Haji Manara: "Simba ndio wa Kimataifa"

Haji Manara: "Simba ndio wa Kimataifa"

Kwani samata wakati anaenda ulaya alikuwa wa simba.? Si ametokea TP Mazembe?
 
Yanga jifunzeni kuongea kwa data.Manara katoa data za simba,toeni na zenu tulinganishe nani wa kimataifa na nani wa kitaifa zaidi.
Data zenyewe uongo. Yeye kasema sunday manara wakat anaenda ulaya alitokea pan. Hapo hapo kamjumuisha samata kwenda genk kama ametokea Simba
 
Katika Hali Isiyokuwa Ya Kawaida Msemaji Wa Klabu Ya Simba Haji Manara Leo Ameamua Kumpiga Vibaya Sana Kwa Knock Out Msemaji Wa Klabu Ya Yanga Jerry Muro Baada Ya Ubishani Mkubwa Wa Ni Timu Gani Kweli au Hakika Inastahili Kuitwa au Kujiita YA KIMATAIFA au WA KIMATAIFA Kutokana Na Rekodi Za KUTUKUKA Ilizonazo Hiyo Timu.

Hiki Ndicho Msemaji Wa Simba Alichokisema...........


Waungwana kila uchwao kwenye jiji hili na viunga vyake sambamba na maeneo mengi ya nchi, kuna neno wa ‘kimataifa’ hulisikia likiimbwa.

Waimbaji wakuu wa neno hilo ni mashabiki wa Yanga wakiongozwa na mpiga zumari wao aliyeacha kazi yake na kujigeuza muimbaji.

Kinyume chake hilo neno klabu ya Simba huitwa wa ‘mchangani’ au wa ‘matopeni’. Wengi wananilaumu kuwa kwa nini huwa sijibu neno lolote la ajabu kwa Yanga. Jibu langu ni jepesi tu, lazima tujitofautishe msemaji wa klabu na mropokaji wa klabu.

Mimi hupenda kuzungumzia issues sio porojo au lugha za uchochoroni. Haiwezekani nikawa kiongozi kisha nikaongea lugha za mashabiki ‘maandazi’.

Kwa hiyo mtaniwia radhi wapenzi wa mpira kwa kutokuwa muimbaji wa ngonjera za uchochoroni. Mara zote nitabaki msemaji wa klabu kubwa nchini na ntaongea facts kwa kadri zilivyo.

Wadau zisomeni sifa za kimataifa kwa klabu ya Simba nje ya nchi halafu zifananisheni na timu nyingine nchini.

Walau kama zitafikia nusu tunawaruhusu watafute tusi jipya. Ombi langu kwenu isambazeni taarifa hii katak kila mtandao wa kijamii kisha waseme wao wanaojiita wa kimataifa.

1. Simba ndiyo timu ya kwanza nchini kupanda ndege na hii ilikuwa mwaka 1963 tena wakati huo taifa la Tanzania halikuwa limeundwa, ilikwenda Ethiopia kwa mwaliko wa rais wa taifa hilo Haile Selassie

2. Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa jezi na hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam.

3. Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa viatu nchini na hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini Navy ya Afrika Kusini.

4. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa na basi lake yenyewe na hili lilinuliwa mwaka1968.

5. Simba ndiyo timu ya kwanza kumiliki jengo lake lenyewe na hili lilizinduliwa 1971.

6. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa bingwa wa ligi kuu nchini1966.

7. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwakilisha nchi na hii ilikuwa 1967.

8. Simba klabu ya kwanza nchini kwenda Ulaya na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland

9. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa mabingwa wa Afrika Mashariki na kati na hii ilikuwa 1974.

10.Simba ndio mabingwa wa kihistoria wa Afrika Mashariki na Kati, ndiyo timu iliyochukua ubingwa mara nyingi kuliko klabu yeyote Afrika Mashariki na Kati (Champs off all time.)

11.Simba ndiyo timu pekee nchini iliyowahi kufika nusu fainali ya klabu bingwa Afrika na hii ilikuwa1974.

