Ninakubaliana nawe, na kwa kweli ni jambo linalojulikana toka zamamni kwa sababu taasisi zote viongozi wake ni watu wa CCM.Hizi taasisi za umma kwa sasa ziko kwa ajili ya kukomoa wenye mitazamo tofauti na watawala. Hata ukitazama uundajwi wake, misingi yake ni kudhibiti wenye mitazamo tofauti na serikali. Inshort ni mechanism za kusaidia chama tawala kukaa madarakani kwa shuruti.
Lakini kinachonisikitisha ni jinsi CHADEMA walivyopoa sana kuhusu haya mambo. Ni kama wamefika mahali imebidi na wao wayakubali tu kama watu wengine wote walivyoyakubali kuwa ni mambo ya kawaida.
CHADEMA wanaposhindwa kuendelea kuyashikia bango haya mauchafu ya CCM, sijui ni nani ataongoza mapambano ya ukombozi huo wa nchi yetu.
Kuna kitu hakiko sawa huko CHADEMA.