Haki ya mtoto huyu wa nje ya ndoa ikoje?

Haki ya mtoto huyu wa nje ya ndoa ikoje?

swali la mtaka ushauri uksoma mwishoni linauliza "sheria au haki ya huyu mtoto ikoje." kwa kuuliza hvo swali lnakuwa halieleweki kwani ukijibiwa anahaki na sheria kama mtoto sidhani kama jibu ltakutosheleza. Sikusaidii kutunga swali ila nahtaji ufafanuzi, hyo haki ya huyo mtoto unaiulizia ktk nyanja gan. Je? Maisha yake binafsi/maisha yake na ndoa yenu mkiwa wote mpo/mirathi ya baba yake au kwenye nin hasa? Ukijarbu kusoma wengi wamekimbilia kukushauri kwenye swala la mirathi.
 
wakati mwingine sitakagi kabisa zungumzia maswala haya mimi kama mwanamke akili yangu imenituma na nimejiwekea kuinvest kila mtoto wangu awe na sehemu ambayo atarithi kwa kuanzia maisha yake serious ,sitaki khabari yakurithi mali za baba blablabla naumia sana kwa kweli
 
Hakukuambia kwa sababu ya woga wa kukupoteza. Elewa hilo kwanza.

Pili, mtoto mwenye umri say wa miaka 20 huwezi kumkumbatia na kumpenda kama wa kwako. Amelelewa malexi tofauti kabisa na ulivyolea wanao, utabahatika kama ana tabia nyingi za kupendeza lakini usiwe na mategemeo makubwa sana kuhusu yeye kwa sababu humjui. Mkubali, msamehe mumeo na endelea na maisha yenu.

Sheria hailazimishi umtunze wala kuishi nae. Mfanye kama binamu za wanao. Aje kuwatembelea. Lakini hana haki ya kurithi chochote ulichochuma na baba yake, hiyo ni wazi. Katika maongezi usilitaje sana hili ili upate habari za ziada.

Pole Mitihani, muambie mumeo akuambie mengine anayokuficha.

Hapo kwenye red mh! Hiyo ndiosheria isemavyo au utakavyo wewe, wewe unafugu lako na baba yake anafungu katika mali hiyo, iweje asirithi fungu la baba yake? Kama kweli kunasheria hiyo basi ni kadhalimu sana, mtoto anakosa gani hadi akose share ya baba yake katika mali.


NB:kama unazungumia sheria ya dini basi sina lakusema.
Lakini kama sheria ya serikali inabidi ibadishwe haraka sana.
 
Last edited by a moderator:
una uhakika aisee? ina maana mama yake yeye ale maisha huko na kulala gesti hausi na mie nnaekula shurba hapa tunapandisha tofali pamoja na baba yao then tugawane?
kama kweli sheria inasema hivyo juu ya urithi nadhani ni makosa kabisa. na je mama akizaa na mtu mwingine ilhali ndani ya ndoa, hiyo sheria nzuri inasemaje juu ya urithi? manake yanatokea hayo na tunayaona

Sheria ndivyo inavyosema mtoto wa nje anahaki ya kurithi na anahaki ya kuhudumiwa kama watoto wengine. The same applies kwa mtoto wa nje wa mama.
Mfano: mie baba yangu anawatoto wa nje ambao wanatambulika.home na kwenye ukoo. Baba anawahudumia na pia ameandika will kila mtoto anachake.
Ndo maana nimemshauri waandike will, likitokea la kutokea kinga yake ni ile will.
 
Sheria mpya ya watoto ya mwaka 2009 imeleta mabadiliko makubwa sana. Mtoto wa nje katika sheria ya zamani hawakuwa na haki ya kurithi,katika sheria mpya mtoto huyu anahaki zote kama watoto waliozaliwa ndani ya ndoa.
Na baba wa mtoto huyu anawajibu wa kumtuza kama watoto wengine na anahaki ya kuwafahamu ndugu zake wote.
Kama mmeo akifariki (god forbid), mtoto anahaki ya kurithi na pia kuhudumiwa kama watoto wengine. Haijalishi kama aliletwa nyumbani au laa. If he can prove kuwa yule ni baba yake na alikuwa anamuhudumia, then he is very much entitled.
Sasa ilikuondokana shari baadae, andikeni will, muende kwa mwanasheria awasaidie. Na pili amjenge huyu mtoto nyumba au ata amnunulie kiwanja amuachie.

