Haji Manara: Mo alitaka niwe balozi wa bidhaa zake badala ya Azam. Asema Mo anadai hapati faida ilhali jezi za Simba zimejaa matangazo yake

Haji Manara: Mo alitaka niwe balozi wa bidhaa zake badala ya Azam. Asema Mo anadai hapati faida ilhali jezi za Simba zimejaa matangazo yake

Hua najiuliza mara kwa mara; katika masuala ya uwekezaji wa Hisa. Mwenye maamuzi makubwa ni yule mwenye hisa nyingi au? ukiangalia ata timu za wenzetu huko majuu.
Huku kwetu mbona Mo akiye na hisa 49% ananguvu kuliko Simba yenye 51%ni kwanini?
Inafikirisha sana.
MO as individual ana hisa 49, nani mwengine Mwenye hisa zaidi ya MO pale? 51 zilizobaki zinamilikiwa na Wanachama kwa pamoja, but kwa mmoja mmoja unadhan watakua wana % ngapi?

Yaan tuseme Wanachama 1,000,000 wa Simba wanamiliki jumla ya hisa 51% za Simba, je kila mmoja wao anamiliki % ngapi hapo? Na huyo kila mmoja Mwenye hizo % utakazopata hapo juu atamzidi MO Mwenye 49?
 
Manara totally mswahili +mzaramo kuna haja gani ya kuongea yote haya, yaani leo ndio kaharibu reputation yake yote na ile sifa yake ya kujitamba eti ana UWELEDI mkubwa leo kajishusha mpaka chekechea.

Haya watani pamabaneni na SEMAJI LENU aka Buggati,mpaka hapo kawavua nguo kwamba timu yenu ina tatizo la management kwani mambo aliyo yasema ni kweli sababu yy alikuwa jikoni.
Tuombe Radhi Waswahili na Wazaramo Haji ni mtu wa Kigoma ila Wa Manyema wamekuja mjini mapema sana mfano msikiti wa Manyema umejengwa mwaka 1922...
 
Aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu Kongwe ya Simba Sports Club leo hii anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya Masuala mbalimbali ikiwemo ya yeye kuondoshwa katika klabu ya Simba

Kuwa nami hapa kwa updates/kinachoendelea


--------------------------------------------
Ameanza kwa kuwasalimu wanahabari...
Anawaomba radhi wanahabari wote wakati anatekeleza majukumu yake, anasema kuwa yeye ni binadamu anakosea...


Anaendelea kusema...nanukuu

HAJI MANARA: Yanga kama watani zangu. Kuna wakati kweli nilizidisha utani. IM SORRY. Lengo langu lilikuwa kuongeza hamasa kwenye mpira. Mashabiki wengi wa Yanga waliokuwa wakinizodoa mitandaoni ndio waliokuwa wananiomba 'Selfie' uwanjani. Mpira sio Uadui, sina chuki na Yanga."

=▷Vitu vilivyoniondoa Simba, moja ni Biashara na la pili ni Umaarufu. Sijui lini niliwahi kutamka mimi ni Mkubwa kuliko Simba. Wakati naanza kazi Simba niliambiwa nijitolee malipo yangefata baadae. Nilikubali huku nikijua aliyekuwepo kabla yangu alikuwa analipwa."

=▷ Msemaji niliyekuwa nafanya promo za mechi nilikuwa sikatiwi tiketi ya safari. Kote mlikokuwa mnaniona nilikuwa najitegemea kwa hela yangu mfukoni. Nilijitolea wakati wa shida, Neema ilipokuja Nikaonekana sifai

=▷ Senzo alipofika tu aliniambia moja ya jukumu alilopewa na mabosi ni kunifukuza kazi. Nikamuuliza kwanini? Akasema hakuna sababu, wanataka tu uondoke.

