedari na Manara ulianza pale jemedari alipokuja anacheza clip za nyuma za Manara kukumbusha kauli zake kuwa hata Kama atakabidhiwa pesa zote BOT hawezi kuhama Simba .
Labda umeanza kumsikia Manara baada ya kuwa msemaji wa Simba Ila story ya maisha yake imejaa utapeli ndio maana alifunguliea kesi na ikabidi ajiuzulu ukaribu mwenyezi wa ccm kwa sababu ya utapeli wa magari.
Namjua manara kiundani sana na hata huyo Ahmed ally namfahamu pia....point yangu nilikueleza kuwa manara,ahmed,alikiba,mkude,Canavaro hao wengi wao wametumikia timu hizo wakati huo mapenzi yao ya asili sio huko waliko....mfano GSM kiasili ni shabiki wa simba ila leo yupo yanga unadhani kwanini?
 
..
IMG-20240324-WA0001.jpg
 
Hivi Tangia kukua kwako umewahi kusikia mtu anahama ushabikinwa Simba na yanga?
Inategemea na mpunga,Manara alienda Yanga baada ya kufukuzwa Simba ili kuwakomoa akina Barbara,anatamani Simba ifanye vibaya ili awaambie watu kuwa Simba ilikuwa inafanya vizuri kwa sababu yake
 
Hii ya kwamba Drogba alikuwa mshabiki wa Arsenal hapa mkuu umetupiga
KuGUGO sio dhambi, mfanye google kuwa rafiki yako.

Drogba alikuwa ni supporter wa araenal hili ameshakili zaidi ya mara 1. Ila ilipokuja mipango ya kazi anapiga kazi.
Mie ni simba sports club kiushabiki ila naweza cheza yanga.
 
Katika muendelezo wa tambo mbali mbali za Simba na Yanga pindi ukiotewa pale ambapo pana mshono hakika nawe lazima ukajipange kuja kurudisha mashambilizi.

Picha ya zamani ya Ahmed Ally akiwa ameshika kombe la Yanga sasa imetumiwa vizuri na Manara kwenye kuwaaminisha wananchi kuwa Ahmed naye pia ni mpenzi wa Yanga japo yupo Simba kwenye kujitafuta

Manara ameandika “Nakiri kwamba hata mimi wakati najitafuta, niliibukia kuwa Mfuasi feki wa Madunduka, na ilifika mahali nikawa nawacharura mno Yanga hadi mimi mwenyewe ilikuwa inanikera, lakini ndio kujitafuta huko, ningefanyaje ndugu zangu? Na bila kufanya hivyo GSM wangenionaje? Ile Siku waliyoniambia rudi home sasa, ooohh ilikuwa siku kubwa sana kwangu, SITASAHAU

Basi bhana Wakulungwa, ndio story ya huyu kijana mkazi wa Tambuka Reli, kelele na kebehi zote anazosema dhidi yetu, ichukuliwe ni kwenye kujitafuta na kujipapatua tu, huyu anaumwa na Yanga yake, hali hata Chakula siku Wananchi wakiwa wanacheza, Kigosi na Jimmy Mafufu waliwahi kuniambia walikuwa wanampa hadi hirizi kuvaa, siku ya mechi ya Yanga.

Miaka ya nyuma ilikuwa kila asubuhi anaenda Jangwani kubusu na kupiga picha na Makombe yetu, na akifika tu anaamkia, Shikamoo Makombe[emoji12] na Wazee wetu pale klabuni walikuwa wanampenda kwa ule usafi wake wa kusafisha kila siku Makombe yetu, hadi Jiki alikuwa anayaoshea.[emoji2957]

Kwa hiyo msameheni Wanayanga, anajitafuta tu, ni kijana wetu mzuri na ana msaada mkubwa kwetu, Mtu wa maana sana na ni familia kabisa, Soon Mtanielewa Wananchi”

View attachment 2942262
images (16).jpeg

images (17).jpeg

images (13).jpeg
 
Canavaro yupi? Yule mzanzibari? Au unamaanisha Privadinho?
Mkuu haya mambo yapo tu mimi ni shabiki wa yanga ila mbona sisi tupo na canavaro wakati kiasili ni shabiki wa simba? Mbona yanga tunae haji manara wakati kila mtu anamjua ni simba damu? Na vipi mkude mbona kaitumikia simba kwa moyo wote hata kama ni yanga damu?namjua vizuri sana ahmed ally huyo ni yanga ila siamini kama anauwezo wa kuhujumu anapopatia ugali wake...manara ni mpuuzi mno mbona hamshangai bosi wetu GSM kuvaa jezi ya yanga wakati ni simba kindakindaki?
 
Hata Mohamed Mwameja ni Shabiki lia lia wa Yanga
 
Naona watu wanasahau kuwa Ahmed ni mwandishi. Na hii picha kwa haraka ni kipindi anajitafuta miaka hiyo. Hata hilo kombe ni la muda mrefu. Ukiwa mwandishi either unatumwa kuleta habari au unaenda kutafuta habari si jambo geni kupiga picha kama hizo.
Ukiona picha enzi zile za kina Isaac Gamba, Kitenge, Kibonde, Michuzi, Abou Liongo wanajitafuta utacheka
Ni sahihi pia haikatazwi kuwa shabiki wa Yanga huku ukiwa mfanyakazi wa Simba.
 
Back
Top Bottom