Haji Manara, staha ni jambo muhimu sana kwa binadamu yeyote mwenye akili timamu

Haji Manara, staha ni jambo muhimu sana kwa binadamu yeyote mwenye akili timamu

Tairi bovu

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2017
Posts
3,063
Reaction score
2,985
Sitaki akili yangu wala ya msomaji yeyote itilie manani juu ya uwezo wako kichwani, elimu yako, makuzi yako wala jamii yako.

Itoshe tu kusema staha ni jambo muhimu sana kwa binaadamu yeyote yule mwenye akili na utashi. wewe sio mmoja wapo mwenye staha. Unaropoka sana. inakera.

Dunia ni kijiji, japo sijui Tanzania ipo sehemu gani ya hicho kijiji kama ni mjini au kijijini mwa kijijini. Juzi tumeshuhudia ligi kuu mbalimbali barani ulaya na kwinginepo duniani zikitia tamati na mabingwa wakitangazwa.

Ligi yetu pendwa pale lwa malikia imeisha na city kuwa bingwa hatujamsikia msemaji wa klabu ile akipayuka hovyo kama Manara. Tuseme hayupo? Ligi ya mabingwa ulaya madrid wamechkua ndoo mara tatu mfululizo hatujamsikia msemaji wao akiropoka kama ufanyavyo manara.

Kote duniani, kazi za ma PR ni kutengeneza postive emergies za taasisi zao. sio mipasho wala kuropoka kama afanyavyo Manara.
sasa linakuja suala la usajili. manara wewe haupo kwenye benchi la ufundi, unaliongelea suala la isajili kutoka kwenye pembe ipi ya mpira?

Wandishi wa habari wa tanzania jirekebisheni? hivi unapomhoji masau bwire kuhusu kikosi cha jkt ruvu unatengeneza picha gani wakati kocha yupo.
haji manara jitathimini mkuu, unajidhalilisha na kuudhalilisha mpira.

Unakera
 
Hio kazi ya HR kumpa huyo mtu Simba walikosea sana; kazi kama hio inataka mtu mwenye uelewa mkubwa na shule kaenda sio kumpatia mtu hata form 4 yenyewe ya shida. Kwa vile sasa itaendeshwa kibiashara zaidi inabidi iangalie na hawa waajiriwa vizuri watakaoleta positive images kwa klabu sio hawa watu wa mipasho utafikiri wako kwenye taarab.
 
sitaki akili yangu wala ya msomaji yeyote itilie manani juu ya uwezo wako kichwani, elimu yako, makuzi yako wala jamii yako. itoshe tu kusema staha ni jambo muhimu sana kwa binaadamu yeyote yule mwenye akili na utashi. wewe sio mmoja wapo mwenye staha. unaropoka sana. inakera.
dunia ni kijiji, japo sijui Tanzania ipo sehemu gani ya hicho kijiji kama ni mjini au kijijini mwa kijijini. juzi tumeshuhudia ligi kuu mbalimbali barani ulaya na kwinginepo duniani zikitia tamati na mabingwa wakitangazwa. ligi yetu pendwa pale lwa malikia imeisha na city kuwa bingwa hatujamsikia msemaji wa klabu ile akipayuka hovyo kama manara. tuseme hayupo? ligi ya mabingwa ulaya madrid wamechkua ndoo mara tatu mfululizo hatujamsikia msemaji wao akiropoka kama ufanyavyo manara.
kote duniani, kazi za ma PR ni kutengeneza postive emergies za taasisi zao. sio mipasho wala kuropoka kama afanyavyo manara.
sasa linakuja suala la usajili. manara wewe haupo kwenye benchi la ufundi, unaliongelea suala la isajili kutoka kwenye pembe ipi ya mpira?
wandishi wa habari wa tanzania jirekebisheni? hivi unapomhoji masau bwire kuhusu kikosi cha jkt ruvu unatengeneza picha gani wakati kocja yupo.
haji manara jitathimini mkuu, unajidhalilisha na kuudhalilisha mpira. unakera

Ngoja na mi nikukere kidogo!!.. nasikia azam jana kawadunda tatu yaani mliloa kama mbweha.. halafu nasikia ngoma kasajili azam ili apate urahisi wa kutua chama la ukweli mnyama unyamani.. haf nasikia ajibu kagoma kucheza tena timu yenu yaani anasema bora avue dagaa mto kaunda kuliko kuchezea yanga.. halafu nasikia mzee akilimali kafunga milango ya klabu hataki kusikia nsajigwa wala nsa job.. kwi kwiiii!.. mi mdogo wake manara haya pasuka sasa chura wa kaunda mkubwa wewe
 
Hivi msemaji wa Abajalo ya sinza ni nani vile?
 
Hio kazi ya HR kumpa huyo mtu Simba walikosea sana; kazi kama hio inataka mtu mwenye uelewa mkubwa na shule kaenda sio kumpatia mtu hata form 4 yenyewe ya shida. Kwa vile sasa itaendeshwa kibiashara zaidi inabidi iangalie na hawa waajiriwa vizuri watakaoleta positive images kwa klabu sio hawa watu wa mipasho utafikiri wako kwenye taarab.
Kuandika hujui, unaleta ubishoo kisa una husda na club Tajiri African mashariki na kati. Hivi kwanza unajua Tshishimbi leo kajifunika shuka nyeupe na nyekundu?

Alafu nasikia jana kabla ya saa tatu usiku, siku ya juma tatu mlipigwa tatu na azam likiwemo goli la Bale/Ronaldo...

Alafu ujue tunaweza inunua yanga yote mkabaki "empty set" [emoji2][emoji2]
IMG-20180529-WA0012.jpg
 
Tuna mkodisha wasaliana na Haji Manara [emoji23][emoji23]
_20180530_002828.JPG
 
Hahaha... day! haya maYanga kama maFisiemu.

Natamani siku moja Mungu azifute katika ramani ya dunia hizi timu
1. Yanga
2. Nyoka - koboko
3. Fisiemu
 
Yanga wata msajili tena Nsajigwa sasa hivi [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Screenshot_20180530-004748.jpg
 
Kuandika hujui, unaleta ubishoo kisa una husda na club Tajiri African mashariki na kati. Hivi kwanza unajua Tshishimbi leo kajifunika shuka nyeupe na nyekundu?

Alafu nasikia jana kabla ya saa tatu usiku, siku ya juma tatu mlipigwa tatu na azam likiwemo goli la Bale/Ronaldo...

Alafu ujue tunaweza inunua yanga yote mkabaki "empty set" [emoji2][emoji2] View attachment 789556
Wewe shabiki maandazi mmekuja mjini jana juzi na mbio za mwenge mnajifanya kuijua simba kuliko sisi.. hovyoo sibishani na mashabiki maandazikaa wewe.
 
Naona watu wanamshambulia mleta mada. Mimi naona kwa kiasi fulani yupo sahihi. Kwa sasa hivi Manara alipofika hana tofauti na Jerry Muro alivyokuwa. Wakati mwingine tuache ushabiki uliopitiliza kiasi ambacho tunakuwa vipofu hatuoni mabaya ya mtu. Na Manara hataweza kujirekebisha iwapo tutaendelea kumkingia kifua kwa baadhi ya mambo ya hovyo anayoyafanya. Akifanya mambo mazuri tumsifie kwa haki na akikosea tumjulishe pia bila kupepesa ili aweze kujirekebisha. Lakini hapa wachangiaji wanamzodoa mleta mada na wote wanaomkosoa Manara na kuanza kuwaita eti wao Yanga.

Kiukweli Mo na bodi mpya ya wadhamini wanapaswa kumfunga gavana Manara. Ikumbukwe kuwa Simba na Yanga ni watani wa jadi wa muda mrefu na kutanianiana ni desturi yetu watanzania. Lakini inapofika mtu anatumia lugha isiyo ya staha haipendezi kwa mashabiki wote wa mpira wawe simba au yanga. Manara akumbuke kuwa yeye ni msemaji wa taasisi kubwa sana nchini inayowagusa kuanzia watoto mpaka vikongwe. Hivyo basi wakati anawatania yanga simchagulii utani wa kuwatania lakini namshauri tu atumie busara kujua kuwa message zake zinasikilizwa na kupokelewa kuanzia na watoto walioanza kuwa na akili mpa na vikongwe. Na pia ajue kuwa Simba inabeba nembo za wadhamini mbalimbali iwapo atafanya mambo ya hovyo ajue anawaharibia wadhamini wa simba. Nafahamu kuwa Manara ni mwelewa akielezwa mapungufu yake atajirekebisha atarudi kuwa Manara yule tuliye mfahamu miaka miwili iliyopita ambaye alikuwa bora sana.
 
Kuandika hujui, unaleta ubishoo kisa una husda na club Tajiri African mashariki na kati. Hivi kwanza unajua Tshishimbi leo kajifunika shuka nyeupe na nyekundu?

Alafu nasikia jana kabla ya saa tatu usiku, siku ya juma tatu mlipigwa tatu na azam likiwemo goli la Bale/Ronaldo...

Alafu ujue tunaweza inunua yanga yote mkabaki "empty set" [emoji2][emoji2] View attachment 789556

Hizi akili za kirithi kwa Manara.

Club Tajiri Afrika Mashariki na kati haina hata uwanja, kuwa serious basi.
 
Yanga kutesa kwa zamu, muda wenu wa maumivu umefika.
Mlitukashifu sana nyie jamaa. Nashauri Manara akaze nati zaidi maana iko loose bado.
 
Issue siyo manara issue hapa ni bashite na mjomba wake kama wanayanga 2020 mtafanya mkosa kama yale ya 2015 mtakuja kushuka daraja mtakuja kuniambia hakuna mtu atajitokeza wekeza yanga kwa kuogopa yaliyo mkuta manji tupo hawa watu hawajuwi mpira hawa watu wanachokipenda wao wanataka kiwe tena kwa nguvu ikibidi wakupoteze ili mradi wanachokitaka kiwe
 
Pia sababu nyingine ni Trump na Kim Jon Un.
 
Back
Top Bottom