Haji Manara: Mo alitaka niwe balozi wa bidhaa zake badala ya Azam. Asema Mo anadai hapati faida ilhali jezi za Simba zimejaa matangazo yake

Haji Manara: Mo alitaka niwe balozi wa bidhaa zake badala ya Azam. Asema Mo anadai hapati faida ilhali jezi za Simba zimejaa matangazo yake

Mtu anayemsema mwajiri wake aliyepita hadharani na kwa kashfa inakua ngumu sana kumuamini ili umuajiri.

Watu watasema "Kawapa makavu" "Kawapa live hajabakisha" ila ni maneno ambayo siyo msaada ukizingatia hili swala kufikia kesho litakua limeisha. Yaani katika sakata zima hili mwajiri mtarajiwa atakachoona ni "Huyu hafai, uswahili mwingi"
 
''Kaka yangu @hajismanara na kukumbusha tu riziki apangae ni mwenyezi Mungu sio Muhamedi au Babra na kila hatua Dua.You never know Mungu anakuepusha na nini na mbele kakupangia nini. Shukuru kwa Yote and Calm Down. Mlango mmoja ukifungwa mwingine uko wazi karibu Yanga kwa baba yako. Ulitukera sana lakini Mtoto akinyea mkono haukatwi. WELCOME BACK HOME'' @official_chidibeenz
 
Haja ipo tena kubwa Tu
Sasa ulitaka anyamaze watu tusijue?
Sifa ya uweledi si kuwa mahiri kwenye fani yako bali unatakiwa kuwa kifua cha kuficha madhaifu, kwa sehemu uliyokuwa unaifanyia kazi. Kesho inaweza ikatoka nafasi kubwa na yenye maslahi mapana kampuni ika kuhitaji tena.
 
Unajua taratibu za Uajiri Mkuu?

Taasisi au kampuni inatakiwa ikufanyie probation (kibarua) ndani ya miezi sita tu. Ikizidi inatakiwa kukupa mkataba
Siyo kanuni kwamba kipindi cha uangalizi kiwe miezi sita.

Yaweza kua hata wiki tu.

Isipokua ni kweli kwamba inatakiwa ukiwa eneo la kazi kwa muda huo inabidi ugewe mkataba na taasisi nyingi zinacounter hiki kipengele kwa ama kukufanyia review ambayo itaonyesha unahitaji uangalizi upya au kila ikitimia miezi sita wanatangaza nafasi za kazi tena na wewe unaomba na wanakuajiri tena na kukupa barua ya uangalizi tena.

Sasa kwa huyu hatujui ilikua wanaishije baada ya hiyo miezi sita.
 
Siyo kanuni kwamba kipindi cha uangalizi kiwe miezi sita.

Yaweza kua hata wiki tu.

Isipokua ni kweli kwamba inatakiwa ukiwa eneo la kazi kwa muda huo inabidi ugewe mkataba na taasisi nyingi zinacounter hiki kipengele kwa ama kukufanyia review ambayo itaonyesha unahitaji uangalizi upya au kila ikitimia miezi sita wanatangaza nafasi za kazi tena na wewe unaomba na wanakuajiri tena na kukupa barua ya uangalizi tena.

Sasa kwa huyu hatujui ilikua wanaishije baada ya hiyo miezi sita.
Kipindi cha Uangalizi kisizidi miezi sita. Kama ameendelea kuwepo na alikuwa akilipwa posho ya laki saba maana yake tayari kanuni zimekiukwa. Utaratibu wa uajiri umepuuzwa.

Hivyo, mwajiri anawajibika.
Watamlipa tu Stahiki zake.
 
Shadeeya Mkuu iko hivi huo mkata wa 350 ml Kwa mwaka ilisainiwa na team zote mbili Yani Simba na Yanga mwaka 2020 kipindi CEO ni Senzo na sio Madam, Ila baada ya tathmini ya kina ya hizi team mbili pamoja na Azam ikaonekana kwamba wamepunjwa hivo ikawa inatakiwa kufanyiwa marekebisho

Yanga kafanya marekebisho yake ndio kaangukia hapo kwenye hizo billion zake ametulia, sasa Azam wanataka na Simba apewe hela Sawa na Yanga Ila Simba hawataki, kama ulismkia Mo majuzi kwenye press yake anasema Simba thamani yake ni kubwa hawezi kukubali akalipwa sawa na watani zake, yeye yupo nafasi ya 12 Africa iweje alipwe Sawa na club iliyopo nafasi ya 80 huko

So issue sio hiyo mil 350 issue ni hizo billion alizolamba Yanga kutaka na Simba apewe the same na Mo akasema siku Ile kama itashindikana Azam kuongeza hela basi atatoa yeye hela ingine kuliko kulipwa Sawa na watani zake, Kwa sasa Haji lengo lake ni kuharibu kwahiyo hawezi kuelezea vizuri, ye anapiga Tu mle ambapo anajua kuna mshono
Mo naye anatakiwa kutueleza kama Simba ni kubwa kama anavyoamini kwanini anataka club iingie mkataba na bidhaa zake kwa milioni 200
 
Yani Mo kumfukuza Haji mpaka apitie kwa Senzo,huu ni uongo Haji ni muongo muongo sio wakuamini hata kidogo.
Kama angekua makini kwa uozo na mizengwe yote aliyoiona akiwa pale Simba kwanini hakusema kabla ya kufukuzwa?
Ataa ungekuwa wew ungesemaji maana MO alitaka asionekane mbaya kwa huyo mswahili
 
Kwanza jamaa ni mvumilivu sana!!miaka sita unafanya kazi bila mkataba, halafu ukijitokeza mbele ya watu una kuwa na furaha kiasi kile??huku timu iko vizuri kiuchumi?!!mibonasi wanapewa wengine tu!!inawezekana manara ni msema hovyo lakini kwenye hili hapana ametoa majibu ya hoja zilizitolewa na Mo, Hans pop!!kosa lake ni nini?!!na kwasasa manara wala hawezi kukosa kazi hapa nchini, leo hata akiamua anze kazi ASAS, ama AZAM, anafanya.
Mkuu nakuelewa sana.
 
Aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu Kongwe ya Simba Sports Club leo hii anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya Masuala mbalimbali ikiwemo ya yeye kuondoshwa katika klabu ya Simba

Kuwa nami hapa kwa updates/kinachoendelea


--------------------------------------------
Ameanza kwa kuwasalimu wanahabari...
Anawaomba radhi wanahabari wote wakati anatekeleza majukumu yake, anasema kuwa yeye ni binadamu anakosea...


Anaendelea kusema...nanukuu

HAJI MANARA: Yanga kama watani zangu. Kuna wakati kweli nilizidisha utani. IM SORRY. Lengo langu lilikuwa kuongeza hamasa kwenye mpira. Mashabiki wengi wa Yanga waliokuwa wakinizodoa mitandaoni ndio waliokuwa wananiomba 'Selfie' uwanjani. Mpira sio Uadui, sina chuki na Yanga."

=> Vitu vilivyoniondoa Simba, moja ni Biashara na la pili ni Umaarufu. Sijui lini niliwahi kutamka mimi ni Mkubwa kuliko Simba. Wakati naanza kazi Simba niliambiwa nijitolee malipo yangefata baadae. Nilikubali huku nikijua aliyekuwepo kabla yangu alikuwa analipwa."

=> Msemaji niliyekuwa nafanya promo za mechi nilikuwa sikatiwi tiketi ya safari. Kote mlikokuwa mnaniona nilikuwa najitegemea kwa hela yangu mfukoni. Nilijitolea wakati wa shida, Neema ilipokuja Nikaonekana sifai

=>Senzo alipofika tu aliniambia moja ya jukumu alilopewa na mabosi ni kunifukuza kazi. Nikamuuliza kwanini? Akasema hakuna sababu, wanataka tu uondoke.

=> Mo alitaka nipewe mkataba niwe balozi wa bidhaa zake ili niache wa AZAM. Alimwambia Babra anipe mkataba lakini Babra alikaa miezi 6 bila kunipa. Alikuwa akipokea simu yangu anajibu tu 'I will call you back" halafu Anakata

=> Mo Dewji aliwahi kunipigia simu akaniambia watu wanasema nimekuwa maarufu kuliko yeye hivyo anataka kunitoa Simba

=> Babra alimpigia simu Diamond na kumwambia mtu pekee anayetakiwa kutajwa kwenye wimbo wa Simba ni MO peke yake. Diamond alikataa akawaambia njooni mchukue hela yenu, msinipangie kazi

=> Mo Dewji anasema hapati faida lakini mkiangalia jezi ya Simba ina matangazo mpaka ya Mo Foundation. Jezi imechafuka matangazo ya Mo kama timu za Sudan halafu mtu anasema hapati Faida.

=> Haji Manara amesema yeye ndiye aliyeanzisha kundi la Simba HQ ambalo lengo lake lilikua kuchangia pesa za bonasi za Wachezaji kipindi hicho Simba iko na hali mbaya.

=> Kundi hilo sasa ni kubwa sana linauwezo wa kuchanga zaidi ya Tsh milioni 30 kila mchezo wa Simba lakini leo hawataji kama ni hazina yake.

Pia kundi hilo hilo ndilo viongozi wa Simba wamesema amejiuzulu kupitia kundi hilo.

=> Mwezi wa kwanza mwaka huu (2021) tarehe 5 na mkataba ninao, Simba kupitia CEO Babra wamesaini na Azam mkataba utakaoisha msimu wa 2022/2023 wa Tsh milioni 385 kwa mwaka, Kashembe aliisema mahali lakini labda mlikuwa hamjaielewa vizuri. - Haji Manara.

CEO Babra toka ameingia ameishafukuza Wafanyakazi viongozi tisa mimi ni wa kumi. - Haji Manara.

=> Hatupo hapa bila Azam Tv, leo mpira umechangamka ligi ya Tanzania kwasababu ya Azam TV. Nilirudi wakati niko simba na narudia wakati sipo Simba.

=> Haji anasema mkataba ambao Hans Pope aliuzungumzia wa milioni nne ulikuja baada ya Mo Dewji kuomba Haji ampelekee mkataba wake wa kibiashara na kampuni ya Azam na hapo akiwa tayari ameitumikia klabu kwa miaka sita bila kuwa na mkataba.

=> Kwenye mkataba huo wa Azam ambao aliupeleka ulikuwa na kipengele kinachotaka kiasi cha shilingi milioni mia tatu hamsini kulipwa ili mkataba uvunjwe, Haji anasema sharti hilo ndilo lililopelekea Simba Sc kumuandalia mkataba ambao haukufikia kiasi cha shilingi milioni nne ukiwa na sharti la kutomtaka kufanya biashara na kampuni nyingine yoyote sipokuwa Mohamed Enterprises.

=> Simba tusikubali kudanganywa,bilion 21 tulizoambiwa zimetumika ni deni"

"Chuki yake kwa Azam ndiyo asili ya kunitengenezea mimi mtego wa kuihujumu timu" Manara.