Ni kweli juu ya Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 imeanisha kuwa mtoto wa nje ya ndoa anaweza kurithi, suala ni je, sheria hiyo mpya ina provision inayoonyesha kuwa vipengele vyote vya Sheria ya ndoa na sheria za mirathi vinayoonyesha mtoto wa nje ndoa asirithi vinafutwa?
 
Hiphop, conflict ndo ipo hapo.But it all comes down to how u present ur arguments in court. Isijasikia any precedent on that or niseme sijafwatilia kama kuna any precedent inayozungumzia hiyo ishu.
But all in all, hiyo sheria inayozunguzia mtoto wa nje asirithi is primitive au unfair. Thats why ilibadilishwa na the new law. Any judge or magistrate would be absurd to render the primitive law valid epecially with the existance of the 2009 law of the child act.
 
Last edited by a moderator:
Baada ya kuoana na kuzaa watoto 4 na kuishi kwenye ndoa pamoja kwa miaka 15 na kuchuma mali zetu pamoja maana wote ni watumishi na kuandika majina yetu mawili kama wamiliki.
Mume anakuja kusema kabla hajanioa alikuwa na mtoto alizaa anaomba nimtambue. Hapa sheria au haki ya huyu mtoto ikoje?

Mgawie urithi au atapata urithi wa baba ake kisheri inaruhusiwa baba kuamua kugawa baadhi ya urithi wake kwa mtu ampendae
 
Hiphop, conflict ndo ipo hapo.But it all comes down to how u present ur arguments in court. Isijasikia any precedent on that or niseme sijafwatilia kama kuna any precedent inayozungumzia hiyo ishu.
But all in all, hiyo sheria inayozunguzia mtoto wa nje asirithi is primitive au unfair. Thats why ilibadilishwa na the new law. Any judge or magistrate would be absurd to render the primitive law valid epecially with the existance of the 2009 law of the child act.

Taxbabe, mpaka sasa sijapata pia kusikia kwenye mahakama yoyote ile conflict ya aina hiyo imejitokeza, mpaka sasa case law iliyotajwa kwenye thread hii imekuwa ikitumika sana kuwanyima watoto wa nje ya ndoa haki ya kurithi, natamani nione hukumu itakayokuja na mtazamo tofauti ya mahakama kuu ili wanasheria waweze kuomba directives Mahakama ya Rufaa ili tupate mwelekeo mpya katika hili suala.
 
Sheria ndivyo inavyosema mtoto wa nje anahaki ya kurithi na anahaki ya kuhudumiwa kama watoto wengine. The same applies kwa mtoto wa nje wa mama.
Mfano: mie baba yangu anawatoto wa nje ambao wanatambulika.home na kwenye ukoo. Baba anawahudumia na pia ameandika will kila mtoto anachake.
Ndo maana nimemshauri waandike will, likitokea la kutokea kinga yake ni ile will.

Hivi wale watoto ambao mama zao huwadanganya kuwa baba mwenye nyumba nj baba yao huju akijua siyo kweli wanaitwaje hao? Kweli wanadhaniwa ni wa ndani lakini ni nje kisawasawa. Baba anakuwa anaambiwa mtoto anafanana na bibi mzaa babu au babu mzaa mama.
 
