tubuwaziri
New Member
- Aug 20, 2021
- 2
- 0
HAKI ZA BINAADAMU.
Haki za binaadamu zinajumuisha mahitaji yote ya muhimu/stahiki za kila binaadamu pamoja na sheria maalumu za kumlinda na kumpa muongozo binaadamu yeyote katika utekelezaji wa maamuzi kulingana na mazingira au utaratibu wa maisha.
Baada ya kuona umuhimu wa kila binaadamu ipo haja ya kupendekeza mikakati ifuatayo maalumu ya mgawanyo wa stahiki/mahitaji/miongozo inayoendana na sheria kutoa utaratibu elekezi pamoja na kumlinda kila binaadamu katika utekelezaji wa majukumu kulingana na mtindo wa maisha yao.
Haki ya kufanya maamuzi na uwajibikaji kulingana na jinsia.
Kwa miaka mingi imekua ikiaminika kuwa mamlaka ya kutoa maamuzi yanayohusu familia na jamii nyingi za kiafrika hutoa kipaumbele kikubwa kwa mwanaume anayetafsiriwa kuwa kichwa cha familia na usukani katika taratibu/shughuli nyingi za maendeleo ya jamii hali hiyo ikiwaacha baadhi ya wanawake ambao mchango wa mawazo/ maamuzi yao vingechochea maendeleo ya jamii/familia husika kwa kiasi kikubwa.
Kutokana na utaratibu huo unao onesha kukiuka haki za binaadamu imeonekana haja ya mamlaka husika ya haki za binaadamu kuanzisha sheria itakayompa kila mmoja nafasi ya ushiriki wa mawazo na maamuzi ndani ya jamii na familia bila kujali jinsia sambamba na kupanua wigo wa uwajibikaji katika shughuli zozote zinazochangia maendeleo ya jamii na familia.
Haki za kudumisha&kuheshimu tamaduni na desturi.
Muendelezo wa tamadani haswa zinazohusu ukabila/mila kwa miaka tunayoishi umeonekana kupoteza nguvu na uhalisia ukifananisha na miaka iliyopita haya yote yakichangiwa na macho ya jamii nyingi tunazoishi leo na mitazamo tofauti inayotokana na matumizi ya tamaduni tofauti ( ngoma za asili, mavazi na shughuli nyingi za kimila) hali hiyo ikiilazimu mamlaka husika ya haki za binaadamu kuonesha ushirikiano mkubwa katika ushiriki wa shughuli hizo na matumizi ya mavazi au lugha zinazoendana utamaduni fulani kuibua ushawishi kwa jamii na koo nyingi kuzoea taratibu hizo na kwa kiasi fulani kuondoa woga wa matumizi ya tamaduni zao baada ya hofu ya kupingwa/kutoungwa mkono kuenea kwa kiasi kikubwa.
Haki ya umiliki na uwajibikaji.
Katika moja ya harakati zinazo changia ukuaji wa uchumi na pato la taifa kwa njia ya ukusanyaji kodi ni mfumo wa vijana wengi sasa kujitengezea kipato kwa umiliki na uwajibikaji katika miradi binafsi ( biashara, taasisi za maendeleo nk).
Kwa kuadhimia kuendeleza mfumo huo serikali kwa kushirikiana na mamlaka husika ya haki za binaadamu inategemewa kuanzisha mifumo ya kisheria kuwalinda na kuwapa muongozo wamiliki wa miradi au taasisi mbalimbali namna wanavyotakiwa kuwajibika kulingana na sheria elekezi katika kukuza na kuendeleza miradi/biashara zao husika.
Mikakati tajwa ( hapo juu) ni kati ya taratibu chache zinazohusisha haki/stahiki za kila binaadamu zinazo aminika kuleta maendeleo na mabadiliko chanya katika mifumo na utaratibu wa maisha ya watu wengi kulingana na utekelezwaji wake unao husisha mamlaka ya haki za binaadamu.
Vilevile kutokana na mitazamo tofauti iliyojengeka na kuaminika ndani ya jamii nyingi juu ya binaadamu wenye utofauti wa kimaumbile ( walemavu ) kuwa kandamizi na inayowatenga watu wa namna hiyo serikali kwa ushirikiano na mamlaka ya haki za binaadamu inatakiwa kurasimisha mifumo/sheria zifuatazo kudhihirisha/kuikumbusha jamii yote umuhimu wa walemavu wa aina yoyote katika jamii nyingi kupitia njia hizo zitakazo walinda, kuwaongoza na kuwaongezea wigo mkubwa katika ushiriki wa majukumu yao kijamii na kitaifa.
Haki ya kuungwa mkono.
