Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
5G3TVR.png

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
Katiba ya nchi inasemaje kuhusu ukomo wa urais?

Na kama unapingana na katiba huoni kama unavunja sheria?

Katiba sio msahafu, inabadirishwa kilwa inapoonekana inafaa.

Sasa ni wakati wa kuibadirisha ili Mhe Rais aongezewe mitano tena
 
wapinzani muwe na akili pia hiv mtu unamlazimisha vip apende unachopenda ww? yeye anapenda Mh Rais aendelee kuwepo ww hupendi sio shida. onyesha kutopenda ila sio matusi
 
Nyenyenyeeeeeeeeh my foot , kuna siku nitatukana tusi hapa JF siku hiyo ndio Mods watanifungia Account kabisa, huu ujinga wa kiwango cha hali ya juu .

Katiba ibadilishwe kwaajili ya kurefusha kipindi cha uraisi madarakani, badala ya kupigania katiba ibadilishwe kwa manufaa ya watanzania wote , wewe unataka wabadilishe kwaajili ya uraisi tu . Shame upon you.

Raisi mwenyewe ameshasema hataki kuongeza muda wake madarakani wewe na genge lako la wapumbavu mnashabikia kinyumbu nyumbu tu, aongezeeeeee aongezeeee nyumbu mnamatatizo sana aise.

Katiba itabadilishwa kwa manufaa ya watanzania wote, sio kwa matakwa yenu nyie watu wachache ambao hamjui nini maana ya katiba na demokrasia , nachelea kusema tunasafari ndefu sana katika kuikomboa nchi yetu mikononi watawala wasiojielewa na wasiojali wanachi kwa ujumla.

Nawasilisha
 
kila siku tunapiga kelele haki ya kutoa maoni ndio hayo sasa! mnachukia nini wewe toa unayohisi ni sahihi
 
Ingawa sijasoma ila heading yako inajipinga yenyewe..., je inaruhusiwa Kikatiba mtu kuongeza muda wa Urais (current Katiba) au ni haki yako Kikatiba kushawishi ili Katiba ivunjwe ?
 
Desturi yetu ni miaka 10 tu! Nchi hii bado ina viongozi wazuri wenye uwezo wa kuivusha nchi.
Pia hili suala halipo kwenye ilani yetu ya uchaguzi.
Nadhani ungeongelea kuhusu utekelezaji wa ilani ungefanya jambo la msingi sana kuliko kuwaza kuongeza muda wa urais.
 
Nyenyenyeeeeeeeeh my foot , kuna siku nitatukana tusi hapa JF siku hiyo ndio Mods watanifungia Account kabisa, huu ujinga wa kiwango cha hali ya juu .

Katiba ibadilishwe kwaajili ya kurefusha kipindi cha uraisi madarakani, badala ya kupigania katiba ibadilishwe kwa manufaa ya watanzania wote , wewe unataka wabadilishe kwaajili ya uraisi tu . Shame upon you.

Raisi mwenyewe ameshasema hataki kuongeza muda wake madarakani wewe na genge lako la wapumbavu mnashabikia kinyumbu nyumbu tu, aongezeeeeee aongezeeee nyumbu mnamatatizo sana aise.

Katiba itabadilishwa kwa manufaa ya watanzania wote, sio kwa matakwa yenu nyie watu wachache ambao hamjui nini maana ya katiba na demokrasia , nachelea kusema tunasafari ndefu sana katika kuikomboa nchi yetu mikononi watawala wasiojielewa na wasiojali wanachi kwa ujumla.

Nawasilisha

Na watanzania ndio sisi;

Kwani kuna ubaya gani? Sisi 84% tuliompigia kura ndio tunataka aendelee kuongoza nchi.

Kama wewe hautaki ni haki yako pia
 
Bora kuwa na ulemavu wowote ule, ila sio ulemavu wa ubongo. Nchi hii unataka utulivu tulionao uondoke nao, kiazi hebu badilika, yaaani wapumbavu wanazaliwa kila uchwao hii nchi. Mtanzania gani utamweleza huuu upuuzi akuelewe? zaidi ya wachumia tumbo wachache na wenye akili Kama zako
 
Ingawa sijasoma ila heading yako inajipinga yenyewe..., je inaruhusiwa Kikatiba mtu kuongeza muda wa Urais (current Katiba) au ni haki yako Kikatiba kushawishi ili Katiba ivunjwe ?

Nashawishi ili tubadirishe katiba ya sasa inayomnyima haki ya kuendelea na nngwe ya tatu Mhe. Rais.

So sivunji katiba, ila nashawishi ili tubadili katiba
 
Desturi yetu ni miaka 10 tu! Nchi hii bado ina viongozi wazuri wenye uwezo wa kuivusha nchi.
Pia hili suala halipo kwenye ilani yetu ya uchaguzi.
Nadhani ungeongelea kuhusu utekelezaji wa ilani ungefanya jambo la msingi sana kuliko kuwaza kuongeza muda wa urais.
Mimi mwenyewe mwana Ccm mzuri sana, lakini najua tuna ilani yetu inayotuongoza na kutupa dira , hawa watu sijui wanatokea wapi?

Mwenyekiti amesema hataki kuongeza muda wenyewe wanakaa kila siku ongezaaaaaa ongezaaaaah, sasa sijui wanataka nn?

Utaratibu wetu ni kupokezana vijiti na katiba imesema ni miaka 10 full stop.
 
Desturi yetu ni miaka 10 tu! Nchi hii bado ina viongozi wazuri wenye uwezo wa kuivusha nchi.
Pia hili suala halipo kwenye ilani yetu ya uchaguzi.
Nadhani ungeongelea kuhusu utekelezaji wa ilani ungefanya jambo la msingi sana kuliko kuwaza kuongeza muda wa urais.

Usinipangie cha kuongea. Wewe ongelea Ilani mimi nitaongelea katiba.

Kwani kila linalofanyika lazima liwe kwenye ilani?

Hapa issue ni Katiba ibadirishwe kwa kufuata process zote na sheria za nchi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom