Haji Manara punguza kuitaja Simba kwenye kila press na maongezi yako

Haji Manara punguza kuitaja Simba kwenye kila press na maongezi yako

Alivyo kua anawadisi Yanga mulikua munafurahia sasa hivi munaona anakera.

"Kuimba kupokezana "
 
Hiyo kauli ilisababisha Simba wakatafuta wapi Yanga wanatoa jezi zao
Kwa mpira niujuavyo wa hapa bongo, lazima kuwe na maneno maneno ndio yanayochochea upinzani, Manara kaja yanga kwa kazi maalum cha kutumia kinywa chake kuwakera simba, kusema kwamba aache sio leo wala kesho.

na kwenye kukera huwa anagonga ndio maana kuna post nyingi sana humu za wanasimba kuchukizwa, wapo wanaofikia hadi kutumia kivule cha haki za binadamu maana si kwa moto wanaopelekewa
 
Haji Manara anaipenda sana simba kuliko yanga, na asichokijua iko siku pia ataondoka yanga, lakini mwanayanga makini hawezi kumfurahia haji utendaji wake amekaa kiuchonganishi zaidi yaani hajengi kitu kabisa
anaipenda sana ndio maana anaipelekea moto sana kiasi kwamba maada za kujaribu kumzuia haziishi humu ndani, hakika kisu kinagonga mfupa maana si kwa kukera huku 😂😂
 
anaipenda sana ndio maana anaipelekea moto sana kiasi kwamba maada za kujaribu kumzuia haziishi humu ndani, hakika kisu kinagonga mfupa maana si kwa kukera huku 😂😂
Simba n timu ya Babu yake, ndiyo maana akina Barbara wasioifahamu timu wanamkera sana
 
Mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu ni mchungu

Haji Manara shikilia hapo hapo ndio panapouma zaidi
 
Binafsi nadhani kila mtu keshajuwa kwanini uko Yanga Sasa. Hakuna sababu ya kuendelea kuitaja Simba katika kila fursa ya kwenda hewani. Ubongo wa Binadamu una tabia ya kuchoshwa (fed up) na kitu kinachojirudiarudia kila wakati, hata harufu ya chooni inapotea puani kama utakaa chooni kwa muda mrefu.

Hebu jikite kwenye club yako mpya ya yanga Sasa wakati huu wa maandalizi ya kuanza msimu mwingine, uchaguzi na mabadiliko.
Kuendelea kuikosoa Simba ni njia nyingine ya wazi ya kuitaka Simba irekebishe makosa yake ili ifanye vizuri kuizidi Yanga, hii ndiyo sababu ya wahenga kusema aliyelala usimwamshe ukimuamsha utalala wewe. Sisi Wanayanga tunadhani kuwa unafanya hivyo ili kuiamsha Simba iliyolala. Maana bado moyo wako uko Simba, siku Barbara na mo wakiondka Simba unaweza kurudi Simba.

Utani uwepo lakini sio wa kila saa 24/7 kwa 365. Mipango ya Yanga Wacha iwe Siri ya Yanga na Simba Wana mipango Yao usiibeze. Mfano, unaposema huwezi kujenga uwanja kwa mchango wa buku buku wewe unaumia nini? Who are you to challenge their plans? Yaani unauza kwa Simba mipango ya Yanga ya kujenga uwanja au una maana gani?

Kila kitu lazima kiwe na kiasi. Iko siku watu watakustukia Haji mwanangu kwa ukosoaji wako huo wa Simba kwa kufananisha na mipango ya Yanga kwenye kila jambo, unauza Siri za Yanga kwa Simba kwa jina la utani wa jadi.
Mkuu na bado hamjamjua huyo kiumbe, hana siri huyo lopolopo..
 
Manara wapelekee moto [emoji444][emoji445] wapelekee moto moto [emoji445][emoji444] wapelekee moto makolo [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]

Ila simba huwa mnatuchekesha, hii kazi ya ushauri mmeanza lini, yani kuna kipindi mkaanza eti kutushauri mambo ya kombe, dadeki Yani mke ni wangu halafu unanishauri jinsi ya kumgegeda, [emoji23][emoji23][emoji23].

Muwe wapole tu, Na vile mlivyo na hasira kwamba mabingwa hawajavunja rekodi yenu ya kukaa misimu mitano mfululizo 2012 hadi 2017 bila kombe, daah [emoji23][emoji23].

Mabingwa tunatembea vifua mbele, Hii ndio yanga aisee, ni mwendo wa kufumua mishono tu..

