Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
5G3TVR.png

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
ni kweli haujavunja katiba wala sheria yoyote ya nchi, na hata wale wanaompinga huyo unayetaka aongezewe muda hawajavunja sheria yoyote vilevile...ajabu huyo unayemsujudia anataka kuwatoa roho (mfano kushambuliwa TL) wote wanaompinga na kumkosoa, wewe unaona ni sawa yeye kufanya hayo?!?!.

Hayo ya kutoa roho ukikamatwa itoe ushahidi unao??

Nashauri ujielekeze kwenye mada usika.

Mambo mengine unaweza kuyaanzisha wewe kwenye thread nyingine
 
Sasa katika historia ya nchi yetu kuna kiongozi anapendwa kama Magufuli?

Kaongoza kura kwa 84% what else do you need to prove his approval ratings??

Unataka tutumie takwimu za Chadema au Ccm??

Oooh come on
Tukisema tuwe fair nadhani unajua kitakachotokea, hizo Approval rating zaka nina mashaka nazo sana.

Ndio maana nikasema kuna mambo huitaji akili kuya ngamua na nimefarijika kuwa kumbe shule umeenda sasa tatizo lako nini?

Tumia elemu yako cheo utapata tu hatakama sio ndani ya CCM, unawezapata Kanisani au Msikitini , mapambio haya huju jamaa mwenyewe hataki.

Naomba vijana tuache praise and worship kwaajili ya kupata uteuzi tufanye kazi.
 
Hao tu waliopewa kuilinda katiba wanaikanyaga Kama hawaioni, NAHISI hili la kutaka kuongezewa muda linatoka huko juu Seema so wananchi tunataarifiwa tu maana si kwa hii mihemko
 
1. Katiba ya Jamuhuri wa muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.
Mimi kama Mtanzania tar.16/02/2020 nilianzisha uzi unaosema " KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFURI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18(UHURU WA MAONI) , ibara ya19( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo jamii forums, bila kuingiliwa na yeyote.Mpaka hapa JamiiForums mmeshavunja kipengele hiki cha katiba kwa kufuta UZI wangu uliokuwa na nia ya kuhamasisha watu wajiunge katika harakati za kumuongezea Mhe. rais Kipindi kingine kwa mujibu wa katiba.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za waTanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli,

3. MODS naowaomba muache mjadala huu uendelee kwani hakuna mahala popote nilipovunja katiba wala sheria ya nchi. Nilichokifanya nikuanzisha mawazo huru katika chombo cha habari huru bila kuathiri matakwa ya kisheria. Ndugu wana jamvi nawaomba muwe na uvumilivu wa kisiasa, muache mihemko isiyo ya lazima, na ninachokifanya mimi sio death penalty kwa watanzania, bali ninatumia haki yangu kikatiba.


4. Naomba nitumie wasaa huu tena kuwakaribisha WATANZANIA wote katika kundi letu la "MAGUFURI TENA 2025" lenye link hii

Group hili liko TELEGRAM, ili kujiunga ni lazima kwanza uwe na APP ya TELEGRAM halafu unaweza kujiunga na kundi letu hili. Linauwezo wa kuwa na wana kikundi mpaka laki mbili, japo kundi litaanza majukumu yaki pindi tutakapofika idadi ya watu 1000.

5. Kama nilivyoeleza hapo juu, lengo la kundi hili sio kuvunja sheria za nchi, ila ni kuhamasishana sisi kwa sisi kama wananchi wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania kubadiri katiba yetu pendwa ili kumpa muda zaidi Rais wetu jemedari wa mapambano, aliyebadirisha kwa haraka sana system za mazoea kuwa system za kizalendo kwenye nchi yetu.

Mhe. Rais Magufuri kafanya mengi, sitasema nini amefanya kwani sote tunayatambua, basi, bila kushurutishwa na yeyote unaombwa kujiunga na kundi letu ili ku support juhudi hizi fuata link hii MAGUFURI TENA 2025.
Kumbuka;
Hakuna posho, wala marupurupu yoyote , hakuna favour yoyote utakayoipata kwa kujiunga na harakati hizi, zaidi ya kuandika historia ya kizalendo kwamba umehusika katika mchakato huu muhimu kwa taifa leo.


KAULI MBIO YETU NI.
"H.E President Magufuri is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuri ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"


MWISHO;
Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe na MODS pamoja na wana Jamvi wote, situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.

Kwani si mumeshaongea naye ndani ya Chama chetu kwamba aendelee milele? Na mkishaamua hakuna wa kusema vyoko. Sasa unakuja kulialia hapa ili tukusaidie nini? Wala hakuna haja ya kuleta mjadala hapa. Ukisema katiba inakupa uhuru wa kutoa maoni yako Mbona wengine wakitumia uhuru huo mnawapoteza? Endeleeni na huyu Shetani wenu hadi mtakapoona mlete shetani mwingine. Hatuna jinsi kwa SISIEM hii. Chochote inachoamua ndio hicho hicho. Hapa mnatusumbua tu.
 
Tukisema tuwe fair nadhani unajua kitakachotokea, hizo Approval rating zaka nina mashaka nazo sana.

Ndio maana nikasema kuna mambo huitaji akili kuya ngamua na nimefarijika kuwa kumbe shule umeenda sasa tatizo lako nini?

