Haji Manara punguza kuitaja Simba kwenye kila press na maongezi yako

Kutesa kwa zamu
Haji yuko vizuri tu ila lazima awe na kiasi katika kila jambo. Kila Club lazima iwe na mipango yake ambayo inatekelezwa kimyakimya, sio lazima tufanane na simba kwa kila kitu kila jambo. Kila mtu afanye kivyake lakini tukutane uwanjani. Ile ya kusema Yanga tuko sahihi tuko sahihi tuko sahihi maana sisi tunafanya hivi nyie mnafanya vilee sio sawa. Huko ni kuuza mipango ya yanga kwa adui kwakujua au kwa kutokujua, makusudi au bahati mbaya, kudhamiria au kuponyokwa tu, Wahenga wanasema "ukijamba kwa hasira utajinyea" be calm brother, hata Mtume Mohamed SAW alidhihakiwa sana lakini hakupoteza focus.
 
Kumuandalia UZI kama huu ndo unazid kumpaisha
 
Sa bruh bila simba atakula wapi maaana pale yanga cheo alicho nacho ndo icho eti mwamasishaji
 
Kumuandalia UZI kama huu ndo unazid kumpaisha
Lengo sio kumshusha bro, kila mtu keshapangiwa na kupewa na Mungu tayari, hapa tunamlingania tu ili kuepuka yale ya wanadamu.
 
Hana lolote yule,isipokuwa kwa wajinga wenye kuhadaika na shombo zake
 
Alipo kua Simba Mbona kila uchwao alikua anaitaja yanga hamkuja na malalamiko tulieni tuu
 
kwani kumtaja mwajiri wa zamani ni dhambi? beside manara ni simba damu, huko yanga aliko ni ajira tu
 
Haji hakuwa Simba kwa bahati mbaya TU, bali ni urithi wa Babu yake mzaa mama yake ambae alikuwa kiongozi mkubwa wa Simba. Sio kwamba ni jambo la utaniutani kwa Haji kuwa Simba na kuondoka Simba.
Na hakuna mtu anakuwa Simba au Yanga akiwa na miaka 40+, huyu msukule yupo Yanga kikazi tu,wacha apige hela.
 
Haji aendeleze kupiga spana kama alizowahi kuipiga Yanga. Kama Yanga tulivyo vumilia na Simba wanahitaji uvumilivu uleule.
 
Timu ya babu yake???kwa hyo ameachiwa urithi co???
Haji inazifahamu simba na yanga kuliko wewe, mimi na vichambuzi uchwara vyote vya mpira nchi. Ana historia nazo, ameziishi. Hata nepi yake ya kwanza alinunuliwa kwa posho ya baba yake aliyoipata Yanga. Lakini babu yake mzaa mama yake aliwahi kuwa mwenyekiti wa Simba.
 
Nilikwambia Haji, wenzako wanakutafuta chini na juu, kushoto na kulima, watakupata tyuuu, ona sasa; badala 20 billion zao ni 20 m zako,
 
Ni ngumu kumsahau mwanaume wako aliyekupa taraka bila kutarajia,Kila kitu utakachokipata utafikiri kasababisha yeye,ukimpata mikosi na balaa utasema yeye ndo amesababisha,ukifanikiwa kimaisha utasema yeye ndo alikuchelewesha,kwahiyo Kila siku utakuwa unasema iwe Kwa mazuri au mabaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…