=▷ Mo alitaka nipewe mkataba niwe balozi wa bidhaa zake ili niache wa AZAM. Alimwambia Babra anipe mkataba lakini Babra alikaa miezi 6 bila kunipa. Alikuwa akipokea simu yangu anajibu tu 'I will call you back" halafu Anakata

=▷ Mo Dewji aliwahi kunipigia simu akaniambia watu wanasema nimekuwa maarufu kuliko yeye hivyo anataka kunitoa Simba

=▷ Babra alimpigia simu Diamond na kumwambia mtu pekee anayetakiwa kutajwa kwenye wimbo wa Simba ni MO peke yake. Diamond alikataa akawaambia njooni mchukue hela yenu, msinipangie kazi

=▷ Mo Dewji anasema hapati faida lakini mkiangalia jezi ya Simba ina matangazo mpaka ya Mo Foundation. Jezi imechafuka matangazo ya Mo kama timu za Sudan halafu mtu anasema hapati Faida.

=▷ Haji Manara amesema yeye ndiye aliyeanzisha kundi la Simba HQ ambalo lengo lake lilikua kuchangia pesa za bonasi za Wachezaji kipindi hicho Simba iko na hali mbaya.

=▷ Kundi hilo sasa ni kubwa sana linauwezo wa kuchanga zaidi ya Tsh milioni 30 kila mchezo wa Simba lakini leo hawataji kama ni hazina yake.

Pia kundi hilo hilo ndilo viongozi wa Simba wamesema amejiuzulu kupitia kundi hilo.

=> Mwezi wa kwanza mwaka huu (2021) tarehe 5 na mkataba ninao, Simba kupitia CEO Babra wamesaini na Azam mkataba utakaoisha msimu wa 2022/2023 wa Tsh milioni 385 kwa mwaka, Kashembe aliisema mahali lakini labda mlikuwa hamjaielewa vizuri. - Haji Manara.

CEO Babra toka ameingia ameishafukuza Wafanyakazi viongozi tisa mimi ni wa kumi. - Haji Manara.

=> Hatupo hapa bila Azam Tv, leo mpira umechangamka ligi ya Tanzania kwasababu ya Azam TV. Nilirudi wakati niko simba na narudia wakati sipo Simba.

=> Haji anasema mkataba ambao Hans Pope aliuzungumzia wa milioni nne ulikuja baada ya Mo Dewji kuomba Haji ampelekee mkataba wake wa kibiashara na kampuni ya Azam na hapo akiwa tayari ameitumikia klabu kwa miaka sita bila kuwa na mkataba.

=> Kwenye mkataba huo wa Azam ambao aliupeleka ulikuwa na kipengele kinachotaka kiasi cha shilingi milioni mia tatu hamsini kulipwa ili mkataba uvunjwe, Haji anasema sharti hilo ndilo lililopelekea Simba Sc kumuandalia mkataba ambao haukufikia kiasi cha shilingi milioni nne ukiwa na sharti la kutomtaka kufanya biashara na kampuni nyingine yoyote sipokuwa Mohamed Enterprises.

=> Simba tusikubali kudanganywa,bilion 21 tulizoambiwa zimetumika ni deni"

"Chuki yake kwa Azam ndiyo asili ya kunitengenezea mimi mtego wa kuihujumu timu" Manara.

"Nimeweka akiba mengine ninayo mengi kwasababu najua watatuma watu"
"Ipo siku haki ya Simba itarejea,
huwezi kuwaongopea watu siku zote ,utawaongopea katika kipindi kifupi tuu" MANARA

Anaendelea kufunguka

MANARA: MIAKA 6 BILA MKATABA

Haji Manara amesema mara nyingi uongozi wa Simba SC haukuwa ukimsafirisha kwenda kwenye michezo ndani na nje ya nchi, hivyo ilimbidi kujigharamia. Amesema kwa miaka sita amefanya kazi bila mkataba na posho, lakini alifanya sababu anaipenda Simba. Kuna kipindi alikuwa akilazwa kwenye makochi anakumbushia mechi ya Mbabane Swaziland

=▷Zile promotion zote nilizokuwa nazifanya Sijawahi kupata posho wala bonus yoyote kutoka Simba, na mara baada ya kusema haya najua watanitengenezea risiti feki nasema haya hili mjue kile kilichotokea Simba kiliniumiza kiasi gani? - Haji Manara

≒▷Senzo alipoingia akaniita ofisini akaniambia moja ya kazi yangu ya kwanza ni kukuondoa wewe ofisini lakini mimi nimewakatalia kwa sababu sijawahi kufanya kazi na wewe na alifanya kazi na mimi miezi miwili akaona msaada wangu

