Mwanzoni nilkuwa nasikia tu kuhusu hiyo "screen shot" nikawa napuuza tu nafikiri watu wasiompenda Manara wamemzushia. Lakini leo ndio nimeiona na kuisoma mara mbili mbili. Kwa kweli kabisa nitashangaa sana iwapo Simba, TFF, Wizara ya michezo na hata serikali wasipomchuikulia hatua huyo jamaa. Kumuacha huyo jamaa afanye anayofanya na akiguswa kidogo tu kelele nyingi kuwa anaonewa kutokana na hali aliyonayo ndio leo kumemfanya awe na kiburi aandike hayo aliyoandika na asipofungwa "speed" gavana tutegemee maandishi yake kuleta balaa kubwa zaidi huko mbele. Akiendelea kuchukuliwa poa ipo siku ataiingiza nchi kwenye taharuki kubwa kwani Simba na Yanga ni timu zilizobeba imani ya mamilioni ya watanzania.
Huyu jamaa nahisi uwezo wake kupambanua mambo ni mdogo sana. Ameshindwa kabisa kujua maudhui ya jumla ya alichoandika sio tu kinaichafua Simba bali mpira wote wa Tanzania na taifa la Tanzania kwa ujumla wake. Huyu akiendelea tu kuchekewa ipo siku Tanzania kama taifa itavuna ilichokiacha kimee maana kama ni mbegu mbaya ilishaota siku nyingi.
Ni mtizamo tu.