Haji Manara kulipwa mshahara laki 7 ni aibu na unyonyaji, arekebishiwe

Kwanza hakuna mshahara unaotosha. Pili yeye anajua hio Ndio stahili inaomfaa. Hivi ana diploma kweli au ana piga domodomo apate kwenda msalani.
Sasa anaondoka Simba aone kama hajaachwa tena na mke huyu.
Haya mambo ya kumlipa mtu mshahara kwa kuangalia vyeti badala ya kuangalia output ndo yanayolirudisha Taifa hili nyuma sana
 
Hivi Manara hiyo posho ya 700,000 ndo kanunua Harrier ?ndo anayokesha nayo Serena hotel? Alipigwa faini na TFF alipeleka cash mil 5,ye anaongea pumba akipigwa club inamsaidia kulipa faini,isitoshe ni mtu wa kutengeneza uhasama Kati ya club na media maana akiongea ni Kama anaisemea timu.

Huyu jamaa aondoke tu tumeijua Simba kabla ya yeye kutokwepo,utashangaa Simba ikishinda Kigoma ataanza kujikomba kwamba ilikuwa mind game ili tushinde ,asichokoze mashabiki next game anatafuta kuzomewa uwanjani ndo ajue wenye timu ni Nani na yeye wa kawaida tu
 
Unafahamu hata Mohamed Hussein na Shomari Kapombe pamoja na juhudi za kuibeba Simba kwenye matokeo ya uwanjani walikuwa wanapata mshahara wa sh. 2,000,000. Mpaka walipotishia wanahamia Yanga ndio wameongezewa. Kwa hiyo si ajabu Haji Manara kulipwa kiwango hicho cha laki 7.
 
Kuropoka tu Laki 7? Kuna watu wana bahati duniani!!
 
Ninachojua mshahara huwa unaendana na ELIMU/CV na sio huruma kuwa unafanya kazi sana au unaongea sana.
 
Laki saba ni hela ndogo sana kumlipa msemaji wa timu kama Haji.
 

Haji awe analipwa vizuri ili akikaa na wanayanga kama hivo asiwe na wasiwasi wala mawazo
 
Siku mishahara Yanga iwekwe hadharani Dah titatafutana akiyanani
Tuache ramli, yaani Manara haspati usingizi kila siku ni kuzimia zimia kwa ajili ya club afu wanamlipa laki saba. Huyu mhindi na vimada wake hapo Simba wanatafuna pesa tu. Hili halikubaliki.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Sijui umeongelea utani ama serious ila Instagram yake tu ina worth milioni 10 ama 20. Jamaa akitafuta Mtu wa kumshauri anaweza Ingiza hela kushinda hata vituo vya TV baadhi. Ana influence sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…