Senzo alifanyiwa figusi baadae uvumilivu ukamshinda Yanga wakampa ofa nzuri akaondoka na kiukweli niliumia sana nikaona nimeshaisha na nikalia sana- Haji Manara


“Waliniita ofisini nikaenda wakaniambia jana ulionekana umeenda kigamboni Kwa Ghalibu kutuhujumu, walinionyesha simu inayoonyesha kuwa nilikuwa Kigamboni lakini nilipoangalia tarehe ilinionyesha ilikuwa tarehe 7 muone jinsi hawa watu walivyokuwa wananichukia,” -Haji manara
Manara ni mpumbavu sana na kwa kauli yake anaonekana ni kijana mwenye chuki na roho mbaya. Barbara ilibidi afukuze kazi viongozi wabovu ndani ya club ili Club iendeshwe kisasa zaidi maana kabla yake kwa kweli Simba ilioza kwani wale viongozi walikuwa walaji tu na hawakuwa pale kwa ajili ya kusaidia timu. Simba ilifanya kosa sana kumuajiri Manara kwani yule dogo ni mpuuzi mno na muongo sana.
 
Huyu mpuuzi MO anataka kujiuzuru,

Sijawahi kuona tajiri mjinga mjinga kama huyu asee

Tajiri gani usiyetaka kuhojiwa?

Mzee kilomoni aliona mbali mno

Au anajua wanachama wa Simba ni wajinga wajinga tu asee

Kila siku unalalama hupati faida, kwanini bado uko Simba?

Inabidi tuanze kuhoji mapato na matumizi, ili kama ni kweli unapata hasara tukushauli uondoke.
Mo anasusasusa Kama demu bhana[emoji1787][emoji1787]

Yaani manara wa kumkosesha usingizi Mo

Halafu hivi huyo No hajui trend ya matukio ya kitanzania siku hizi .

Mambo yanakuja na upepo na yanapita Hali inakuwa shwari.

Anyway wote ni CCM acha wanyukane[emoji1787]
 
Aongee mpaka anabinuka lakin Simba ni kubwa kuliko yeye...nje ya Simba Manara hamna kitu
 
Hadi wachezaji ni weusi na wananamikataba huyu haji ni pumbavu
Kuna watu wajinga..

Chama analipwa mshahara milion 12
Kagere milion 11

Wale wakina ndemla na hajibu milion 3 na 4

Halafu anakuja mtu kuongea ujinga
 
Yani Mo kumfukuza Haji mpaka apitie kwa Senzo, huu ni uongo Haji ni muongo muongo sio wakuamini hata kidogo.

Kama angekuwa makini kwa uozo na mizengwe yote aliyoiona akiwa pale Simba kwanini hakusema kabla ya kufukuzwa?
Alikuwa analinda kibaru saiz hana cha kupoteza mbona hujiongezi mkubwa
 
Huyu mpuuzi MO anataka kujiuzuru,

Sijawahi kuona tajiri mjinga mjinga kama huyu asee

Tajiri gani usiyetaka kuhojiwa?

Mzee kilomoni aliona mbali mno

Au anajua wanachama wa Simba ni wajinga wajinga tu asee

Kila siku unalalama hupati faida, kwanini bado uko Simba?

Inabidi tuanze kuhoji mapato na matumizi, ili kama ni kweli unapata hasara tukushauli uondoke.
Kipimo cha mpuuzi na asiye mpuuzi ni fwedhaaa!

Hakuna tajiri mjinga. Mjinga hawezi kuwa tajiri.

Yaani uwe unazo akili alafu usizitumie kupata pesa hizo akili ni za nini sasa!?

Mo sio mjinga kwa sababu ni tajiri. Wewe ni tajiri!? Ushaona sasa kati yako wewe na Mo nani mjinga!?

Alafu sio 'kujiuzuru' jifunze kuandika vizuri Topolo mmoja wewe
 
Kipimo cha mpuuzi na asiye mpuuzi ni fwedhaaa!

Hakuna tajiri mjinga. Mjinga hawezi kuwa tajiri.

Yaani uwe unazo akili alafu usizitumie kupata pesa hizo akili ni za nini sasa!?

Mo sio mjinga kwa sababu ni tajiri. Wewe ni tajiri!? Ushaona sasa kati yako wewe na Mo nani mjinga!?

Alafu sio 'kujiuzuru' jifunze kuandika vizuri Topolo mmoja wewe
Hata wewe na ujinga wako ungekua kwenye family ya Dewji tungekuita tajiri!

Umegundua sasa kua kuna matajiri wajinga?
 
Hata wewe na ujinga wako ungekua kwenye family ya Dewji tungekuita tajiri!

Umegundua sasa kua kuna matajiri wajinga?
".... unge.... tunge..." yaani umejaa wishful thinking za kijinga jinga tupu.

Kwa hiyo hapo ndio unajiona 'umeprove' kwamba matajiri wajinga wapo [emoji1787]

Coach Luc aishi sana. Gongowazi wahed wewe
 
".... unge.... tunge..." yaani umejaa wishful thinking za kijinga jinga tupu.

Kwa hiyo hapo ndio unajiona 'umeprove' kwamba matajiri wajinga wapo [emoji1787]

Coach Luc aishi sana. Gongowazi wahed wewe
Kwenda zenu na huyo tajiri poli wenu,

Tajiri gani kila siku unasubiri free agents ndo Usajili.
 
Mo alikuwa analalamika udhamini wa sportPesa wa 1B kwa mwaka ni kidogo wakati yeye ameichafua jezi ya Simba kwa 200M kwa mwaka.

Wanasimba wengi wamekauka kwasababu tunashinda mataji na ukijaribu kuhoji unazimwa papo hapo.
Wote tunaipenda Simba linapokuja swala la maslahi ya Simba ushabiki inabidi tuweke pembeni
 
Kwenda zenu na huyo tajiri poli wenu,

Tajiri gani kila siku unasubiri free agents ndo Usajili.
Huna hoja [emoji1787]

Unataka tukuorozeshee sajili ambazo sio 'free agent' sasa

Nyie mnaovunja mikataba mbn mmeishia kushinda vikombe vya mbuzi huko visiwani mwaka wa nne huu. Na kagame hii pia hampati

Sare sare maua FC nyie.
 
Kuna cha kujifunza hapa mikataba mingi tunasaini kwa uchu wa pesa na njaa kali ukisoma kara nyingi nyingi unastukia kitu...

 
Ila washabiki wa uto mnakazi sana miaka 4 bila kombe sio mchezo lazma chochote kitu kutoka simba mkidakie na mnasahau ku focus kwenye kujenga team yenu
 
Tuassume kuwa yote aliyoyasema manara ni kweli hakuna, hata uongo mmoja bado yeye ndio mwenye matatizo......
nililala kwenye makochi_ asa tangu lini team zina safiri na wasemaji kwenda nje ya nchi? We wako wanahabari kaa nyumbani usubirie press.
Walimkataza Mond asinitaje_ Yes usitajwe kama mtu amelipa hela wimbo utengenezwe maanake kuna aina ya maudhui anayahitaji....., wimbo wa timu unatakiwa kudumu miaka na miaka, why tuanze kutaja msemaji wa timu ili iwaje?, msemaji wa team kimekuwa cheo kikubwa kiasi hicho?
Mo anachukia bakhresa atakuwa mkubwa kuliko yeye_Yes ni washindani sidhani hata kama bakhresa anapenda kuzidiwa na MO kawaida sana hii.
Hapati faida wakati team imejaa matangazo_ hayo matangazo si analipia kwani anatangaza bure? Mfano Kale kanembo ka MO extra tu kushoto kanalipa 250M hii ni nje ya ruzuku anazotoa.
Umeijenga brand ya simba_ Yes ahsante kwa hili, ila umesahau kuwa simba ndio imekujenga wewe zaidi kuliko ulivyoijenga.
Hujawahi pewa bonus wanapewa wachezaji tu_ Vipi, kuna viongozi wanapewa bonus, kama viongozi wanapewa bonus basi ulistahili.....

Tusaidiane kumjibu Manara.
 
Back
Top Bottom