Haki na wajibu ni sawa na pande mbili za shilingi

Haki na wajibu ni sawa na pande mbili za shilingi

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
678
HAKI NA WAJIBU NI SAWA NA PANDE MBILI ZA SHILINGI.

Na Elius Ndabila
+255768239284

Neno "HAKI" limepata umaarufu sana, hasa vinywani mwa wanasiasa. Wanasiasa wengi hasa wa vyama vya Upinzani wamekuwa wakitumia msamiati huu na kuwaaminisha Watanzania kuwa nchi hii hakuna Uhuru wala haki. Leo stazungumza juu ya Uhuru, nitazungumza juu ya Haki lakini nikinasibisha na Wajibu ili kuweka haya mambo sawa. Huwezi kudai haki kama hujatimiza wajibu. Haki na wajibu ni sawa na pande mbili za shilingi ambapo upande mmoja unapokosekanika basi inaathiri uhalali wa hiyo shilingi.

Hata hivyo ni muhimu kukumbushana kuwa matunda au faida za haki hizi za kibinadamu ni matokeo ya kutimiza wajibu kwa kila mwananchi. Siku zote hakuna haki inayokuja peke yake pasipo wajibu, hivyo mahali penye kudai haki au kutaka kutendewa haki ni lazima kujiuliza kwanza ni wajibu gani ambao umetekeleza ili kupata haki hiyo. Haki ni matokeo ya wajibu ambao umetekelezwa na mtu katika eneo Fulani. Hivyo kwa msingi wa kuwa raia zipo haki ambazo unastahili kuzipata na wajibu wa kutekeleza ili haki hizo zipatikane.

Huwezi kuvunja sheria za nchi na ukaachwa. Ukivunja sheria ni lazima utawajibika na kitendo cha kukuwajibisha ni haki yako kwa kuwa umeenda kinyume na sheria za nchi. Unapovunja sheria ni haki yako kuadhibiwa na unapoadhibiwa usiseme hii nchi hakuna haki, bali tambua kuwa ulishindwa kutimiza wajibu wako wa kutii sheria bila shuruti.

Katiba inaweka wazi kuwa raia wote ni sawa na kila mmoja ana hadhi na uwezo wa kushika madaraka au cheo kutokana na vigezo vya kitaaluma au vingine vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo kuwa na vigezo hivyo haikufanyi tu kuwa kiongozi, bali kuna haki na wajibu wa wapiga kura kufanya maamuzi. Wapiga kura ndio wenye haki na wajibu wa mwisho kukuhalalisha kuwa kiongozi au kukukataa.

Katiba imeweka marufuku juu ya kupata haki yoyote ikiwa ni ya madaraka au cheo kwa misingi ya kabila au jadi au hadhi au nasaba. Kila mmoja apate haki kwa mujibu wa vigezo husika vya kazi au shughuli husika. Kufanya uchochezi ili uchagulike ni kuvunja sheria. Unapohamasisha watu wavunje sheria kwa kuandamana na kulisema vibaya JWTZ unavunja sheria kwa makusudi.Halikadhalika Katiba inaweka mazingira ya kila mtu kuweza kufaidi haki zinazotolewa katika Katiba kwa kuhakikisha kila mmoja anafanya kazi kwa namna ambayo haingiliia haki za mwengine [Ibara ya 29 (5)].

Kama nilivyosema kuwa HAKI na WAJIBU ni vitu vinavyoendana sana ni kama pande mbili za shilingi huwezi kuvitenganisha. Ni muhimu sana kufahamu haki zako kama raia wa Tanzania ili uhakikishe haki hizo zinalindwa. Lakini ni vyema zaidi kufahamu wajibu wako ili utekeleze kila siku na kuhakikisha haki zako zinatimizwa.

Kumbuka ‘kutokujua sheria si utetezi iwapo utatenda kosa lolote’
 
Sisi wa upande wa pili hatuna uhuru tunaogopa kuweka namba zetu tunaogopa kutekwa.
 
Bora kutekwa mkuu kuliko kupotezwa kama Ben wa Sanane na Anzory Gwanda.
 
Back
Top Bottom