12.Simba ndiyo timu pekee nchini na Afrika Mashariki kufika fainali ya kombe la Caf na hii ilikuwa1993.

13.Simba ndio timu inayoshikilia rekodi Afrika kama si duniani kwa kufungwa na Mufurila Wonderers ya Zambia magoli 4-0 na kwenda kuibamiza 5-0 kwao, mbele ya rais wao Kenneth Kaunda. Hii haijafanywa na klabu yeyote Afrika na nina mashaka duniani, hii ilikuwa 1979.

14.Simba ilicheza katik hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika 2003 kwa mafanikio makubwa kulinganisha na timu yoyote nchini.

15.Simba ndiyo timu pekee kuivua ubingwa klabu bingwa Afrika nadi Zamalek hii ilikuwa pia 2003.

16.Simba ndiyo klabu pekee nchini kuzifunga timu zote za mataifa ya kiarabu kuanzia

· Waliowatoa mwaka jana Etoile du Sahel (Tunisia)

· Widad Casablanca (Morocco)

· El Setif (Algeria)

· El Harach (Algeria)

halaf tumezifunga timu zote kubwa za Misri Zamelek,Al Ahly, Arab Contractors, Ismailia, Mehala, Al kubra na timu nyingine mnajua huwa inafanywaje ikigusa kule.

Pia imeshaitoa El Merekh ya Sudan 1994 katak klabu bingwa ya Afrika. Simba pia imeshazifunga miamba ya Afrika Magharibi kuanzia Asec, Asante Kotoko, Hafia ya Guinea hata mabingwa wa kihistoria wa Zambia Nkana Red Devils.

17. Tukirudi juu Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa suti na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland.

18.Simba ndiyo klabu pekee nchini kujenga jengo lake yenyewe kwa nguvu za wanachama na mashabiki, wenzetu ni mkopo na msaada toka kwa mzee Karume100%, Simba ilipewa kiasi flan na mzee karume baada ya jengo kukamilika na hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 70.

19.Angalia idadi ya wachezaji wa Simba walioenda Ulaya kucheza soka la kulipwa.

· Nico Njohole

· Deo Njohole

· Kassim Matitu

· George Kulagwa

Huku ikiwa na makumi ya nyota wake kadhaa waliowahI kutapakaa sehemu mbalimbali duniani.

Nikutajie wachache.

· Khalid Abeid

· Haidar Abeid

· Martin Kikwa

· Athman Mambosasa

· Zamoyoni Mogella

· Hamis Gaga

· Lilla Shomari

· Iddi Pazi

· Kiwelu Mussa

· George Masatu

· Hussein masha na wengine wengi.bila kumsahau nguli wa sasa mbwana samata.mutoto ya msimbazi.

Na hapa kumbukumbu zikae vizuri wazee wangu mimi, Sunday na Kassim Manara wakati wanaenda kucheza Ulaya hawakuwa wachezaji wa Yanga, walikuwa wakicheza Pan African.

20. Nimalizie kwa kuwaambia FIFA ilizitaja timu bora za karne kwa kila nchi kwa Tanzania Simba ilitajwa ndio timu bora ya karne na wenye mpira wao FIFA. Nenda kwenye rekodi za Caf ndio utajua nani wa kimataifa baina ya cc na wao.

Porojo za mjini ntakuwa nimezimaliza sasa na anayebisha abishe kwa data. Wakoloni wetu walitufundisha hivi…No reaserch no data no right to speak.Tafsiri isiyo rasmi, hujafanya utafiti na huna takwimu funga bakuli lako.

Asanteni na nendeni mkawaambie.

Haji S Manara
Msemaji wa klabu bora ya muda wote Tanzania (best club of all time)
Ukiona errors zipotezee jadili issues na nnaruhusu challenges kama zipo
Porojo peleka kuleeeeeee.

Nimalizie Tu Kwa Kusema Msemaji Wa VYURA FC au Yanga Football Club Jerry Muro Anyamaze Tu Kwani Sasa Wanasimba Wameamua Kutembea Na Facts Hizi Ambapo Sasa Watakuwa Kama Wakimsikia Anaikashifu au Kuitukana Simba Sports Club Basi Na Wao Watamkabidhi Hizi Data Ili Kusudi Na Yeye Pia Atupatie Za Yanga Kama Zipo.


Shikamoo Msemaji Wa Simba Sports Club Haji Manara Hakika Leo Umemaliza Kila Kitu Huku Ukimtia Aibu Mtu Anayejitamba Kuwa Ana Masters Degree, Kaoa Mzungu Na Anaishi Mbezi Beach Mropokaji Wa Yanga Jerry Muro.

Na Mwisho Ningeshauri Sana Ewe Mwana Yanga Football Club Yoyote Utakayeiona Hii Na Kuisoma Basi Si Vibaya Ukaisambaza Kwa Wana Yanga FC Wenzio Popote Pale Walipo au Watakapokuwepo Ili KUMBUKUMBU Hii Muhimu Isije Ikawatoka AKILINI Mwenu. Kila Mwana Yanga Apate Copy Ya Hii Tafadhali.
We jamaa kumbe pamoja na kuwa ccm ila unaipenda simba
 
Hapa ni record za simba vs yanga.....Tp mazembe anaingiaje tena? Mnatafuta chaka?
Sawa. Maana yangu ni kwamba hizi record hazitusaidii kitu. Yanga kawa bingwa wa Tanzania mara nyingi zaidi lakini haijasaidia kutwaa ubingwa wa Africa.
Sasa record eti timu ya kwanza kuwa na jengo.
 
Kwakua mpaka sasa,yanga wameshindwa kutoa data zinazovunja record za simba.Nashauri hivi,Yanga mwaka huu angalau mfike robo fainali ili tuanze kuwapa hiyo heshima ya KIMATAIFA.
 
Si busara kutukana timu ambayo ndiyo iliyojenga jina la Nchi kimataifa eti kwasababu ya kukosa ubingwa.Tujenge heshima kwa wanaotuzidi na tujifunze kwao.Sisi simba tunasema hivi,Yanga bado ni timu isiyo na record kimataifa hivyo HAISTAHILI KUJIITA YA KIMATAIFA.Acheni ushabiki wa kupelekwa na taahira Muro.
 
Si busara kutukana timu ambayo ndiyo iliyojenga jina la Nchi kimataifa eti kwasababu ya kukosa ubingwa.Tujenge heshima kwa wanaotuzidi na tujifunze kwao.Sisi simba tunasema hivi,Yanga bado ni timu isiyo na record kimataifa hivyo HAISTAHILI KUJIITA YA KIMATAIFA.Acheni ushabiki wa kupelekwa na taahira Muro.
Mchezaji anaitwa International kama anachezea timu ya taifa lake kwa wakati huo. Hali kadhalika, timu ni kimataifa au international kama inashiriki mashindano ya kimataifa wakati huo. Siyo hali ya kudumu. Inaenda na hali halisi kwa wakati husika.
 
Tuendelee kujivunia wachezaji wetu wawe yanga au simba hao waliotajwa 90%wamecheza Asia!
 
Nonda
Mnawakumbuka hawa: Peter Manyika, Ali Mayai, Salvatory Edward, Bakari Malima, Sekilojo Johnson Chambua, Ephraem Makoye, Edibily Jonas Lunyamila, Kali Ongala. Tajeni wengine wakuu kikosi hiki cha 1998-1999.

Uniambii kitu kuhusu YANGA!!
Nonda shabani"papii"hahusiki hapo?
 
