kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Binafsi nadhani kila mtu keshajuwa kwanini uko Yanga Sasa. Hakuna sababu ya kuendelea kuitaja Simba katika kila fursa ya kwenda hewani. Ubongo wa Binadamu una tabia ya kuchoshwa (fed up) na kitu kinachojirudiarudia kila wakati, hata harufu ya chooni inapotea puani kama utakaa chooni kwa muda mrefu.
Hebu jikite kwenye club yako mpya ya yanga Sasa wakati huu wa maandalizi ya kuanza msimu mwingine, uchaguzi na mabadiliko.
Kuendelea kuikosoa Simba ni njia nyingine ya wazi ya kuitaka Simba irekebishe makosa yake ili ifanye vizuri kuizidi Yanga, hii ndiyo sababu ya wahenga kusema aliyelala usimwamshe ukimuamsha utalala wewe.
Sisi Wanayanga tunadhani kuwa unafanya hivyo ili kuiamsha Simba iliyolala. Maana bado moyo wako uko Simba, siku Barbara na mo wakiondka Simba unaweza kurudi Simba.
Utani uwepo lakini sio wa kila saa 24/7 kwa 365. Mipango ya Yanga Wacha iwe Siri ya Yanga na Simba Wana mipango Yao usiibeze. Mfano, unaposema huwezi kujenga uwanja kwa mchango wa buku buku wewe unaumia nini? Who are you to challenge their plans? Yaani unauza kwa Simba mipango ya Yanga ya namna yao ya kujenga uwanja au una maana gani?
Kila kitu lazima kiwe na kiasi. Iko siku watu watakustukia Haji mwanangu kwa ukosoaji wako huo wa Simba kwa kufananisha na mipango ya Yanga kwenye kila jambo, unauza Siri za Yanga kwa Simba kwa jina la utani wa jadi, haitakubalika kwa wanayanga.