Tumia elemu yako cheo utapata tu hatakama sio ndani ya CCM, unawezapata Kanisani au Msikitini , mapambio haya huju jamaa mwenyewe hataki.

Naomba vijana tuache praise and worship kwaajili ya kupata uteuzi tufanye kazi.

Baki kwenye hoja ya msingyi, naona unahama mada.

Hakuna mahala nilipo praise wala ku worship zaidi ya kuongea fact.

Over
 
Hata kama kafanya mengi kubadili katiba eti akae madarakani mda mlefu hapana, akija mwingine akaharibu utabadili katiba tena acha hizo mda wake ukiisha aje mwingine.
 
Acha uzuzu, una ushahidi na unayoyasema??
Umasikini wa fikra na mwili unakusumbua.
Fanya kazi ujitegemee, hicho kibarua ulichopewa ni cha muda tu.
Jenga sasa makwenu, maana Magufuli amekataa kujiongeza muda.
 
Hata kama kafanya mengi kubadili katiba eti akae madarakani mda mlefu hapana, akija mwingine akaharibu utabadili katiba tena acha hizo mda wake ukiisha aje mwingine.

Sawa na wewe ni mawazo yako na ninayaheshimu.

Mimi nina mawazo yangu sio lazima yakubaliwe na kila mmoja, so relax
 
Baki kwenye hoja ya msingyi, naona unahama mada.

Hakuna mahala nilipo praise wala ku worship zaidi ya kuongea fact.

Over
Anapendwa na nani? Ulisikia wapi data hizo ni manipulation tu hakuna Actual data hapo . Unajua Aidan yakuze? Unaijua twaweza? Fuatilia kwanza mikasa na visa hivyo then njoo tuendelee na mada .

Approval rating ya wapi? Aise kuna mada zingine inabidi mtu ukae kimya tu.

Ndio maana kuna raisi mstaafu mmoja ameamua kukaa kimya maana ukimya ni jibu pia .
 
Katika vitu vinavyotupima maturity ni pamoja na kuwa na ustaarabu katika wale watu na vitu usivyokubaliana navyo.
Na ustaarabu hapa ni kutoa hoja na sio kutoa maneno ya kuudhi na matusi
 
Anapendwa na nani? Ulisikia wapi data hizo ni manipulation tu hakuna Actual data hapo . Unajua Aidan yakuze? Unaijua twaweza? Fuatilia kwanza mikasa na visa hivyo then njoo tuendelee na mada .

Approval rating ya wapi? Aise kuna mada zingine inabidi mtu ukae kimya tu.

Ndio maana kuna raisi mstaafu mmoja ameamua kukaa kimya maana ukimya ni jibu pia .

Sasa Iyakuze na Twaweza wameingiaje hapa?

Kama kuna namna nimewagusa samahani, ila tubaki kwenye mada kuu.

Mhe. Rais aongezewe muda kwa kubadili katiba
 
Wapo shida mtu mmoja ID 13, sasa kwa akili ya mleta mada anafikiri kuna watu wengi.

Hapo hapo utakuta yeye mwenyewe mleta mada, anajijibu [emoji23] [emoji1787]

Everyday is Saturday................................😎

Sawa bambushka

Hapa mada ni Mh. Rais aingezewe muda ili akamilishe miradi yote mikubwa aliyoianzisha
 
Ningekuwa MOD mimi hata huu hapa ulioleta ningeufutilia mbali maana ni ujinga mtupu umejaza humo kwenye mimaandishi yako hata kusoma sijasoma mpaka nikamaliza
Mawazo kama haya uliyoandika hapa hayana tofauti na ya baadhi ya viongozi walioko madarakani ambao hawataki kusikia mtu yeyote akitamka neno CORONA.

Acheni watu watoe mawazo yao kwa uhuru!
 
Sawa na wewe ni mawazo yako na ninayaheshimu.

Mimi nina mawazo yangu sio lazima yakubaliwe na kila mmoja, so relax
Nataka kukwambia tu kwa faida yako na watu wengine 9999 unaowatafuta . Watanzania ni watu wa amani sana.

Lakini kile watanzania wameifadhi mioyoni mwao ni kitu kingine kabisa.

Kubadili katiba na kuongeza muda wa uraisi wewe umeona ni maendeleo kwa watanzania[emoji3][emoji3][emoji3] aise upo vizuri ndugu.

Biashara kufungwa kila kukicha , ushuru kuwa mkubwa na vikesikesi vya ajabu ajabu unaona ni maendeleo [emoji3]

Matukio ya ajabu ajabu unayoyasikia na kuyaona yakifanyika unaona ni vizuri [emoji3]

Ok fine endelea kusifu na kuabudu .
 
Mawazo kama haya uliyoandika hapa hayana tofauti na ya baadhi ya viongozi walioko madarakani ambao hawataki kusikia mtu yeyote akitamka neno CORONA.

Acheni watu watoe mawazo yao kwa uhuru!
Tanzania ina vitu vingi sana vya msingi vya kuzungumzia sio upuuzi wa kuongezea muda eti rais atawale milele wakti kuna watu kibao hapa na wanaweza kuongoza vizuri kabisa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom