sijakushauri wewe au mwingine chochote bali nasema wapalestina wanaonewa,vyombo vya kidunia vinavyohusika viwatetee.
Kama Dunia inataka amani mashariki ya kati, kama inataka wapalestina na Wayahudi waishi kwa amani, lazima itafutwe njia ya kuidhibiti Iran. Iran ndiye shetani mkubwa hapo Mashariki ya kati, siyo tu kwa Wayahudi na wapalestina bali kwa nchi zote za Mashariki ya kati.
Mazungumzo yalikuwa yanaenda vizuri, mpaka Wapalestina wakapewa mamlaka yao ya ndani, wakawa na Serikali yao, na kufuatia makubaliano yale ya wakati wa utawala wa George Bush, aliyesimamia makubaliano kati ya Israel na Wapalestina, ilikuwa zoezi la Wapalestina kupewa nchi kamili liende hatua kwa hatua. Kwanza wapewe mamlaka ya ndani, wakati huo kuwe na ufuatiliaji wa kuona kama wapalestina hawataishambulia Israel, maana hofu kubwa ya Israel ni kuwa na Taifa hasimu kwenye mipaka yake. Mambo yalienda vizuri mwanzoni, lakini Iran haikutaka, ikiwa imeshikilia falsafa yake kuwa Wayahudi hawastahili kuwepo Duniani, na wapalestina wamefanya makosa kufanya makubaliano na wazayuni ambao dini yao inasema hawatakiwi kuwepo Duniani, wanatakiwa kuangamizwa; Iran ikaanzisha kundi la kigaidi la Hamas, kwanza kundi hili la kigaidi likaipiga Serikali ya Palestina, ikateka eneo la Gaza, na kuanzisha utawala wake uliokuwa adui wa utawala wa Ramallah, na kisha ikaanza kufanya mashambulio ya kuwaua wayahudi. Serikali ya Israel ikachukua msimamo mkali dhidi yao maana hujui yupi anakusogelea kwa nia njema na yupo kwa dhamira mbaya, ikajenga uzio, lakini hamas wakawa wanaoenya na kwenda kuwashambulia Israel au kuwaua wapalestina wanaonekana kuwa karibu na Israel. Wawo wanachotaka ni kuwepo na uhasama mkubwa.
Hivyo ufahamu kuwa, hata leo hii Israel ikatangaza kuwapa nchi Wapalestina, Iran haitakubali, itaitumia nchi hiyo ya Palestina kujijenga na kuanzisha mapigano dhidi ya Israel.
Ufahamu kuwa makundi ya kigaidi ya Iran, yalizipiga Serikali za Lebanon, Yemen, Syria, na sasa Iraq. Serikali za nchi hizo zimebakia serikali jina lakini wenye nguvu ni hayo makundi ya kigaidi. Ndiyo maana serikali za nchi hizo zinaisaidia Israel kwa kuipa taarifa za kiintelijensia kwa siri.
Bila kudhibitiwa Iran, Mashariki ya kati, yote ipo hatarini. Tatizo ni Iran, nchi inaongozwa na kiongozi wa dini ambaye ana imani kwamba Serikali katika nchi zote Duniani zinatakiwa kuwa kwa mujibu wa quran, na sheria inayotakiwa kufuatwa Duniani kote ni Sharia Law. Na anaamini kuwa siku moja Dunia yote itakuwa ya waislam, na serikali itakuwa moja tu inayofuata sharia law, na hivyo ili kulifikia hilo, Duniani kote waislam wote wanatakiwa kupambana kuhakikisha hilo linatokea. Falsafa ya Iran ni hatari kwa usalama wa Dunia nzima.