Inafanana na hii:

[h=1]Amezaa Nje Ya Ndoa, Mume Anajua Na Ameridhika, Mtoto Apewe Jina La Baba Yupi Kati Ya Wawili – Nini Hukmu Ya Mirathi?[/h]

SWALI: Asalaa alaykum. Mimi nina swali mbalo nimejaribu kulituma kupitia kwenye website yenu limekataa, hivyo basi ndio maana nimetumia private e-mail adr. Nilikua nauliza, Kama mume hamsikilizi mkewe kwa lolote lile. Mke akijaribu kuongea na mume lakini mume hataki hata kusikiliza, nakama alikua na safari basi huvaa viatu nakutoka. Na wakati mwengine kama mume alikua anangalia TV basi huongeza na sauti kabisa. Hali hiyo iliendelea mpaka siku moja mke akajikuta anatoka nje ya ndoa na kuzini. Wakati huohuo mke alimpenda sana mumewe na hakuchoka kupigana na hali hiyo. Siku moja mume akamjia mkewe na kumuomba samahani kwa yote na akaomba wasameheane ili walee watoto wao wawili wa kiume. Na mke bila ya kusita wakasaeheana na wote wamekuwa ni wafanya ibada mchana na usiku kwa ajili ya kumuomba mwenyeezi mungu awasamehe madhambi yao waliyoyatenda na waliotendeana. Na mume alifaham ya kwamba mkewe alikwenda nje ya ndoa. Lakini wakati huo mtihani mgumu ukawajia, mke alijikuta ni mja mzito wa mtu mwengine na akaogopa kumuambia mumewe. Na vile vile mke aliogopa dhambi ya kutoa mimba ni kama ya kuua hivyo basi akaamua kuzaa. Baada ya mtoto kuzaliwa kukapita kama kipindi cha miaka miwili mke hana raha kwa sababu ya siri hiyo. Na mungu mkubwa mume huyo akaligundua hilo na kumuuliza mkewe na mke hakukataa akasema ukweli. Mume huyo alijilaumu sana ya kwamba yote hayo aliyasababisha yeye kutokusikilizana na mkewe. Na akamuambia mkewe ya kwamba najua kwenda nje ilikua uamuzi wake hakuna aliyemshauri kufanya vile. Lakini kwa kuwa yeye ndio aliye lea ujauzito na mtoto mpaka akazaliwa na akafikisha miaka 2 basi yeye anaona ni bora wasameheane na waendelee kuishi na kulea watoto wao kama kawaida. Sasa hali kama hiyo, kwa sababu baba mzazi wa mtoto huyo alifaham ya kwamba huyo mwanamke alikua mke wa mtu. Je baba huyo anastahili kupata haki kama baba? na kivipi? Na je kama ilivyo kidini yetu mtoto huyo anastaili kutumia ubini upi, wa baba amleae au huyo baba mzazi? Vile vile mtoto ikibidi alitumie jina la baba mzazi je hali hiyo si inaweza ikasababisha baba mlezi kupata hasira na labda kutokea kumchukia mtoto huyo. Na haswa ukizingatia wote mke na mume wameamua kuwa wachamungu. Halafu pia kwenye maswaala ya Mirathi inakuaje ikiwa mke na mume huyo wanashirikiana wote katika maswala ya kuzalisha mali kwa ajili ya watoto wao na urithi wao hapo baadae? Shukran. Neema na Amani zake Allah ziwashukie ninyi mnaoutumia muda wenu kwakuielimisha jamii ya kiislam. Mwenyeezi mungu awazidishie kila la kheri hapa duniani na a kesho akhera, na pia awarahisishie yaliyoko magumu kwenu.
JIBU: Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuzaa nje ya ndoa. Mwanzo tunawapatia pongezi hao wanandoa ya kuweza kusameheana kwa yote yaliyopita baina yenu na kuanza maisha yetu mapya kwa kumuabudu Allaah Aliyetukuka na kuendea uchaji Mungu. Hata hivyo, mara nyingi yanayotupata kisha tukajuta ni kwa yale yaliyochuma mikono yetu. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Na misiba inayokupateni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu, na juu ya hivi Allaah Anasemehe mengi” (42: 30). Kwa hiyo, yaliyopita yamepita lakini baada ya hapo wanatakiwa wasifanye makosa mengine, ambayo yanaonekana ya kwamba yatakuja kutokea kwa kuzaliwa mtoto huyo nje ya ndoa. Baba wa nje ya ndoa hana haki yoyote kwa mtoto anayezaliwa mbali na kwamba ni damu yake, shari'ah ya Kiislamu haimtambui kabisa. Na huyo mume pia si baba wa huyo mtoto na hilo linatakiwa lifahamike vyema ili wasije wakadhurika wengine na kukosa haki. Shari'ah ya Kiislamu inatufahamisha kuwa mtoto wa nje ya ndoa anaweza kumrithi mama yake mzazi lakini hawezi kumrithi wa kurithiwa na baba wa kibayolijia wala mume ambao amemkubali huyo mtoto kumlea. Pia haifai huyo mtoto kuitwa kwa jina la mwanaume aliyemtia mimba huyo mke au huyo mume wa halali. Linalotakiwa ni huyo mtoto kuitwa kwa ubini wa mama yake au kwa ubini wa ‘Abdullaah. Kwa mfano ikiwa mtoto jina lake ni ‘Uthmaan, anaweza kuitwa ‘Uthmaan bin Maryam (kwa jina la mama) au ‘Uthmaan bin ‘Abdillaah. Huyo baba mwenye kumlea ndio atakuwa na haki ya ulezi kwani atakuwa ni kama baba yake ilhali mwengine hatokuwa na haki yoyote. Ama kuhusu mas-ala ya mirathi, mtoto huyo aliyezaliwa nje ya ndoa ataweza kumrithi huyo mama yake na huyo mama kumrithi yeye. Ikiwa mali mnazalisha nyote mnaweza kufanya hesabu ya mgao wa kila mmoja, na lile fungu la mama ndilo linaloweza kurithiwa na huyo mtoto pindi mama huyo atakapofariki. Na Allaah Anajua zaidi

