Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
5G3TVR.png

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
Alieshinda kura za maoni Kawe alikatwa akapewa mtu ambae sio chaguo la wanachi

Alieshinda kura za maoni Vunjo hakupitishwa bali akapewa mtu ambae sio chaguo la wanachi....
Hapo utashangaa mchakato wa kubadili kipengele cha madaraka ya uraisi kitakavyofanyoka kwa wepisi tena bila gharama.

Ila kubadili katiba yote kupata katiba mpya hapo tutazunguahana mpaka wajukuu watazeeka.

Maajabu haya.
 
Unataka kumlazimisha mtu ambaye kashasema hataki kuwa rais baada ya 2025?

Unaelewa kwamba hiyo katiba unayoishadadia ina term limits?

Kwani hata Urais wa awamu ya kwanza si alisema alikua anajaribisha tu??

Halafu wananchi wakamchagua kwa kimbunga.

Hivi wewe unaweza kuona asali halafu ukaogopa nyuki kuilina hiyo asali?

Rais Magufuli ni Asali na nyie wapinzani ndio nyuki, tutawaelimisha mpaka mjue utamu wa asali.

Hatuwezi kukubali
 
Alieshinda kura za maoni Kawe alikatwa akapewa mtu ambae sio chaguo la wanachi...

Sasa usilazimishe nifanye matakwa yako, yani haiwezekani.

Kama unataka katiba ya warioba, anzisha wewe huo mchakato.

Mimi niko hapa hapa na sihami.

Over
 
Alieshinda kura za maoni Kawe alikatwa akapewa mtu ambae sio chaguo la wanachi

Alieshinda kura za maoni Vunjo hakupitishwa bali akapewa mtu ambae sio chaguo la wanachi

Hao wote walipitishwa ili waende kuunga juhudi za kubadilisha katiba.

Kuna siku aliwahi kusema hajawahi kuhubiri katiba mpya wala kwenye kampeni zake hajawahi kusema chochote kuhusu katiba mpya, nyie mnaetaka kipengele cha katiba kibadilishwe kisa matamanio ya wahuni wachache ni bora mrudishe rasimu ya katiba ya warioba ibadilishwe katiba yote na sio kipengele kimoja
Umenisoma mkuu wangu 'Complex31'?

Naomba unisome tena kabla hujanibugiza haya uliyoniachia hapa.

Ikikupendeza roho, rekebisha maanake sistahili kutwishwa lawama uliyonitwisha mimi.
nyie mnaetaka kipengele cha katiba kibadilishwe kisa matamanio ya wahuni wachache ni bora mrudishe rasimu ya katiba ya warioba ibadilishwe katiba yote na sio kipengele kimoja
Maandishi yangu uliyoyajibu hayahusiki kabisa na haya maneno uliyoweka hapa.
 
Mwandishi ni kama ni mtu aliyefanya machafu sana awamu hii hivyo anataka aendelee kuwa madarakani ili awe kinga kwake!
 
Kwani hata Urais wa awamu ya kwanza si alisema alikua anajaribisha tu??

Halafu wananchi wakamchagua kwa kimbunga.

Hivi wewe unaweza kuona asali halafu ukaogopa nyuki kuilina hiyo asali?

Rais Magufuli ni Asali na nyie wapinzani ndio nyuki, tutawaelimisha mpaka mjue utamu wa asali.

Hatuwezi kukubali
Unaji contradict.

Unataka kutumia haki yako ya kikatiba lakini hutaki kufanya wajibu wako wa kufuata katiba.

Unajua hata unataka nini?
 
Taratibu naanza kukuelewa wewe ni mtu wa aina gani kutokana na bandiko hili hapa.

Ninakubaliana kabisa na jibu lako katika mstari wa kwanza.

Kama hujawahi kumsoma mkuu 'Kiranga' kuhusu msimamo wake kuhusu hili; nadhani hapa umejaribu kumpa kipande cha "ushuhuda" juu ya msimamo wake huo.

Katika hili tu, ndilo ninalokubaliana nawe; siyo hayo mengine
 
Unaji contradict.

Unataka kutumia haki yako ya kikatiba lakini hutaki kufanya wajibu wako wa kufuata katiba.

Unajua hata unataka nini?

Katiba sio Msaafu wala sio Bibilia. Katiba haijaandikwa na Malaika, imeandikwa na wanadamu kwa hiyo itabadilishwa na wanadamu kwa muda muafaka
 
Katiba sio Msaafu wala sio Bibilia. Katiba haijaandikwa na Malaika, imeandikwa na wanadamu kwa hiyo itabadilishwa na wanadamu kwa muda muafaka
Sasa kama katiba siyo msahafu mbona unaishadadia haki yako ya kikatiba?

Si ungetaja kitu kingine tu, si katiba, kwa sababu katiba si msahafu.

Unaelewa ukishasema katiba si msahafu unanipa mimi haki ya kusema hiyo haki yako ya kikatiba unayoishadadia ni batili, kwa sababu katiba si msahafu?

Unanipa mimi haki ya kusema haki hiyo ya kikatiba ni ya watu wenye mawazo mapana tu, guluguja kama wewe hustahili haki hiyo?

You are contradicting yourself.
 
Taratibu naanza kukuelewa wewe ni mtu wa aina gani kutokana na bandiko hili hapa.

