Haji Manara soma alama za nyakati kabla haujastaafu kwa aibu

Haji Manara soma alama za nyakati kabla haujastaafu kwa aibu

sonofobia

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
1,171
Reaction score
4,295
Zama za Haji Manara zinaelekea mwishoni. Kwa sasa awepo au asiwepo kwenye jambo hakuna kinachoongezeka wala kinachopungua.

Sasa ameamua kupambana na wakati hataki kuonekna yeye ni ziada.

Anatumia njia zile zile za miaka yote kukanyaga vichwa vya wenzie ili yeye apande juu.

This time naona anaenda kuchemka. Upande aliopo kuna culture tofauti ya mashabiki.

Asilazimishe umuhimu atulie aanze kujiandaa kujaribu taaluma nyingine.

Tunajua nje ya Yanga na Simba hana ishu anategemea ukubwa wa hizi brand kusafiria nyota. TV yake imefeli sababu hana maudhui amezoeleka ni mtu wa kushambulia watu kutumia mgongo wa hizi club kubwa nje ya hapo atafanya tour Marekani au mwezini ila nobody cares.

Manara usipostuka utaaga kazi yako kwa aibu.

Muda wako ushapita kubali matokeo.
 
Huyu mkuu alijiaminisha bila yeye hakuna mpira Tanzania na hakuna wa kumfanya chochote hususani ktk mpira hata akivunja sheria!!

Kapigwa pin time mby ambapo Yanga ipo moto, angeuza sana wakati huu...

Nikumaanisha yeye si chochote, huenda hata pin likiisha akakosa kiti vijana wako busy 😄
 
Inamuumiza sana kuona timu zinafanya vizuri yeye akiwa pembeni na viwanja vinajaa. Anatafuta kutambulika umuhimu wake.
 
Kiuhalisia Yanga haimuitaji tena manara. Ali kamwe anatosha na kwa upande wa simba ahmed ally anatosha. Ukienda azam kuna ibwe. Kiufupi aende pale kishamba Tv kuwa mchambuzi nadhani prisca atamlipa vizuri.
 
Manara ni giant, fursa nyingi zinamfata. Ni ambassador yuleeee na anaweza kuwekeza kokote akafika mbali Zaid ya waliomtangulia. Muhimu aweke watu sahihi na wenye nia na malengo tu. TV yake ameweka vijana wadogo wadogo wotee hii inanipa waswas juu ya mishahara anayolipa. Na hii itamuumiza sana kwenye compitence ya anachotoa na ubunifu
 
Mwacheni afanye yake ! Na nyie fanyeni yenu ! kila siku manaraaa manaraaa hamchoki !!???
Naona umeandika huku ukiwa na hasira kali!! Salama lakini? Tatizo la huyo ndugu yako ni kupenda pia ligi na watu wengine. Hivyo jitahidi tu uwe mpole pale wapinzani wake naye wakimpopoa kwa mawe.

Na kama huamini, basi watafute wale marafiki zake wa siku nyingi! Mfano Jemedari Said aka Bin Kazumari na Moo, halafu watakuambia huyo Haji Manara ni mtu wa aina gani.
 
Kuna siku aliwahi ku post clip inayomuonesha Mayele akikataa kufanya mahojiano na Kay Mziwanda kwasababu ni Simba.

Manara alipigilia msumari kuwa alichofanya Mayele kwa Kay Mziwanda kukataa interview kwasababu Kay Mziwanda ni Simba hivyo hakutakiwa kufanya interview na mchezaji wa Yanga.

Manara alimrushia maneno ya kejeli Kay Mziwanda kutokana na kukataliwa kwake.

Sasa Manara naye kafungua TV yake, maana yake kupitia ile post yake hakuna mwana Simba ambaye ataenda kufanya interview kwenye TV yake.

Japo nilimuona akisema TV yake haitahusiana na itikadi zake lakini namuona ni mnafki kwasababu hata Kay Mziwanda alikuwa amesimamia kwenye brand ya TV na sio swala la ushabiki.
 
Kiuhalisia Yanga haimuitaji tena manara. Ali kamwe anatosha na kwa upande wa simba ahmed ally anatosha. Ukienda azam kuna ibwe. Kiufupi aende pale kishamba Tv kuwa mchambuzi nadhani prisca atamlipa vizuri.
Si ndo alimwambia prisca ana pua kama gunzi...
 
Back
Top Bottom