Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
5G3TVR.png

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
Haijawahi kutokea , wala haitakuja kutokea , kwa watawala walio mfuatisha Mwl. Kupendwa na kulazimishwa kubaki madarakani hata siku moja. Ukweli unajulikana na wewe unajua pia .

Haki kila mtu anayo hakuna asiye na haki, sote tuna haki ya kukubali au kupinga jambo fulani .

Unayo yaendeleza ni mawazo yako binafsi, hata mwenyekiti wako hayataki. Kwa ushahidi polepole alioleta bungeni siku sio nyingi.

[emoji117]Unataka kutuambia wewe na polepole nani anajua zaidi maswala ya ndani ya chama?

[emoji117]Unataka kusema wewe na mwenyekiti wa chama nani anamaamuzi juu ya kuongoza taifa na undani wake?

[emoji117]Unataka kutuambia kuwa alichokisema mwenyekiti kuwa hata ongeza muda wa madaraka sio sahihi?

[emoji117]Mwl. Alipoulizwa aendelee kuongoza alijibu nini?

Ukishajibu hayo maswali njoo tuendelee na mada .................

Sasa Polepole na yeye si ana uhuru wake wa kuongea na kutoa maoni? Kwani lazima nifate kile Polepole au Mwenyekiti wanasema?

Nimekueleza, kiongozi bora ni yule anayetafutwa na Watu, sio yule anayetafuta uongozi.

Sisi kama wana Nchi, tunamtaka Mhe. Rais aridhie nngwe ya tatu pindi yutakapofanikisha marekebisho ya katiba
 
Mimi sijaongelea vyama hapa.

Wewe kama ni CCM baki na chama chako. Mimi ni Mtanzania mwenye haki zote za kumshawishi mwananchi yeyote tubadilishe katiba ili Mhe. Rais azidi kutuhudumia

katiba ina mapugufu mengi kuliko hilo la kuongeza muda wa raisi, tupunguze kqanza madaraka ya rais mule na tuweze kumwajibisha akikosea yeye asiwe final say.. mambo ya msingi hamwongelei mnaongelea upumbavu.
 
Yap kabla hajazaliwa , Uraisi ni tasisi kubwa sana na inaheshimika sana.

Hatutaki watu wachache waichafue nchi hii , Nchi ni yetu sote tunawajibu wa kuilinda na kuipigania.

Umeongea ukweli,

Ila Wengi wape. Kwa hili hamna pa Kukimbilia, itawalazimu mkubali tu.

Maana wananchi wengi tunania ya kumshawishi MH Rais
 
Ndio, nitafuata taratibu zote. Na ndio nimeanza sasa kama ifuatavyo
 
Ni uchafu mtupu umeandika humu.Hata kiswahili kinakushinda"Eti Magufuri,Nani mwenye jina hili,ulitaka kuandika jina la Mkiti Wa chama cha cicem au ulitakaje.Jaribu kuandika tena ili ueleweke.

Na kama ulikuwa unamaanisha President of United Repulic Of Tanzania Anaitwa Dr.Magufuli.hayo majina mengine jazia hapo isomeke vizuri.

Na kukusaidia vizuri rudi kwenye vyombo vya habari,kwani inaonekana hata habari husikilizagi bali unakurupuka tu na taarifa na mazungumzo ya kwenye bao,draft na vikao vya kwenye migahawa au kahawa.

Nikujulishe tu kuwa: Yeye Dr.Alishasema,tena sio mara moja au 2 au 3 haikutosha akamtuma polepole (kama unamfahamu) kwamba,hataongeza hata sekunde moja baada ya muda wake kwisha.Sijui wewe unatakaje,mtu ale mataapishi yake mwenyewe? HAIWEZEKANI.

Njoo huku tuungane turekebishe katiba ambayo mpaka sasa ina vipengele vya chama kimoja kimaandishi ila kiuhalisia ni nchi ya vyama vingi.

Kama askofu amekamatwa na jeshi la polisi kwa kuandaa kudai katiba mpya ya nchi kitu ambacho kisheria katiba inaruhusu.Tunajiuliza maswali mengi.Kwa nini yeye akamatwe na polisi na wewe usikamatwe na jeshi hilo hilo kwa kuandika hayo.Ndio maana nimesema katiba inatumika na jeshi la polisi kidouble standard kama sio amri kutoka juu.

Samahani nimeandika nikiwa na hasira mlima.
 
katiba ina mapugufu mengi kuliko hilo la kuongeza muda wa raisi, tupunguze kqanza madaraka ya rais mule na tuweze kumwajibisha akikosea yeye asiwe final say.. mambo ya msingi hamwongelei mnaongelea upumbavu.

Sasa hayo ya msinga ni according to who? Says who? Wewe???

Ok, mimi ninabaki na langu moja, wewe baki na lakk la msingi
 
Sasa Polepole na yeye si ana uhuru wake wa kuongea na kutoa maoni? Kwani lazima nifate kile Polepole au Mwenyekiti wanasema?

Nimekueleza, kiongozi bora ni yule anayetafutwa na Watu, sio yule anayetafuta uongozi.