Kweli watani wetu wa mchangani wechanganyikiwa na kukosa hoja.
Kweli mtu anajisifia eti kuvaa suti kwa mara ya kwanza ni historia katika soka?
Halafu anaita ni fact na mashabiki wa mchangani walivyo mapopoma wanashangilia!
Endeleeni kujivunia historia zenu hadi za kuvaa viatu kwa mara ya kwanza huku wenzenu wa kimataifa tunazidi kuchanja mbuga kimataifa.
 
kwanza manara kapotosha uma Timu yake ya 36 yanga 35 inamaana yanga haikushiriki mashindano mwaka huo

pili jengo la yanga ndiyo la kwanza ndiyo likajengwa la simba huo uongo akawadanganye wa matopeni wenzake
 
Kweli watani wetu wa mchangani wechanganyikiwa na kukosa hoja.
Kweli mtu anajisifia eti kuvaa suti kwa mara ya kwanza ni historia katika soka?
Halafu anaita ni fact na mashabiki wa mchangani walivyo mapopoma wanashangilia!
Endeleeni kujivunia historia zenu hadi za kuvaa viatu kwa mara ya kwanza huku wenzenu wa kimataifa tunazidi kuchanja mbuga kimataifa.
mkuu tupe data kama za Manara , usizunguke sana utani wa jadi unanoga mtu akitoa data na wewe unakuja na data
 
mkuu tupe data kama za Manara , usizunguke sana utani wa jadi unanoga mtu akitoa data na wewe unakuja na data
Data gani?Za kuvaa suti/viatu kwa mara ya kwanza?
Hili ni soka,nadhani tungejadili kuhusu data za kisoka zaidi.

Subiri msemaji wetu msomi ALIYETUKUKA Gerry Muro atakapotoa data za kisomi,sio hizo za STD 7 za Manara.
 
Subiri msemaji wetu msomi ALIYETUKUKA Gerry Muro atakapotoa data za kisomi,sio hizo za STD 7 za Manara.[/QUOTE]
hana data yeyote yule,
 
Nimemskia Afisa Hbr Wa Simba HAJI MANARA, Akiwa Studio Za Efm Redio, Jamaa Ametulia Mno, Sikusikia Akiropokwa Na Kupayuka Hovyo, Hata Kufikia Kung'an'ania Kuongea, Kama Anapokuwa Msemaji Mmoja Wa Klabu Fulani!! Studio Uwa Makelele Tupu, Hoja Zenyewe Hazina Mashiko, Lkn Kila Mara Ataomba Aongee 'Yeye Tu!! Kongole Kwako Afisa Hbr Wa Simba!!!
 
Data gani?Za kuvaa suti/viatu kwa mara ya kwanza?
Hili ni soka,nadhani tungejadili kuhusu data za kisoka zaidi.

Subiri msemaji wetu msomi ALIYETUKUKA Gerry Muro atakapotoa data za kisomi,sio hizo za STD 7 za Manara.
Je, Anaposema Nenda Ktk Website Ya CAF, Ukaperuzi Ili Upate Kujua CAF Ktk Ukanda Wa East Africa Inaitambua Klabu Gani Kuwa Ndio Yenye Mafanikio!!!?? Hilo Limethibitishwa Na Katibu Mkuu Wa TFF Na Mchezaji Nguli Wa Zamani Na Mpenzi Wa Yanga, Ally Mayai Tembele, Wakihojiwa Na Mtangazaji Wa Efm Redio Asbh!! Sasa Pinga Kwa Asili Yako Ya Ubishi Tu!!! LKN Hoja Ya Kupingia Hauna Ww Na Hata Viongozi Wenu!!!
 
Kweli watani wetu wa mchangani wechanganyikiwa na kukosa hoja.
Kweli mtu anajisifia eti kuvaa suti kwa mara ya kwanza ni historia katika soka?
Halafu anaita ni fact na mashabiki wa mchangani walivyo mapopoma wanashangilia!
Endeleeni kujivunia historia zenu hadi za kuvaa viatu kwa mara ya kwanza huku wenzenu wa kimataifa tunazidi kuchanja mbuga kimataifa.
Kweli Mpira Umeingia VILAZA!!!! Hivi History Sio Sehemu Ya Soka Kweli!!!!?? Haya Huo Wakimataifa Wenu Kwa Miaka Ambayo Mnashiriki Kwa Kuiwakilisha Tanzania, Ni Mafanikio Yepi Ambayo Mmeyafikia!!?? Zaidi Kuishia Raundi Ya Kwanza Au Pili Tu!!!!
 
Back
Top Bottom