Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Manara: Sikuwa nataka baada ya kusomwa hukumu ile niseme lolote wala sio kawaida yangu lakini kwakuwa hukumu ile ilikuwa na mambo mengi ya kuchafua jina langu, kuharibu reputation na image yangu lakini ya kuififisha brand yangu ambayo nimeijenga kwa jasho jingi na kwa miaka mingi.
INAENDELEA...
Manara: Kwanza niwaeleze exacly nini kilitokea, nilikuwa nimekifumba wakati ule kwa nia tu kumaliza jambo lile kiungwana, kwa nia ya kujishusha ili mambo yamalizike katika mambo ya kiungwana.
Nilikuwepo mpirani kwenye mechi ile ya fainali, tulitangulia kufungwa goli na Coastal union na nilikaa katika eneo la wageni. Half time kama wengi mnanifahamu, mechi huwa siangalii dakika 90 nyingi tena zile ambazo bahati mbaya tunatangulia kufungwa, presha iko juu.
Half time nimeshawaambia vijana tushuke tuondoke, presha ilikuwa ishapanda.
========
Manara amedai akiwa anandoka uwanjani, mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella alimuita na akiwa anaongea naye, Rais wa TFF aliongea kwa ukali aondoke eneo hilo akidai amekufa mtu, Manara anasema mwili wa Wallace Karia ulikwa umeelekea kwa viongozi wa coastal union huku kidole kimeenda kwa Manara.
Manara anasema mkuu wa mkoa na viongozi wengine wakamtoa akaondoka lakini baadae akamfata alipo ndipo na yeye akapandisha.
Manara: Ilikuwa ni tukio baya sana lakini Mungu alinipa subra sikumjibu jibu lolote baya, baadae nikaondoka nikarudi, penati niliangalia nikiwa chumbani.. Tulipopata penati ya mwisho nikachukua gari nikarudi uwanjani, hoteli niliyofikia ilikuwa dakika tano.
Manara anadai Karia alimtaka akamuombe msamaha nyumbani kwake, wapige picha na azungumze na waandishi wa habari. Manara amesema picha aliyoweka mtandaoni ilipigwa na mtoto wa Karia.
Manara anadai Karia alimwambia maneno ambayo yeye Manara kinywa chake kuyatamka ni aibu. Alitamka kwamba watu wa Yanga wamepambana sana mechi ilikuwa ngumu kwenye nguo zao za ndani zina kinyesi.