sio kweli kuwa hakuna mtoto wa nje, mtoto wa nje yupo na sheria inatambua kuwa huyo ni mtoto wa nje. maana ya mtoto wa nje ni kwamba, huyo ni mtoto wa nje ya ndoa.watoto wanatakiwa kutokana na ndoa, kama hawajatokana na ndoa wanaitwa watoto wa nje. kama ni kupata haki wanaweza kupata haki lakini ile status yao kama watoto wa nje ya ndoa haibadiliki kwasababu sio watoto wa ndani ya ndoa.
kitu cha muhimu kuelewa ni kwamba, kama unao watoto wa nje ya ndoa, hawawezi kupata haki zao hadi pale utakapowathibitisha/wakomboa. maana ya kuwathibitisha/kuwakomboa kuna namna nyingi kutokana na makabila mbalimbali ya Tanzania, wengine wanapeleka ng'ombe kwa wazazi wa mama mtoto, wengine wanaenda na washenga na kutoa fungu la pesa kutambulisha kuwa mtoto huyo ni wa kwao hivyo awe included kwenye ukoo wao etc.hatari yake ni kwamba, mfano kwa sheria za mirathi, kama hautamthibitisha kwa namna hiyo na akawekwa wazi kuwa ni mtoto wako, ukifa hawezi kurithi mali zako kabisa labda kama umeandika kwenye wosia lakini si kwasababu yeye ni mrithi halali.
pili, huwezi kuondoa dhana ya mtoto wa nje ya ndoa kwamba ipo, kwasababu kwamfano kwa dini ya kiislam, mtoto wa nje ya ndoa ni haram hata akithibitishwa hatambuliki katika dini hiyo, na sheria mfano; za mirathi za kiislam haziwezi kumtambua kabisa. ni mtoto wa uzinifu/haram na huwezi kukukifanya kitu haram kuwa si haram.
utanisamehe sana, kwasababu najua wengi humu ni watoto wa nje ya ndoa, Mungu anawapenda kuliko wanadamu, hata kama dunia itawakataa Mungu anawatambua. kuna umuhimu sheria zetu kuwekwa vizuri zaidi ya hapa ili watoto wote wapate haki zote, pamoja na kwamba, utakatifu wa ndoa nao ni muhimu sana, in order to keep the sanctity of marriage, children born out of wedlock wasiwe kama ni altenative.
View attachment 115643
View attachment 115644View attachment 115644