Hakuna mtoto anaitwa wa nje tafadhali sana heshimu haki za watoto na kwamba huyo mtoto kama mumeo alimzaa kabla ya kuwa nawe na kwamba kosa lake ni kutokukuambia mapema bado hailalalishi wewe kumwita ni mtoto wa nje na kwa minajili hiyo ni kama unataka kusema humtambui
Jitahidi uondokane na roho ya namna hiyo na jifunze kukubali uhalisia kwani hata kama ukimkataa atabaki kuwa ni mtoto wenu au wako kama utamkumbatia kwa dhati na kumpenda kama uliyemzaa mwenyewe, kama ungekuwa ni wewe mezalishwa na mwanaume ambaye baadae akakukacha na baadae akataka kumhudumia mwanao ungekataaa?
kila mtoto anahaki na kwamba neno mtoto wa nje halipaswi litamkwe kwenye vinywa vya watu wenye kujua maana ya utu