Sisi kama wana Nchi, tunamtaka Mhe. Rais aridhie nngwe ya tatu pindi yutakapofanikisha marekebisho ya katiba
Hujamaliza kujibu Ok fine tuache maana majibu yake ni jibu tosha katika uzi huu.

Kama nilivyotangulia kusema awali sijawahi kuona katika historia ya uongozi hapa kwetu kwanzia ngazi za chini mpaka juu ulio wahi kutafutwa kwa nguvu kama huu. Sijawahi

Kweli kiongozi bora anatafutwa naomba tufanye kitu kimoja kusanya data free and fair je kweli viongozi wetu hawa wanapendwa na wananchi? Bila kuathiri pande yoyote anza sasa.
 
Sasa wewe ndio umeleta mawazo mgando na yakijinga.

Unajua maana ya uhaini? Au unaropokwa tu kufurahisha nafsi yako?

Jitulize hivyo hivyo dawa iingie.
Mhaini hana nafasi ya kujadiliana naye. JPM kasema hataki kuongeza nyie na njaa zenu mnalazimisha. Mpo sawa na mpuuzi Tundu Lissu nyote wabinafsi. Futa huu upuuzi
 
Ni uchafu mtupu umeandika humu.Hata kiswahili kinakushinda"Eti Magufuri,Nani mwenye jina hili,ulitaka kuandika jina la Mkiti Wa chama cha cicem au ulitakaje.Jaribu kuandika tena ili ueleweke.

Na kama ulikuwa unamaanisha President of United Repulic Of Tanzania Anaitwa Dr.Magufuli.hayo majina mengine jazia hapo isomeke vizuri.

Na kukusaidia vizuri rudi kwenye vyombo vya habari,kwani inaonekana hata habari husikilizagi bali unakurupuka tu na taarifa na mazungumzo ya kwenye bao,draft na vikao vya kwenye migahawa au kahawa.

Nikujulishe tu kuwa: Yeye Dr.Alishasema,tena sio mara moja au 2 au 3 haikutosha akamtuma polepole (kama unamfahamu) kwamba,hataongeza hata sekunde moja baada ya muda wake kwisha.Sijui wewe unatakaje,mtu ale mataapishi yake mwenyewe? HAIWEZEKANI.

Njoo huku tuungane turekebishe katiba ambayo mpaka sasa ina vipengele vya chama kimoja kimaandishi ila kiuhalisia ni nchi ya vyama vingi.

Kama askofu amekamatwa na jeshi la polisi kwa kuandaa kudai katiba mpya ya nchi kitu ambacho kisheria katiba inaruhusu.Tunajiuliza maswali mengi.Kwa nini yeye akamatwe na polisi na wewe usikamatwe na jeshi hilo hilo kwa kuandika hayo.Ndio maana nimesema katiba inatumika na jeshi la polisi kidouble standard kama sio amri kutoka juu.

Samahani nimeandika nikiwa na hasira mlima.
Mkuu tumesha mwambia mapema sana , by the way umetoa point nzuri sana.
 
Kuna sehemu nimevunja Katiba au sheria za nchi?

Please help me
ni kweli haujavunja katiba wala sheria yoyote ya nchi, na hata wale wanaompinga huyo unayetaka aongezewe muda hawajavunja sheria yoyote vilevile...ajabu huyo unayemsujudia anataka kuwatoa roho (mfano kushambuliwa TL) wote wanaompinga na kumkosoa, wewe unaona ni sawa yeye kufanya hayo?!?!.
 
Ni uchafu mtupu umeandika humu.Hata kiswahili kinakushinda"Eti Magufuri,Nani mwenye jina hili,ulitaka kuandika jina la Mkiti Wa chama cha cicem au ulitakaje.Jaribu kuandika tena ili ueleweke.

Na kama ulikuwa unamaanisha President of United Repulic Of Tanzania Anaitwa Dr.Magufuli.hayo majina mengine jazia hapo isomeke vizuri.

Na kukusaidia vizuri rudi kwenye vyombo vya habari,kwani inaonekana hata habari husikilizagi bali unakurupuka tu na taarifa na mazungumzo ya kwenye bao,draft na vikao vya kwenye migahawa au kahawa.

Nikujulishe tu kuwa: Yeye Dr.Alishasema,tena sio mara moja au 2 au 3 haikutosha akamtuma polepole (kama unamfahamu) kwamba,hataongeza hata sekunde moja baada ya muda wake kwisha.Sijui wewe unatakaje,mtu ale mataapishi yake mwenyewe? HAIWEZEKANI.

Njoo huku tuungane turekebishe katiba ambayo mpaka sasa ina vipengele vya chama kimoja kimaandishi ila kiuhalisia ni nchi ya vyama vingi.

Kama askofu amekamatwa na jeshi la polisi kwa kuandaa kudai katiba mpya ya nchi kitu ambacho kisheria katiba inaruhusu.Tunajiuliza maswali mengi.Kwa nini yeye akamatwe na polisi na wewe usikamatwe na jeshi hilo hilo kwa kuandika hayo.Ndio maana nimesema katiba inatumika na jeshi la polisi kidouble standard kama sio amri kutoka juu.

Samahani nimeandika nikiwa na hasira mlima.

Kwa kuwa umeandika kwa hasira, acha nikujibu kwa akili.

Kwanza kuhusu jina sio issue kwangu, kama umekereka pole, jambo la msingi ujumbe umefika.

Pili, nina haki zote za kufanya niliyoyafanya as long as sivunji katiba.

Tatu inaonekana akili zako ni finyu kwani umekosa kabisa uvumilivu wa kisiasa.
Unatamani kusiakia unachokipenda tu.

Hupendi kuambiwa ukweli. Sasa haya ni mawazo yangu binafsi na ninashawishi yawe mawazo ya watanzania wengi

Over
 
Kura za maoni za nini?

Mimi niko mtani kutafuta signatures millioni tano.

Karibu uniunge mkono pia
Hivi kwamba huyu amefanya lipi, ambayo akina Mkapa, Nyerere etc hawakufanya ?! Maghufuli mara kadhaa keishasema haongezi hata dkk moja nyie mmekazana tu.
 
Hujamaliza kujibu Ok fine tuache maana majibu yake ni jibu tosha katika uzi huu.

Kama nilivyotangulia kusema awali sijawahi kuona katika historia ya uongozi hapa kwetu kwanzia ngazi za chini mpaka juu ulio wahi kutafutwa kwa nguvu kama huu. Sijawahi

Kweli kiongozi bora anatafutwa naomba tufanye kitu kimoja kusanya data free and fair je kweli viongozi wetu hawa wanapendwa na wananchi? Bila kuathiri pande yoyote anza sasa.

Sasa katika historia ya nchi yetu kuna kiongozi anapendwa kama Magufuli?

Kaongoza kura kwa 84% what else do you need to prove his approval ratings??

Unataka tutumie takwimu za Chadema au Ccm??

Oooh come on
 
1. Katiba ya Jamuhuri wa muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.
Mimi kama Mtanzania tar.16/02/2020 nilianzisha uzi unaosema " KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFURI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18(UHURU WA MAONI) , ibara ya19( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo jamii forums, bila kuingiliwa na yeyote.Mpaka hapa JamiiForums mmeshavunja kipengele hiki cha katiba kwa kufuta UZI wangu uliokuwa na nia ya kuhamasisha watu wajiunge katika harakati za kumuongezea Mhe. rais Kipindi kingine kwa mujibu wa katiba.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za waTanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli,

3. MODS naowaomba muache mjadala huu uendelee kwani hakuna mahala popote nilipovunja katiba wala sheria ya nchi. Nilichokifanya nikuanzisha mawazo huru katika chombo cha habari huru bila kuathiri matakwa ya kisheria. Ndugu wana jamvi nawaomba muwe na uvumilivu wa kisiasa, muache mihemko isiyo ya lazima, na ninachokifanya mimi sio death penalty kwa watanzania, bali ninatumia haki yangu kikatiba.

4. Naomba nitumie wasaa huu tena kuwakaribisha WATANZANIA wote katika kundi letu la "MAGUFURI TENA 2025" lenye link hii

Group hili liko TELEGRAM, ili kujiunga ni lazima kwanza uwe na APP ya TELEGRAM halafu unaweza kujiunga na kundi letu hili. Linauwezo wa kuwa na wana kikundi mpaka laki mbili, japo kundi litaanza majukumu yaki pindi tutakapofika idadi ya watu 1000.

5. Kama nilivyoeleza hapo juu, lengo la kundi hili sio kuvunja sheria za nchi, ila ni kuhamasishana sisi kwa sisi kama wananchi wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania kubadiri katiba yetu pendwa ili kumpa muda zaidi Rais wetu jemedari wa mapambano, aliyebadirisha kwa haraka sana system za mazoea kuwa system za kizalendo kwenye nchi yetu.

Mhe. Rais Magufuri kafanya mengi, sitasema nini amefanya kwani sote tunayatambua, basi, bila kushurutishwa na yeyote unaombwa kujiunga na kundi letu ili ku support juhudi hizi fuata link hii MAGUFURI TENA 2025.
Kumbuka;
Hakuna posho, wala marupurupu yoyote , hakuna favour yoyote utakayoipata kwa kujiunga na harakati hizi, zaidi ya kuandika historia ya kizalendo kwamba umehusika katika mchakato huu muhimu kwa taifa leo.

KAULI MBIO YETU NI.
"H.E President Magufuri is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuri ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO;
Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe na MODS pamoja na wana Jamvi wote, situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.

Wewe ni mvivu wa kujitegemea.
Watu wa aina yako mmepewa vyeo ambavyo hamstahili.
Mnavumiliwa tu hapo mlipo na ni wazi Magufuli akistaafu mtapigwa chini.
 
Mhaini hana nafasi ya kujadiliana naye. JPM kasema hataki kuongeza nyie na njaa zenu mnalazimisha. Mpo sawa na mpuuzi Tundu Lissu nyote wabinafsi. Futa huu upuuzi

Sasa kama JPM hataki ndio final say? Watakao amua ni wananchi walimpa madaraka.

Sisi tunataka aendelee sasa kuna shida gani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom