secret file
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 5,843
- 8,637
Masikini anapambana na tajiri pakali hapa....Aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu Kongwe ya Simba Sports Club leo hii anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya Masuala mbalimbali ikiwemo ya yeye kuondoshwa katika klabu ya Simba
Kuwa nami hapa kwa updates/kinachoendelea
--------------------------------------------
Ameanza kwa kuwasalimu wanahabari...
Anawaomba radhi wanahabari wote wakati anatekeleza majukumu yake, anasema kuwa yeye ni binadamu anakosea...
Anaendelea kusema...nanukuu
"Yanga kama watani zangu. Kuna wakati kweli nilizidisha utani. IM SORRY. Lengo langu lilikuwa kuongeza hamasa kwenye mpira. Mashabiki wengi wa Yanga waliokuwa wakinizodoa mitandaoni ndio waliokuwa wananiomba 'Selfie' uwanjani. Mpira sio Uadui, sina chuki na Yanga."
----------‐---------------------------------
"Vitu vilivyoniondoa Simba, moja ni Biashara na la pili ni Umaarufu. Sijui lini niliwahi kutamka mimi ni Mkubwa kuliko Simba. Wakati naanza kazi Simba niliambiwa nijitolee malipo yangefata baadae. Nilikubali huku nikijua aliyekuwepo kabla yangu alikuwa analipwa."
Haji Manara
--------------------------------------------
"Msemaji niliyekuwa nafanya promo za mechi nilikuwa sikatiwi tiketi ya safari. Kote mlikokuwa mnaniona nilikuwa najitegemea kwa hela yangu mfukoni. Nilijitolea wakati wa shida, Neema ilipokuja Nikaonekana sifai"
Haji Manara
--------------------------------------------
"Senzo alipofika tu aliniambia moja ya jukumu alilopewa na mabosi ni kunifukuza kazi. Nikamuuliza kwanini? Akasema hakuna sababu, wanataka tu uondoke."
Haji Manara
--------------------------------------------
"Mo alitaka nipewe mkataba niwe balozi wa bidhaa zake ili niache wa AZAM. Alimwambia Babra anipe mkataba lakini Babra alikaa miezi 6 bila kunipa. Alikuwa akipokea simu yangu anajibu tu 'I will call you back" halafu Anakata"
Haji Manara
--------------------------------------------
"Mo Dewji aliwahi kunipigia simu akaniambia watu wanasema nimekuwa maarufu kuliko yeye hivyo anataka kunitoa Simba"
Haji Manara
--------------------------------------------
"Babra alimpigia simu Diamond na kumwambia mtu pekee anayetakiwa kutajwa kwenye wimbo wa Simba ni MO peke yake. Diamond alikataa akawaambia njooni mchukue hela yenu, msinipangie kazi"
Haji Manara
---------------------------------------------
"Mo Dewji anasema hapati faida lakini mkiangalia jezi ya Simba ina matangazo mpaka ya Mo Foundation. Jezi imechafuka matangazo ya Mo kama timu za Sudan halafu mtu anasema hapati Faida."
Haji Manara
---------------------------------------------
Haji Manara amesema yeye ndiye aliyeanzisha kundi la Simba HQ ambalo lengo lake lilikua kuchangia pesa za bonasi za Wachezaji kipindi hicho Simba iko na hali mbaya.
Kundi hilo sasa ni kubwa sana linauwezo wa kuchanga zaidi ya Tsh milioni 30 kila mchezo wa Simba lakini leo hawataji kama ni hazina yake.
Pia kundi hilo hilo ndilo viongozi wa Simba wamesema amejiuzulu kupitia kundi hilo.
--------------------------------------------
Mwezi wa kwanza mwaka huu (2021) tarehe 5 na mkataba ninao, Simba kupitia CEO Babra wamesaini na Azam mkataba utakaoisha msimu wa 2022/2023 wa Tsh milioni 385 kwa mwaka, Kashembe aliisema mahali lakini labda mlikuwa hamjaielewa vizuri. - Haji Manara.
--------------------------------------------
CEO Babra toka ameingia ameishafukuza Wafanyakazi viongozi tisa mimi ni wa kumi. - Haji Manara.
Hatupo hapa bila Azam Tv, leo mpira umechangamka ligi ya Tanzania kwasababu ya Azam TV. Nilirudi wakati niko simba na narudia wakati sipo Simba.
--------------------------------------------
Haji anasema mkataba ambao Hans Pope aliuzungumzia wa milioni nne ulikuja baada ya Mo Dewji kuomba Haji ampelekee mkataba wake wa kibiashara na kampuni ya Azam na hapo akiwa tayari ameitumikia klabu kwa miaka sita bila kuwa na mkataba.
Kwenye mkataba huo wa Azam ambao aliupeleka ulikuwa na kipengepe kinachotaka kiasi cha shilingi milioni mia tatu hamsini kulipwa ili mkataba uvunjwe, Haji anasema sharti hilo ndilo lililopelekea Simba Sc kumuandalia mkataba ambao haukufikia kiasi cha shilingi milioni nne ukiwa na sharti la kutomtaka kufanya biashara na kampuni nyingine yoyote sipokuwa Mohamed Enterprises.
--------------------------------------------
"Simba tusikubali kudanganywa,bilion 21 tulizoambiwa zimetumika ni deni"
"Chuki yake kwa Azam ndiyo asili ya kunitengenezea mimi mtego wa kuihujumu timu" Manara.
"Nimeweka akiba mengine ninayo mengi kwasababu najua watatuma watu"
"Ipo siku haki ya Simba itarejea,
huwezi kuwaongopea watu siku zote ,utawaongopea katika kipindi kifupi tuu" MANARA
-----------------------------------
Anaendelea kufunguka
MANARA: MIAKA 6 BILA MKATABA
Haji Manara amesema mara nyingi uongozi wa Simba SC haukuwa ukimsafirisha kwenda kwenye michezo ndani na nje ya nchi, hivyo ilimbidi kujigharamia. Amesema kwa miaka sita amefanya kazi bila mkataba na posho, lakini alifanya sababu anaipenda Simba. Kuna kipindi alikuwa akilazwa kwenye makochi anakumbushia mechi ya Mbabane Swaziland
Manara wamalize hao.....
watajua hawajui public sympathy ipo upande wako