Source: Amezaa Nje Ya Ndoa, Mume Anajua Na Ameridhika, Mtoto Apewe Jina La Baba Yupi Kati Ya Wawili
 
kinauche, Kama ikigungulika mtoto sio wako, huyo mtoto atakuwa ni mtoto wa nje (illegitimate child). Kwa maana hiyo sheria haikulazimishi kumhudumia huyo mtoto. Na incase mama yake akifa, huyu mtoto atakuwa entitled urithi wa mali za mama yake this is according to the law of the child act 2009. Hata hivyo sheria za kimila zinasema mtoto wa ndani ya ndo ni wa baba na mtoto wa nje ya ndoa ni wa mama. So automatically huyu mtoto atakuwa jukumu la mama na baba yake mzazi (biological father).
Na pia huyu mtoto anahaki ya kuwafahamu ndugu zake. So kama kuna watoto uliozaa na huyo mama, huyo mtoto anahaki ya kuwafahamu.
 
Last edited by a moderator:
kinauche, Kama ikigungulika mtoto sio wako, huyo mtoto atakuwa ni mtoto wa nje (illegitimate child). Kwa maana hiyo sheria haikulazimishi kumhudumia huyo mtoto. Na incase mama yake akifa, huyu mtoto atakuwa entitled urithi wa mali za mama yake this is according to the law of the child act 2009. Hata hivyo sheria za kimila zinasema mtoto wa ndani ya ndo ni wa baba na mtoto wa nje ya ndoa ni wa mama. So automatically huyu mtoto atakuwa jukumu la mama na baba yake mzazi (biological father).
Na pia huyu mtoto anahaki ya kuwafahamu ndugu zake. So kama kuna watoto uliozaa na huyo mama, huyo mtoto anahaki ya kuwafahamu.

Asante kwa ufafanuzi
 
Last edited by a moderator:
Ikumbukwe kwamba huyu mtoto anamama yake ambaye pia anamwandalia maisha yake ya baadae.
Napata na kigugumizi ni vipi aje kurithi mali nilizowachumia wanangu? Bora angekuwa anaishi na sisi tunashirikiana kwa namna moja au nyingine, yeye anaishi na mama yake alafu mwisho wa siku aje kurithi kwenye nyumba ambayo alikuwa hatambuliki???.
Na je vitu tumeandika majina mawili la kwangu na la baba yake ni vipi hapo nifafanulieni tafadhali kwa busara hakuna haja ya kupanick.
 
Sheria mpya ya watoto ya mwaka 2009 imeleta mabadiliko makubwa sana. Mtoto wa nje katika sheria ya zamani hawakuwa na haki ya kurithi,katika sheria mpya mtoto huyu anahaki zote kama watoto waliozaliwa ndani ya ndoa.
Na baba wa mtoto huyu anawajibu wa kumtuza kama watoto wengine na anahaki ya kuwafahamu ndugu zake wote.
Kama mmeo akifariki (god forbid), mtoto anahaki ya kurithi na pia kuhudumiwa kama watoto wengine. Haijalishi kama aliletwa nyumbani au laa. If he can prove kuwa yule ni baba yake na alikuwa anamuhudumia, then he is very much entitled.
Sasa ilikuondokana shari baadae, andikeni will, muende kwa mwanasheria awasaidie. Na pili amjenge huyu mtoto nyumba au ata amnunulie kiwanja amuachie.
elezea ana haki kivipi na weka vifungu vya sheria hapa. i will come back to this with authorities.
 
Dunia inawakataa kivipi wakati umesema ni dini - yani Mungu - ndio anawakataa?

Halafu hapo hapo unarudi kinyume nyume unajaribu kumpa Mungu credit kwa kuwapenda hawa watoto wakati wewe mwenyewe umesema ni watoto wa uzinifu na ni haramu na hawatakasiki hata ufanyeje! Sasa kama ni watoto haramu hiyo haramu ni kwa mujibu wa nani, shetani? Haramu kwa Mungu no less! Mbona mnapenda kumfagilia huyu Mungu kwa vitu senseless vinavyodhihirisha kwamba dini hai make sense at all?


technical comment, a very rare brand at JF.
nilijua labda umeeelewa, sahamani. but, unaongea kutokana na hisia au unaongea vile sheria inavyosema? do you have any knowledge of this type of law?
 
Umesite kesi ya mwaka 90 kama precedent? Najua hiyo kesi mnasoma vyuoni sababu ndo ni ya CAT na ndo TLR mlizonazo kwa wingi..lakini Hujui position imebadilika hasa baada ya kuja into force The Law of the Child Act,2009 iloanza rasmi kutumika mwaka 2010?
naomba sisi sote tuje na vifungu vya sheria ya watoto namba 21 ya 2009 vinavyosema hivyo, hapo ndio tutaelewana. kwa mfano:

Section 36(4) of the Law of the Child Act No.21 of 2009 kinasema;

(4) Where the court has made an order on a biological father,
such biological father shall assume the responsibility to the child
in the same manner as may be in respect of a child born in
wedlock and the child shall, subject to religious belief of the
biological father, have such other rights devolving from the parent
including a right to be an heir.

kwanza kabisa, hapo inaonyesha kumbe kuna watoto waliozaliwa in wedlock na wale wa out of wedlock, na kama mahakama ikishapata uthibitisho kuwa mwanaume fulani ni biological father wa mtoto fulani, inaweza kutoa order ya baba huyo kumtunza mtoto na mtoto huyo ataweza kurithi hata mali za mwanaume huyo LAKIN its subject to religious belief of the biological father. hapa ina maana kwamba, kwamfano kwa waislam mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ni haramu na hawezi kurithi, hivyo kama mwanaume ni mwislam mtoto wa kambo asitegemee kurithi pale.

hata hivyo kuna mwanya wa kurithi hata kama mtoto wa kambo lakini hatarithi kama ni mrithi halali/mtoto bali atarithi kama mtu baki tu kwa kugawiwa toka kwenye ile 1/3 ya ruhusa ya kwenye wosia kama vile tu ambavyo mwanaume huyo angempa kwenye wasia mtu yeyote baki. yaani pale hampi kwenye wosia kama mtoto wake au mrithi wake anampa kwenye wosia kama mtu baki tu, na lazima awe ni mwislam. however, watoto hawa kwa waislam ataweza kurithi toka kwa mama kama ni mwislam.

kwa habari ya dini nyingine, i think its just a matter of argument and evidence in court, hata kama hatuna precedent.

bofya hapa sheria ya watoto ya 2009. View attachment 116166
 
Back
Top Bottom