Haji Manara: "Simba ndio wa Kimataifa"

ngoja tumsubiri na huyo wa kimataifa aje.....hala hala tu.....uvumilivu unahitajika......hadj umesahau kuwa washabiki wenu mmewajenga kusikiliza zaidi POROJO kuliko FACTS Si ajabu hata ulichokizungumza hapo hakijaeleweka hata kwa hao washabiki maandazi.......nawasih nyote wawili muwe na uvumilivu
 
Hapa ni record za simba vs yanga.....Tp mazembe anaingiaje tena? Mnatafuta chaka?
Anajaribu tu kuonyesha kwama si sahihi kujifungia ndani sababu ya records bali ni wakati wa watu kutoka nje ya maboksi, yaani tuachane na tabia ya kuishi katika historia na tuanze kuuisgi uhalisia. Ni mzigo mkubwa kuishi na mzigo wa historia mabegani wakati haukusaidii chochote katika wakati tulio nao sas.

Ndiyo chanzo cha kuiongelea TP Mazembe ambayo haina kabisa huo mkeka wa historia
 

 
Hata mazuri na mafanikio wanayo yapata Tp mazembe ni record wanatengeneza......

Tukubali record zinawekwa ili zivunjwe kwa kuangalia mafanikio ya pande zote.
 
Kapigwa APR jana hapo kwao Rwanda wewe uko unawasubiri Prison ya Mbeya basi haina haja ya kusumbua akili Simba ni WAMCHANGANI najua inauma ila hakuna namna mkiweza jikwamueni.
 
Siku zote hawezi kupiga hoja kwa matusi tu toa hoja zako ndiyo tukuamini mambo ya Manara yako sawa ili uyapinge weka record ya Yanga siyo matusi mbona nyie mnakuwa wapuzi kama msemaji wa Yanga pinga kwa topic za maana siyo matusi
 
atoto ebu njoo huku kwanza ule fact. Soma uzi wenye facts!
Vyura fc tupa kule, hapa ni MNYAMA aka SIMBARCELONA, mpira kapetini!
 
Simba ndio timu pekee isiokuwa na uwanja tangu Mwaka 1938 hadi Leo. Ongezea nyingine.
 
Huu ni ujinga na majungu kama ulivyo ujinga mwingine,ndo maana hizi timu zetu haziendelei kazi kuendekeza ujinga kama,nawachukia kishenzi Simba na Yanga katika ustawi wa mpira wa Tanzania,eti mtu anajisifu kupanda ndege wakati hata uwanja hana!!!
 
atoto ebu njoo huku kwanza ule fact. Soma uzi wenye facts!
Vyura fc tupa kule, hapa ni MNYAMA aka SIMBARCELONA, mpira kapetini!
Hana ishu hiyo Manara, anatafuta kumletea kesi Murro tu, hivi akimkimbiza mchana ili amuadhibu unadhani wananchi watamsaidia nani?
 
haji manara sijui tatizo lako haswa nini!hebu tulia kwanza tusubir wanaume walioenda kutafuta warudi tuwapokee halafu ndo uje na huu upuuzi wako.
 
Simba ndio timu pekee isiokuwa na uwanja tangu Mwaka 1938 hadi Leo. Ongezea nyingine.
Angalau tuna eneo la kujenga uwanja, hivi Vyura Fc lile bwawa la samaki na vyura mnaita uwanja?? Basi kituko!
 
Kwa kuwa anazungumzia Simba FC ukilinganisha na timu ya Yanga,nilidhani angelilinganisha na kulinganua (Compare and Contrast) kumbe ameorodhesha tu zile za Simba tofauti na dhamira yake..Katika historia Uingereza ndiyo ilikuwa ndio nchi ya kwanza kuwa na Viwanda,uliza leo kama bado wanaongoza.
 
Kwamba ndio walivaa viatu wa kwanza, walivaa suit wa kwanza, walipanda ndege wa kwanza..... Vp leo je hata hiyo ndege ya kuvuka mpaka wanapanda kwel? Tuzungumze leo upo ktk hali gan sio kusema tulikuaga ambao hata kwenye miaka aliosema wengne tulikuwa hatujazaliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…