Haji Manara aitaka Clouds FM kuthibitisha au kuomba radhi juu ya habari yao kwamba Simba SC kapigwa 6-0 nchini Uturuki

Haji Manara aitaka Clouds FM kuthibitisha au kuomba radhi juu ya habari yao kwamba Simba SC kapigwa 6-0 nchini Uturuki

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amekiomba kituo cha redio cha Clouds FM kuthibitisha au kukanusha taarifa waliyoitangaza ya kuwa Klabu ya Simba imefungwa goli 6-0 katika mchezo wa kirafiki nchini Uturuki

Manara ameyasema hayo kupitia ukurasa wake mtandao katika wa Kijamii wa Instagram na kuongeza kuwa yeye kama msemaji kazi yake pia ni kulinda taswira ya klabu ya Simba na hayupo tayari kuona inaharibiwa

Aidha amesisitiza kuwa endapo habari hiyo haitakanushwa au kuthibitishwa basi itaaminika kuwa waliotanganza walikuwa na nia ovu ya kuidhalilisha Simba

Klabu ya Simba ipo nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2018/19 na ikiwa huko inaelezwa kuwa itacheza michezo kadhaa ya kirafiki
 
Kuna kila sababu ya habari hiyo kua Uongo.Timu imeenda Juzi tu J2 then J5 inacheza Mechi ya Kirafiki!!!!???Hiyo Cla uzi ni Radio uchwara
 
Msemaji ameenda na timu?
Timu imecheza friend match?
Matokeo yakoje?
Kama clouds imesema uongo, ukweli ni UPI?
 
Kuna kila sababu ya habari hiyo kua Uongo.Timu imeenda Juzi tu J2 then J5 inacheza Mechi ya Kirafiki!!!!???Hiyo Cla uzi ni Radio uchwara
kwani wanakaa muda gani huko hadi uone hizo siku mbili hazitoshi kucheza mechi!?..kula sauzi zile sita mlibiishaaa!
 
Mungu alivyo wa ajabu unaweza kuona kabla clouds hawajakanusha basi simba akapigwa sita kweli kweny hizo gem zake
 
walikuwa wanawashangaa waarabu sio...Uturuki ni middle east sio Ulaya..
 
Back
Top Bottom