Haji Manara: Mo alitaka niwe balozi wa bidhaa zake badala ya Azam. Asema Mo anadai hapati faida ilhali jezi za Simba zimejaa matangazo yake

Mtu anayemsema mwajiri wake aliyepita hadharani na kwa kashfa inakua ngumu sana kumuamini ili umuajiri.

Watu watasema "Kawapa makavu" "Kawapa live hajabakisha" ila ni maneno ambayo siyo msaada ukizingatia hili swala kufikia kesho litakua limeisha. Yaani katika sakata zima hili mwajiri mtarajiwa atakachoona ni "Huyu hafai, uswahili mwingi"
 
''Kaka yangu @hajismanara na kukumbusha tu riziki apangae ni mwenyezi Mungu sio Muhamedi au Babra na kila hatua Dua.You never know Mungu anakuepusha na nini na mbele kakupangia nini. Shukuru kwa Yote and Calm Down. Mlango mmoja ukifungwa mwingine uko wazi karibu Yanga kwa baba yako. Ulitukera sana lakini Mtoto akinyea mkono haukatwi. WELCOME BACK HOME'' @official_chidibeenz
 
Haja ipo tena kubwa Tu
Sasa ulitaka anyamaze watu tusijue?
Sifa ya uweledi si kuwa mahiri kwenye fani yako bali unatakiwa kuwa kifua cha kuficha madhaifu, kwa sehemu uliyokuwa unaifanyia kazi. Kesho inaweza ikatoka nafasi kubwa na yenye maslahi mapana kampuni ika kuhitaji tena.
 
Unajua taratibu za Uajiri Mkuu?

Taasisi au kampuni inatakiwa ikufanyie probation (kibarua) ndani ya miezi sita tu. Ikizidi inatakiwa kukupa mkataba
Siyo kanuni kwamba kipindi cha uangalizi kiwe miezi sita.

Yaweza kua hata wiki tu.

Isipokua ni kweli kwamba inatakiwa ukiwa eneo la kazi kwa muda huo inabidi ugewe mkataba na taasisi nyingi zinacounter hiki kipengele kwa ama kukufanyia review ambayo itaonyesha unahitaji uangalizi upya au kila ikitimia miezi sita wanatangaza nafasi za kazi tena na wewe unaomba na wanakuajiri tena na kukupa barua ya uangalizi tena.

Sasa kwa huyu hatujui ilikua wanaishije baada ya hiyo miezi sita.
 
Kipindi cha Uangalizi kisizidi miezi sita. Kama ameendelea kuwepo na alikuwa akilipwa posho ya laki saba maana yake tayari kanuni zimekiukwa. Utaratibu wa uajiri umepuuzwa.

Hivyo, mwajiri anawajibika.
Watamlipa tu Stahiki zake.
 
Mo naye anatakiwa kutueleza kama Simba ni kubwa kama anavyoamini kwanini anataka club iingie mkataba na bidhaa zake kwa milioni 200
 
Yani Mo kumfukuza Haji mpaka apitie kwa Senzo,huu ni uongo Haji ni muongo muongo sio wakuamini hata kidogo.
Kama angekua makini kwa uozo na mizengwe yote aliyoiona akiwa pale Simba kwanini hakusema kabla ya kufukuzwa?
Ataa ungekuwa wew ungesemaji maana MO alitaka asionekane mbaya kwa huyo mswahili
 
Mkuu nakuelewa sana.
 
"Bugati" katufumbua macho watu wengi hasa wale tuliokuwa hatumpendi . Ndio maana MO kila siku alikuwa anamsifia Mwendazake alielewa kwa dhati kuwa Mwendazake akiamua kufukunyua mambo pale clubuni hapatakalika....Tuache utani pamoja na kwamba sie washabiki tunataka makombe tu lakini tukatae tusikubali pale MO anatupiga vibaya...Manara ametumiwa tu watu wenye akili kuropoka ila wapo wengi wanaumia rohoni number moja ikiwa ni watu wa tume ya FCC
 
Baada ya kupiga uswahili amepata nini?'njaa imeisha au ataendelea kuitangaza GSM na kwingine,mwambieni huyo mswahili wenu huwezi kufanya kazi coca ukalipwa pepsi simply haiwezekani,hata hivyo wamemlea sana,miaka sita!!
 
Toka lini mukora akawa mwekezaji. Wacha inyeshe tuone panapovuja.
 
Sema huyo kaharibu watu wengi sana walimsihi tena waliokuwa wanamheshimu lakini najua kuanzia sasa watamuona ni snitch mtu mnafiki asiyeaminika wala si wa kujua jambo lako maana siku mkigombana atalisema. Mimi naona kunyamaza kwake kungemjenga sana na kuonekana mtu mwenye hekima.
 
IPO siku atakuja kuwageuka hao azam Kama ni kweli mbona kipindi chote hicho hakusema miaka sita hiyo unafanyiwa yote hayo uko kimya hapo azam amepata kwa sababu ya kuwa simba angeeleza na faida aliyopata ya yeye kuwa simba
 
Sifa ya uweledi si kuwa mahiri kwenye fani yako bali unatakiwa kuwa kifua cha kuficha madhaifu, kwa sehemu uliyokuwa unaifanyia kazi. Kesho inaweza ikatoka nafasi kubwa na yenye maslahi mapana kampuni ika kuhitaji tena.
Then Bora kaongea ili watu wajue kuwa msemaji wa timu anakwenda mkoani na timu Kwa gharama zake
 
Then Bora kaongea ili watu wajue kuwa msemaji wa timu anakwenda mkoani na timu Kwa gharama zake
Haji anajichanganya, this season simba imefanya dafari nyingi sana za nje na walikua wanafikia kwenye 5 star hotel, alishatuambia kua analipwa laki saba, kwa mshahara wa laki saba utalala 5 star hotel ipi? Safari za bongo zenyewe utaishia kupanda super champion wala sio BM au shabiby.
Manara ni kichwa maji hasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…