sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Najaribu tu kuwaza,kwamba Klabu ya simba inalipa wachezaji, benchi la ufundi, n.k mamilioni ya pesa,ina mdhamini wake ni tajiri kabisa hapa Afrika lakini leo nimepigwa na bumbuwazi bada ya mambo kuwa wazi kwamba msemaji mkuu wa simba analipwa hela ndogo ambayo hailingani na hadhi na mchango wake ndani ya klabu, kumlipa manara laki 7 si haki hata kidogo.
semeni yoote lakini manara amekuwa wa faida sana simba, ameipambisha sana hiyo timu yenu na kuwatia moyo hata wakati mlipokuwa mnakata tamaa. kwahiyo mshahara kama ndio huo mnampa jueni anajitolea tu hapo. kuweni na utu. ondoeni mtu huyo mmuweke mwingine muone kama ataleta hamasa kama anazoleta huyo kwenye klab ya simba.
Nadhani hii ilikuwa ni kama bakora pale manara alipokataa kusaini mkataba wa milioni kuwa rasmi mwajiriwa wa simba, Ila manara hakuwa kichaa kuuacha huu mkataba, aliuacha mkataba kwasababu ungemfunga asipate dili kutoka makapuni mengine, Ikumbkwe kwa sasa licha ya manara kupokea hio laki 7 kutoka simba, bado ana mikataba minono kutoka gsm, bakhresa, asas, n.k hii mikataba imemfanikisha mpaka ana nyumba yake na gari zake, kiufupi hii mikataba inamlipa vizuri sana, Hio milioni 4 ya simba ilikuwa ni ofa nzuri lakini kitendo cha kumfunga manara asitoke nje ya simba hicho kipengere kingempunguzia manara mapato.
Hata simba inapocheza wengi huwa wanafatilia manara kasema nini wenye press confrence, mitandao ya jamii, n.k. wengine hata page za simba hawafatilii wao wanafata page ya manara wa updates zote za simba, manara ana followers weng kuzidi hata page za simba.mbaya zaidi simba ikifungwa iwe ni mtani ama klabu nyingine basi mtu wa kwanza kushambuliwa na hizo timu huwa ni manara, maana ni kama kitovu kikuu cha brand ya simba, hatashambuliwa mo, hatashambuliwa mchezaji, hatashambuliwa kocha, hatashambuliwa babra, ni manara ambae anashambuliwa.
Kinachoonekana wazi ni kuwa, viongozi wa Simba wakiongozwa na MO na Babra, hawapendezwi na Manara kufanya kazi na makampuni ya nje, wanataka manara afanye kazi za simba tu na kama mnavyojua simba mfadhili ni MO kwahio wanataka kumtega manara atangaze kampuni zinazotengeneza bodhaa za MO, hawataki manara afanye kazi kwa makampuni mengine kama kuwa balozi wa gsm, azam au asas, kwahio wakaamua kuutumia huo mshahara wa laki 7 kama bakora ya kukaidi ofa ya kitumwa.
Na hicho ndicho kimemponza.
anamapungufu yake lakini kazi anayofanya ni kubwa kwakweli......he deserves more