HAKI ni neno geni lenye ukakasi, je dhamira yake ni nini?

HAKI ni neno geni lenye ukakasi, je dhamira yake ni nini?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,678
Reaction score
5,166
Mungu ni mmoja hayupo mfano wake,nguvu yake ni kuu hakuna wa kuisambaratisha na duniani kuna sura mbili unaweza kuchagua mwenge au bichwa je,ni njia gani utaitumia kupata matokeo unayoyataka?

Mahubiri ya haki siyo jambo geni katika vichwa vyetu wapo wanazuoni Kama akina aristotle na Plato,Weber na Marcom X wote wameiongelea haki kwa namna ya tofauti ila ningependa kuuliza.

JE,dini inaweza kukupatia haki?

siwahi kusikia hata siku moja kuna mungu wawili mmoja akawa na anakunyima na mwengine akawa anakupa ridhiki,wewe mahubiri ya haki katika dunia ya nyavu nyingi unaitolea wapi?

Haki ni neno la kuzushwa lengo ni kujenga misingi isiyo imara katika kudhibiti hali fulani kwa watu au jamii,kwa mungu kuna haki sababu mwenyewe anajitegemea anachoamua yeye ndiyo sahihi ila kwa binadamu unaongelea haki gani??

Mapokeo ni mabaya sana hasa unapoyapupia kwa ukubwa ila siyo kila kinachong'aa ni dhahabu,tupunguze jazba na joto la kisiasa katika maeneo yetu ya ibada dini haitakiwi kuhubiri siasa,zaidi ni amani na mshikamano.

#Mapendekezo ni vizuri yakatolewa kwenye chemba za uongozi na siyo nje kuzusha taharuki.

Naondoka kama nilivyokuja.
 
Back
Top Bottom