Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
5G3TVR.png

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
Suluhisho ni nini?

Mfumo imara? Ambao unatengenezwa na nani? CHADEMA???? what do want to say?

Kwamba kwa kuwa ulipitia Bagamoyo kwenda Chalinze basi nikipitia Kibaha Sifiki?

Oooh please, kila nchi ina utaratibu wake, huo mfumo imara na taasisi imara zinawekwa na watu sampuli ya Magufuli.

So relax

confirmed: very likely unatatizo la mahaba kwa mtawala wa sasa.

I rest my case.
 
Ni kweli usiopingika Magufuli amefanya mambo ambayo nashindwa kuficha support yangu kwake,

Na ndio maana nafanya hizi harakati
pole sana. Wengi wenye hili tatizo hujuta sana linapokwisha. Enjoy while it lasts.
 
Wewe kwako Haki ni nini?

Ni CHADEMA kuwa na wabunge wengi bungeni au Lowasa kuhamia CHADEMA.

Kwako haki ni Lipumba kuisaliti CUF au membe kuhama CCM?

Una maana gani unaposema Haki?
Je? Ni kwa Mbowe kuwa Mwenyekiti wa maisha au Halima mdee na wenzake kuwasaliti CHADEMA.

Kwako haki ni nini hasa?
Unazo changamoto nyingi JJB.

Hata "HAKI" hujui maana yake?

Sasa ngoja nikupe mfano mmoja tu kati ya mingi inayoelezea HAKI, pamoja na kwamba najua, kutokana na uliyokwishaandika humu hautakusaidia kujua haki ni nini:

WaTanzania wanapokwenda kupiga kura, maana yake ni kwamba wanatumia 'HAKI' yao ya msingi ya kuwachagua viongozi wanaotaka wawaongoze.
Hawataki mtu au taasisi nyingine yoyote iingilie mchakato na kuharibu haki yao hiyo kwa kuwaweka viongozi ambao wananchi hawakuwachagua.

Sitataka kupoteza muda zaidi nawe juu ya hili.
 
“JJB you have no need for using” like seriously??? Wat do u mean?

Kama unataka tuhamie kwenye kurekebishana Lugha then karibu, rekebisha tenses
"tenses"? zipi tena hapo!

Sawa. Rekebisha.
 
Wenye akili walipogusa katiba YENU kwenye eneo la MUUNDO WA MUUNGANO, MATOKEO YA URAIS KUHOJIWA MAHAKAMANI, TUME HURU YA UCHAGUZI, MAMLAKA YA RAIS KUPUNGUZWA,mlipiga kelele mlikauka makoromeo pale kwenye Bunge la Katiba.
 
Ulitakaje sasa ndiyo kapata 84% official votes.

Mengine ni Porojo tu


ukishachaguliwa asilimia 84 basi unakuwa unafanya upuuzi ? ivi mnakuwaga mnawaza kutumia ubongo huu huu tunaotumia sisi ?
 
Wenye akili walipogusa katiba YENU kwenye eneo la MUUNDO WA MUUNGANO, MATOKEO YA URAIS KUHOJIWA MAHAKAMANI, TUME HURU YA UCHAGUZI, MAMLAKA YA RAIS KUPUNGUZWA,mlipiga kelele mlikauka makoromeo pale kwenye Bunge la Katiba.

Sasa mimi ndiye niliyetoka Bungeni au ni Mwenyekiti wenu na genge lake?

Unamlaimu nani sasa?
 
Unataka “maendeleo” yanayoletwa na mtawala fulani au unataka “maendeleo endelevu”yasiyofungamana na mtawala?

kama ni ya kwanza, basi angalau jifunze kwenye historia ili kuona tatizo lake. Nyerere alitawala kwa miaka 25! na sera ya ujamaa na kujitegemea. Umeona kilichotokea baada ya kuachia ngazi?

kama unataka ya pili, kwa maoni yangu, historia imeonyesha kuwa tunahitaji mipango ya kitaifa sio ilani za vyama + katiba inayowapa wananchi madaraka zaidi (katiba ya warioba ni mwanzo mzuri) na sio hii ya kifalme.
Huu ukweli hawa wachumia tumbo wa ccm hawawezi kuuona
 
Sasa mimi ndiye niliyetoka Bungeni au ni Mwenyekiti wenu na genge lake?

Unamlaimu nani sasa?
Mkuu hivi waliotoka walikuwa wangapi na waliobaki walikuwa wangapi? Je baada ya wale wengine kutoka,wale waliobaki walibaki wanafanya nini?
 
Hapana !



Kwa sasa sisi wananchi tunamiin Magufuli miaka 5 tu inatosha acha ushabiki.
 
Na watanzania ndio sisi;

Kwani kuna ubaya gani? Sisi 84% tuliompigia kura ndio tunataka aendelee kuongoza nchi.

Kama wewe hautaki ni haki yako pia
Kura 85% apate wapi? Zile zilichapishwa na Jamana Printers kisha vijana wa TISS wakatick. Baada ya hapo DSOs wa kila wilaya wakagawiwa. Uchaguzi wa 2020 katika historia ya Tanzania utafutwa ili vizazi vijavyo visitumie takwimu FAKE. Hakuna kura iliyohesabiwa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom