Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
“Mimi nalipwa hela nyingi, sasa nawezaje kuwa Chawa Mtu mwenye Ubalozi wa Kampuni zaidi ya 20, nani ananiweza Nchi hii kwa Ubalozi? tena sio kampuni ndogo Mimi sitangazi nyanya ya kopo, mmeshawahi kuona nawaita kutangaza bidhaa ndogo?, Mimi natafuta maisha nahangaika napambana Mtu anaponitukana sasa nitamjibu nini?, nitawajibu wangapi”“Waseme Mimi napiga hela, Mimi na Mke wangu kazi yetu ku-mantain brand, sisi tunapiga hela, wewe tukana, sema, wamesema juzi jana, leo naitwa hapa kuwa Balozi imenipunguzia au imeniongezea?, wakati mwingine Watu wakikusema wanainyanyua brand”
“Mimi siangalii nani ananisema nishavuka yaani, Mimi nishasemwa tangu niliposemwa hadi leo sijawahi kupungukiwa chochote yaani hata useme nini Mimi sihangaiki” ——
hayo ni majibu ya Haji Manara akijibu maswali ya Waandishi wa Habari katika mkutano wake akitangazwa kuwa Balozi wa Kampuni ya Surveyed Plot ambapo Waandishi walitaka kufahamu maoni yake kuhusu wale waliomuita kuwa Chawa wa GSM kutokana na mahojiano yake akiwa na Millard Ayo na Frida Amani.