Ninakubaliana kabisa na jibu lako katika mstari wa kwanza.

Kama hujawahi kumsoma mkuu 'Kiranga' kuhusu msimamo wake kuhusu hili; nadhani hapa umejaribu kumpa kipande cha "ushuhuda" juu ya msimamo wake huo.

Katika hili tu, ndilo ninalokubaliana nawe; siyo hayo mengine
[emoji3][emoji3]
 
Sasa kama katiba siyo msahafu mbona unaishadadia haki yako ya kikatiba?

Si ungetaja kitu kingine tu, si katiba, kwa sababu katiba si msahafu.

You are contradicting yourself.

Do you even know the meaning of “contradicting” or you just insensible in your justifications?

Nimesemema Katiba sio Bibilia kwa sababu inaweza kubadilika, sijasema Katiba inahitaji kuwa kama Bibilia ili niifuate, nitafata kila kilicho kwenye katiba mpaka pale itakapobadilishwa.

As far as am concerned, hakuna ibala yoyote ya Katiba yetu, au sheria zozote za nchi hii, zinazonizuia kujadili na kuhamasisha mchakato wa Kubadili Katiba ili kumpa Rais wetu nyongeza ya Muda, kama kipo please quate for me hapa.
 
Na watanzania ndio sisi;

Kwani kuna ubaya gani? Sisi 84% tuliompigia kura ndio tunataka aendelee kuongoza nchi.

Kama wewe hautaki ni haki yako pia
Akili matope kwa lipi alilofanya la maana
 
Taratibu naanza kukuelewa wewe ni mtu wa aina gani kutokana na bandiko hili hapa.

Ninakubaliana kabisa na jibu lako katika mstari wa kwanza.

Kama hujawahi kumsoma mkuu 'Kiranga' kuhusu msimamo wake kuhusu hili; nadhani hapa umejaribu kumpa kipande cha "ushuhuda" juu ya msimamo wake huo.

Katika hili tu, ndilo ninalokubaliana nawe; siyo hayo mengine
Nina allergy na contradiction.

Mtu anakwambia anapenda sana kutumia haki zake za kikatiba, wakati hajui au hataki kukubali katiba hiyo hiyo anayotaka kutumia haki zake ina vipengele vya term limits.

Ukimwambia katiba ina term limits, anakwambia katiba si msahafu.

Sasa, alipokuwa anapiga kelele kuhusu haki zake za kikatiba, alikuwa hajui katiba si msahafu?

Hapo ndipo utajua njia ya muongo fupi.

Huyu hajali katiba, anajali "cult of personality".

Angesema hilo tangu mwanzo tungemuelewa tu.
 
Nchi sio mtu aliondoka Nyerere na atujayumba tunasonga.Mda wako ukipita umepita nchi haiwezi simama kwa kuondoka kwa mtu mmoja.
Toka lini daladala imewahi kosa abiria
 
Usinipangie cha kuongea. Wewe ongelea Ilani mimi nitaongelea katiba.

Kwani kila linalofanyika lazima liwe kwenye ilani?

Hapa issue ni Katiba ibadirishwe kwa kufuata process zote na sheria za nchi
Haya ni mawazo ya mlala bure kula kulala kwa shemeji, jitegemee uwe na akili
 
Nipe mfano wa taasisi imara
Taasisi imara duniani hazitegemei watu kama tanzaniaj inavyomtegemea kichaa wake.
Mfano israel kuna maandamano ya muda mrefu kwa sababu PM amenunua nyumba kwa kinachodaiwa rushwa.
MAGUFULI alinunua nyumba za NIC akiwa wazir ulishawahi sikia zikitajwa popote?
Aliwauzia nyumba za umma mahawala zake kina kajala wa kebys ambao hawakuwa watumishi ulishawahi kusikia akitaja popote?
Yeye alighiribu WAKULIMA wa KOROSHO huko kusini aliadhibiwa na mamlaka yyte?
Anatapanya peas za umma bila hata kulishirikisha bunge hapo kuna taasisi au kuna mtu?
Soma vizuri uelewa maana ya separation of power checks and balance. Ukikuta hayo matawi yanaingiliana hapo hakuna taasisi imara.
WALAANIWE WAMTEGEMEAO BINAADAM
 
Do you even know the meaning of “contradicting” or you just insensible in your justifications?

Nimesemema Katiba sio Bibilia kwa sababu inaweza kubadilika, sijasema Katiba inahitaji kuwa kama Bibilia ili niifuate, nitafata kila kilicho kwenye katiba mpaka pale itakapobadilishwa.

As far as am concerned, hakuna ibala yoyote ya Katiba yetu, au sheria zozote za nchi hii, zinazonizuia kujadili na kuhamasisha mchakato wa Kubadili Katiba ili kumpa Rais wetu nyongeza ya Muda, kama kipo please quate for me hapa.
"Or you just insensible"?

Wewe jifunze hiyo lugha kabla ya kujianika utupu wako.

Idiot.
 
Na watanzania ndio sisi;

Kwani kuna ubaya gani? Sisi 84% tuliompigia kura ndio tunataka aendelee kuongoza nchi.

Kama wewe hautaki ni haki yako pia
Ok magufuli kaongeza..je ao maraisi wengine watakao kuja unazani awatatak kuongeza nao afu ukute ni wala rusha. Fikiria future ya taifa mkuu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom