Wakuu,
Nadhani wengi wenu mmeona au kusikia taarifa za mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na Sheikh Said Mwaipopo mnamo Juni 20, 2026, kuelekea maandamano yaliyopangwa ya tarehe 7 Julai (Saba Saba). Katika kauli yake, ametishia kuwepo kwa "kikosi kazi maalum" kitakachowashughulikia waandamanaji kwa madai ya kulinda miundombinu. Alikwenda mbali zaidi na kutoa lugha ya vitisho vya kikatili akisema,
"Tutakayemkamata tutamtahiri bila ganzi...".
View: https://www.youtube.com/watch?v=Ol5xflQ1lJg
Hili jambo linazua maswali mazito sana ya kisheria na kikatiba ambayo kama wadau wa jukwaa hili tunapaswa kuyajadili kwa mapana:
1. Maandamano ya Amani ni Haki ya Kikatiba, si Hisani
Kwanza kabisa, ikumbukwe kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua maandamano ya amani kama haki ya msingi ya kiraia. Kisheria, wananchi wanaopanga kuandamana wanatakiwa
kujaarifu tu Jeshi la Polisi na sio kuomba kibali. Polisi wana wajibu mkuu kisheria wa kuwepo eneo la tukio ili kuwalinda waandamanaji na mali zao, na sio kuzuia haki hiyo au kuruhusu makundi mengine kuingilia kati.
Hapa naomba kunukuu kifungu cha Katiba kinacholinda haki hii:
Uamuzi wa Mahakama Kuu na Sheria ya "Taarifa" (Notification):
Msisitizo wa kisheria hapa unakuja kufuatia
Uamuzi wa Kihistoria wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa Mwaka 1994 katika Kesi ya Rev. Christopher Mtikila v. The Attorney General (Civil Case No. 5 of 1993). Katika uamuzi huo, Mahakama Kuu ilitengua rasmi matakwa ya zamani ya kisheria yaliyokuwa yanawataka raia kuomba "kibali" cha polisi ili kukusanyika au kuandamana. Mahakama ilitamka wazi kuwa sheria inayolazimisha raia kuomba kibali cha polisi inakiuka Katiba na inaminya kwa namna isiyo halali uhuru wa kimsingi wa kukusanyika.
Kufuatia uamuzi huo wa mwaka 1994, chini ya
Kifungu cha 43 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Sadizi (Sura ya 322), utaratibu pekee halali uliosalia ni waandaaji kutoa taarifa ya maandishi kwa mkuu wa polisi wa eneo husika saa 48 kabla ya mkusanyiko. Polisi hawana mamlaka ya kutoa au kuzuia "kibali," bali wajibu wao wa kisheria ni kutoa ulinzi ili kuhakikisha amani inadumishwa na haki ya kikatiba inalindwa dhidi ya vikundi binafsi.
2. Je, Kikosi Kazi cha Mwaipopo Kiko Kisheria?
Katiba ya nchi inasema chombo chenye mamlaka ya kukamata na kuzuia uhalifu ni Jeshi la Polisi pekee. Tamko la raia binafsi au kiongozi wa dini kudai ana kikosi chake cha "kushughulikia" raia wenzake barabarani ni ukiukaji wa wazi wa sheria na ni jaribio la kujichukulia sheria mkononi. Hii inaweza kuzaa machafuko iwapo upande wa pili nao utaamua kuunda vikosi vya kujihami.
Kuhusu suala la mtu yeyote kutishiwa ukatili au kudhalilishwa utu wake na raia mwingine, Katiba inakataza vikali:
3. Fumbo la Ukimya wa Jeshi la Polisi
Hadi sasa, Jeshi la Polisi limekaa kimya utadhani halijasikia kauli hizi za hatari. Ukimya huu unazua maswali mengi ya kiundumilakuwili (double standards):
Mbona upande wa upinzani ukitoa matamko ya kisiasa unashughulikiwa kwa kasi ya ajabu?
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, alikamatwa na hadi sasa
anakabiliwa na mashtaka mazito ya uhaini na uchochezi, ambapo kesi yake bado inaendelea kuunguruma mahakamani huku akiwa kuzuizini. Inakuwaje mtu anayetoa kauli za kisiasa na kukosoa mfumo anashtakiwa kwa uchochezi na uhaini, lakini kiongozi anayesimama hadharani na kutishia kufanya ukatili wa kimwili ("kutahiri watu bila ganzi") na kuunda vikosi haramu vya ulinzi anaachiwa akidunda mitaani bila hata kuitwa polisi kuhojiwa?