Tunasubiri kukwapua F.A., Azizi mlieshindwa kumnasa kwa dau dogo anakuja kwa mabingwa wenye mkwanja, [emoji23][emoji23] Dewji kafunga kiwanda chake cha mkonge huko sasa nikianza kufikiria makolo wanavyotoa pesa kwenye michangonya kiwanja isije ikawa mnachangia fidia za hasara za watu wenye biashara zao [emoji23][emoji23]

Dah, alafu nikifikiria Simba imenunuliwa milele ndio nacheka hadi machozi [emoji23][emoji23]
Pale UTOPOLO, ukiondoa wale WAWILI, wewe na mlio baki, ndio mnao mharibu kwa kumsifia kwa huo upuuzi wake!
 
Manara utamchukia akiwa timu pinzani, akiwa timu yako ni burudani tu.

Kipindi manara akiwa simba hata yanga walikuwa wanalalamika hivi hivi.

Jamaa linajua kukera hiloo , ile mineno sijui anatoaga wapi huyu kiumbe, eti jezi za simba ni kama shuka la kihadzabe[emoji23][emoji23]
Hata huko Simba, wapo ambao walikuwa hawapendi UPUUZI wake!
 
Binafsi nadhani kila mtu keshajuwa kwanini uko Yanga Sasa. Hakuna sababu ya kuendelea kuitaja Simba katika kila fursa ya kwenda hewani. Ubongo wa Binadamu una tabia ya kuchoshwa (fed up) na kitu kinachojirudiarudia kila wakati, hata harufu ya chooni inapotea puani kama utakaa chooni kwa muda mrefu.

Hebu jikite kwenye club yako mpya ya yanga Sasa wakati huu wa maandalizi ya kuanza msimu mwingine, uchaguzi na mabadiliko.

Kuendelea kuikosoa Simba ni njia nyingine ya wazi ya kuitaka Simba irekebishe makosa yake ili ifanye vizuri kuizidi Yanga, hii ndiyo sababu ya wahenga kusema aliyelala usimwamshe ukimuamsha utalala wewe.

Sisi Wanayanga tunadhani kuwa unafanya hivyo ili kuiamsha Simba iliyolala. Maana bado moyo wako uko Simba, siku Barbara na mo wakiondka Simba unaweza kurudi Simba.

Utani uwepo lakini sio wa kila saa 24/7 kwa 365. Mipango ya Yanga Wacha iwe Siri ya Yanga na Simba Wana mipango Yao usiibeze. Mfano, unaposema huwezi kujenga uwanja kwa mchango wa buku buku wewe unaumia nini? Who are you to challenge their plans? Yaani unauza kwa Simba mipango ya Yanga ya kujenga uwanja au una maana gani?

Kila kitu lazima kiwe na kiasi. Iko siku watu watakustukia Haji mwanangu kwa ukosoaji wako huo wa Simba kwa kufananisha na mipango ya Yanga kwenye kila jambo, unauza Siri za Yanga kwa Simba kwa jina la utani wa jadi.
alivyokua makolokoloni pia alikua anaitajaa sanaaa yanga hata kwenye press zake za binafsi so vumilieni tuu
 
Naona mna kasirika kwa kitendo kilichokuwa kikiwafurahisha kipindi akiwa kwenu akiiponda Yanga, ila leo mnakasirika mmemlea wenyewe cha msingi mvumilieni mwanenu huyu.
 
Sitaki kuamini kuwa humjui Haji Manara.. Haji Huyu ni Haji yuleyule aliyekuwa Simba Sport Club na kazi yake kubwa ilikuwa kuicharura Club ya Yanga na Mashabiki wake pia, licha ya ubora wa Simba kipindi kile kuwa juu sana zaidi ya Yanga Ila kucha kutwa alikuwa anainanga Yanga. Sasa Leo hii Haji Yuko Yanga ndo ushangae kweli Haji kuinanga Simba Kila wakati au Kila sekunde ya maisha yake..? Na isitoshe the way alimove from Simba to Yanga.
Naona dhahiri mtoa mada UNATESEKA na kitu Fulani.. Haji Manara ni wa kumuacha hivyohivyo hiyo ndo Style yake ya maisha kwanza tulishajua toka mwanzo kuwa huyu bwana akichukuwa kombe Huku Yanga lazima Mashabiki wa Simba wateseke na Hii naona ilikuwa nadhiri yake kwa Simba.

Pole sana kwa Mateso boss fanya mambo yako Haji muache na maisha yake.
 
.
 
Attachments

  • IMG-20220620-WA0000.jpg
    IMG-20220620-WA0000.jpg
    27.4 KB · Views: 5
Back
Top Bottom