"Nimeweka akiba mengine ninayo mengi kwasababu najua watatuma watu"
"Ipo siku haki ya Simba itarejea,
huwezi kuwaongopea watu siku zote ,utawaongopea katika kipindi kifupi tuu" MANARA

Anaendelea kufunguka

MANARA: MIAKA 6 BILA MKATABA

Haji Manara amesema mara nyingi uongozi wa Simba SC haukuwa ukimsafirisha kwenda kwenye michezo ndani na nje ya nchi, hivyo ilimbidi kujigharamia. Amesema kwa miaka sita amefanya kazi bila mkataba na posho, lakini alifanya sababu anaipenda Simba. Kuna kipindi alikuwa akilazwa kwenye makochi anakumbushia mechi ya Mbabane Swaziland
"Bugati" katufumbua macho watu wengi hasa wale tuliokuwa hatumpendi . Ndio maana MO kila siku alikuwa anamsifia Mwendazake alielewa kwa dhati kuwa Mwendazake akiamua kufukunyua mambo pale clubuni hapatakalika....Tuache utani pamoja na kwamba sie washabiki tunataka makombe tu lakini tukatae tusikubali pale MO anatupiga vibaya...Manara ametumiwa tu watu wenye akili kuropoka ila wapo wengi wanaumia rohoni number moja ikiwa ni watu wa tume ya FCC
 
Chezea mutoto ya mujini wewe!
Unaweza ukawa na mielimu yako, mipesa yako, lakini ukazidiwa talanta na mtoto wa mjini.

Tulio zaliwa Dar- es Salam mikono juu.

Wa mikoani endeleeni kutuita "waswahili" lakini ndio hivyo tena, bila kuja kwetu nyinyi ni bure.
Baada ya kupiga uswahili amepata nini?'njaa imeisha au ataendelea kuitangaza GSM na kwingine,mwambieni huyo mswahili wenu huwezi kufanya kazi coca ukalipwa pepsi simply haiwezekani,hata hivyo wamemlea sana,miaka sita!!
 
Huyu Haji na waliomtuma ni hovyo sana, na kajichanganya sana.

Kashashindwa. Simba sct msimjibu. Mwacheni abwabwaje mpaka aridhike na roho yake. Hana Nia njema na Simba na anaombea ipate mabalaa. Eti anaongea na mashabiki!

Azam nao kumbe ovyo sana kumtuma huyo ili kutangaza TV yao ndo nn sasa. Simba achaneni na Azam, ukimsoma vizuri manara kila mara Azam tv ndo waliomtuma kutukana live!

Serikali kwa nn mtu huyu atukane muwekezaji tena live kabisa?
Toka lini mukora akawa mwekezaji. Wacha inyeshe tuone panapovuja.
 
Sema huyo kaharibu watu wengi sana walimsihi tena waliokuwa wanamheshimu lakini najua kuanzia sasa watamuona ni snitch mtu mnafiki asiyeaminika wala si wa kujua jambo lako maana siku mkigombana atalisema. Mimi naona kunyamaza kwake kungemjenga sana na kuonekana mtu mwenye hekima.
 
IPO siku atakuja kuwageuka hao azam Kama ni kweli mbona kipindi chote hicho hakusema miaka sita hiyo unafanyiwa yote hayo uko kimya hapo azam amepata kwa sababu ya kuwa simba angeeleza na faida aliyopata ya yeye kuwa simba
 
Sifa ya uweledi si kuwa mahiri kwenye fani yako bali unatakiwa kuwa kifua cha kuficha madhaifu, kwa sehemu uliyokuwa unaifanyia kazi. Kesho inaweza ikatoka nafasi kubwa na yenye maslahi mapana kampuni ika kuhitaji tena.
Then Bora kaongea ili watu wajue kuwa msemaji wa timu anakwenda mkoani na timu Kwa gharama zake
 
Then Bora kaongea ili watu wajue kuwa msemaji wa timu anakwenda mkoani na timu Kwa gharama zake
Haji anajichanganya, this season simba imefanya dafari nyingi sana za nje na walikua wanafikia kwenye 5 star hotel, alishatuambia kua analipwa laki saba, kwa mshahara wa laki saba utalala 5 star hotel ipi? Safari za bongo zenyewe utaishia kupanda super champion wala sio BM au shabiby.
Manara ni kichwa maji hasa
 
Back
Top Bottom