Je, ukimya huu hautafsiriwi kama baraka au kibali cha Polisi kwa makundi haya yanayoiunga mkono dola kufanya fujo na kukiuka sheria?
Mjadala:
Wakuu, hivi nchi yetu inaongozwa na misingi ya Sheria na Katiba au inaongozwa kwa matakwa ya kiitikadi? Je, ukimya huu wa polisi kwa Sheikh Mwaipopo huku upande wa pili kama akina Tundu Lissu wakisota mahakamani unajenga au unabomoa taswira ya vyombo vyetu vya usalama?
Karibuni kwa hoja.
🇬🇧 INTERNATIONAL AUDIENCE VERSION
TITLE: CONSTITUTIONAL RIGHTS VS PRIVATE MILITIAS: WHAT DOES THE SILENCE OF THE POLICE FORCE REGARDING SHEIKH MWAIPOPO’S THREATS MEAN?
Dear members,
I believe most of you have seen the footage or heard about the press conference held by Sheikh Said Mwaipopo on June 20, 2026, regarding the planned demonstrations on July 7th (Saba Saba). In his statement, he threatened the existence of a "special task force" that would deal with the demonstrators under the guise of protecting infrastructure. He went further to use harsh, cruel words of threat, stating,
"Whoever we catch, we will circumcise them without anesthesia...".
This incident raises heavy constitutional and legal questions that we, as stakeholders of this platform, need to discuss extensively:
1. Peaceful Demonstration is a Constitutional Right, Not a Privilege
First and foremost, it must be recalled that the Constitution of the United Republic of Tanzania recognises peaceful demonstration as a fundamental civil right. Legally, citizens planning to demonstrate are only required to
notify the Police Force and not to beg for permission. The police have one primary legal obligation:
to be present at the scene to protect the demonstrators and their property, rather than stopping the exercise of this right or allowing other groups to interfere.
Here, let me quote the specific constitutional provision protecting this right:
The High Court Precedent and the "Notification" Requirement:
This legal standpoint is heavily backed by a landmark
1994 Tanzanian High Court Ruling in the case of Rev. Christopher Mtikila v. The Attorney General (Civil Case No. 5 of 1993). In this watershed judgement, the High Court decisively struck down old statutory provisions requiring citizens to acquire a police "permit" before holding a public assembly or demonstration. The Court boldly declared that forcing citizens to seek permission fundamentally infringes upon the constitutional freedom of assembly.
Consequently, following that 1994 precedent and under
Section 43 of the Police Force and Auxiliary Services Act (Cap 322), the operational protocol is restricted strictly to a 48-hour prior written notification to the officer in charge. The police have absolutely no legal powers to issue or deny a "permit"; their statutory mandate is solely to regulate traffic, maintain public order, and shield peaceful demonstrators from external interference or private actors trying to hijack the law.
2. Is Mwaipopo's Task Force Legally authorised
The country's Constitution explicitly states that the only institution with the mandate to arrest, investigate, and prevent crime is the Police Force. A declaration by a private citizen or a religious leader claiming to have his own militia to "deal" with fellow citizens on the streets is an open violation of the law and an attempt to take the law into his own hands. This could trigger chaos if the opposing side also decides to form self-defense forces.
Regarding the issue of anyone being threatened with violence or having their human dignity degraded by another citizen, the Constitution strictly forbids it:
3. The Mystery of the Police Force's Silence
Up until now, the Police Force has remained completely silent, acting as if they haven't heard these dangerous remarks. This silence raises many questions about double standards:
Why is it that when the opposition issues political statements, they are dealt with at an incredible speed? CHADEMA Chairman, Tundu Lissu, was arrested and currently faces serious charges of treason and incitement, with his case still
roaring in court while he remains in detention. How is it that a person making political remarks and criticizing the system is prosecuted for incitement and treason, yet a leader who stands publicly and threatens physical cruelty ("circumcising people without anesthesia") and forms illegal security forces is left roaming the streets without even being summoned by the police for questioning?
Does this silence not translate to an indirect endorsement or permission from the Police for these pro-state groups to cause chaos and violate the law?
Discussion Point:
Members, is our country guided by the principles of Law and the Constitution, or is it ruled by ideological preferences? Does this silence of the police regarding Sheikh Mwaipopo, while the other side like Tundu Lissu suffers in court, build or destroy the image of our security organs?
Welcome for your arguments.