Haji Manara punguza kuitaja Simba kwenye kila press na maongezi yako

Alivyo kua anawadisi Yanga mulikua munafurahia sasa hivi munaona anakera.

"Kuimba kupokezana "
 
Hiyo kauli ilisababisha Simba wakatafuta wapi Yanga wanatoa jezi zao
Kwa mpira niujuavyo wa hapa bongo, lazima kuwe na maneno maneno ndio yanayochochea upinzani, Manara kaja yanga kwa kazi maalum cha kutumia kinywa chake kuwakera simba, kusema kwamba aache sio leo wala kesho.

na kwenye kukera huwa anagonga ndio maana kuna post nyingi sana humu za wanasimba kuchukizwa, wapo wanaofikia hadi kutumia kivule cha haki za binadamu maana si kwa moto wanaopelekewa
 
Haji Manara anaipenda sana simba kuliko yanga, na asichokijua iko siku pia ataondoka yanga, lakini mwanayanga makini hawezi kumfurahia haji utendaji wake amekaa kiuchonganishi zaidi yaani hajengi kitu kabisa
anaipenda sana ndio maana anaipelekea moto sana kiasi kwamba maada za kujaribu kumzuia haziishi humu ndani, hakika kisu kinagonga mfupa maana si kwa kukera huku 😂😂
 
anaipenda sana ndio maana anaipelekea moto sana kiasi kwamba maada za kujaribu kumzuia haziishi humu ndani, hakika kisu kinagonga mfupa maana si kwa kukera huku 😂😂
Simba n timu ya Babu yake, ndiyo maana akina Barbara wasioifahamu timu wanamkera sana
 
Mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu ni mchungu

Haji Manara shikilia hapo hapo ndio panapouma zaidi
 
Mkuu na bado hamjamjua huyo kiumbe, hana siri huyo lopolopo..
 
Pale UTOPOLO, ukiondoa wale WAWILI, wewe na mlio baki, ndio mnao mharibu kwa kumsifia kwa huo upuuzi wake!
 
Hata huko Simba, wapo ambao walikuwa hawapendi UPUUZI wake!
 
alivyokua makolokoloni pia alikua anaitajaa sanaaa yanga hata kwenye press zake za binafsi so vumilieni tuu
 
Naona mna kasirika kwa kitendo kilichokuwa kikiwafurahisha kipindi akiwa kwenu akiiponda Yanga, ila leo mnakasirika mmemlea wenyewe cha msingi mvumilieni mwanenu huyu.
 
Sitaki kuamini kuwa humjui Haji Manara.. Haji Huyu ni Haji yuleyule aliyekuwa Simba Sport Club na kazi yake kubwa ilikuwa kuicharura Club ya Yanga na Mashabiki wake pia, licha ya ubora wa Simba kipindi kile kuwa juu sana zaidi ya Yanga Ila kucha kutwa alikuwa anainanga Yanga. Sasa Leo hii Haji Yuko Yanga ndo ushangae kweli Haji kuinanga Simba Kila wakati au Kila sekunde ya maisha yake..? Na isitoshe the way alimove from Simba to Yanga.
Naona dhahiri mtoa mada UNATESEKA na kitu Fulani.. Haji Manara ni wa kumuacha hivyohivyo hiyo ndo Style yake ya maisha kwanza tulishajua toka mwanzo kuwa huyu bwana akichukuwa kombe Huku Yanga lazima Mashabiki wa Simba wateseke na Hii naona ilikuwa nadhiri yake kwa Simba.

Pole sana kwa Mateso boss fanya mambo yako Haji muache na maisha yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…