Katika kipindi cha miaka michache iliyopita baadhi ya makundi ya watu wenye ulemavu wa aina tofauti tofauti wamevunja imani ya kuwa hawawezi kufanya chochote baada ya wengi wao kujikita katika miradi ya biashara mbalimbali na sanaa zinazohusisha muziki, maigizo, uchoraji, uchongaji nk.kama njia kuu za kujiingizia kipato kinachotegemewa kuendesha maisha ya wengi wao.
Kutokana na mitazamo hasi ya jamii kwa watu wa aina hiyo serikali na mamlaka husika ya haki za binaadamu inategemewa kurasimisha utaratibu wa kuunga mkono juhudi zao ikiwa ni pamoja na kuanzisha makongamano ya maonesho ya kibiashara na sanaa kutoka kwa watu hao kama sehemu ya kuitikia na kuthamini harakati zao.
Haki za ushiriki.
Kwa tathmini iliyo wazi ndani ya kipindi kirefu asilimia chache ya watu wengi wenye utofauti wa kimaumbile ya aina yoyote wameonekana katika ushiriki wa matukio mengi ( kisiasa,michezo nk) wakati asilimia kubwa ya wengi wao wakibaki nyuma kutokana na woga wa mitazamo iliyojijenga ndani ya watu wengi juu yao kuwa viumbe dhaifu katika ushiriki wa aina yoyote hali hiyo ikiilazimisha na kuitaka serikali kwa kushirikiana na mamlaka ya usimamizi wa haki za binaadamu kuibua utaratibu unaotoa kipaumbele kwa watu wa namna hiyo kujihusisha katika ushiriki wa nyanja tofauti tofauti kupitia mikakati ya vyombo vya habari na midaharo ya mara kwa mara kurudisha uwezo wa kujiamini kwa watu hao waliokwisha poteza uwezo wa kujiamini na kujithamini kutokana mitazamo ya jamii wanazoishi.
Katika kuhakikisha ukomavu na muendelezo wa mikakati tajwa ya kisheria serikali kwa ushirikiano mkubwa na mamlaka ya usimamizi wa haki za binaadamu pamoja na jamii husika vinategemewa kuanzisha mikakati ya kufanikisha hili ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa kampeni ndani ya jamii zitakazo saidia kupaza sauti kwa niaba ya binaadamu yeyote anaye kuwa treated kinyume na sheria elekezi pamoja na mijadala ya mara kwa mara ya serikali inayoelezea makundi mbalimbali ya binaadamu kulingana na stahiki zao na sheria kali za utekelezwaji wa baadhi ya mikakati/sheria hizo.
UTAWALA BORA.
Utawala bora unatafsiriwa kwa mifumo huru na stahiki ya uongozi inayoendana na demokrasia pamoja na uadilifu wa viongozi wa ngazi zote katika utekelezaji wa majukumu yao kijamii na kitaifa vyote hivyo vikiunganishwa na utaratibu wa haki na ulio wazi katika uteuzi na uchaguzi wa viongozi wa ngazi zote kuufanya utawala wowote kuwa bora na wa kidemokrasia.
Ndani ya kipindi cha muda uliotengwa wa uongozi wa aina yoyote katika nchi, sehemu au vitongoji husika mifumo ifuatayo ya uongozi ni baadhi ya viashiria vichache vya utawala wa eneo hilo kuwa bora na unaofuata/kuheshimu misingi ya demokrasia.
Uhuru wa kujieleza.
Kwa kipindi kirefu imeaminika na kuonekana kuwa haja ya wananchi wengi kutaka kuwasilisha hoja/malalamiko yao huleta vurugu na machafuko yasiyotarajika hii yote ikitokana na kukosekana kwa utaratibu wa kisheria unaomlinda mwanachi kuwasilisha hoja/malalamiko yake
Kwa kuhakikisha utawala husika unakuwa bora, huru na wa kidemokrasia vyombo husika vinavyoamua / kuendesha masuala ya kisiasa vinategemewa kurasimisha sheria zitakazompa mwananchi yeyote uhuru wa kujieleza kuhusiana na kero/ malalamiko yake kufuatana na utaratibu sahihi.
Umoja na ushirikiano wa vyama vya siasa.
Kwa miaka mingi iliyopita nchi nyingi za Afrika zimeathiriwa na migogoro ya kisiasa haswa ikichangiwa na mgawanyo unaoletwa na wakuu wa vyama fulani wanao azimia kujiongezea wafuasi wa vyama vyao kwa njia isiyo na amani hali hiyo kwa baadae ikififiza ushirikiano katika uendelezaji wa miradi na ushiriki wa kampeni/mikutano ya kimaendeleo kwa ukubwa.
Hivyo kuendana na tafsiri ya utawala bora serikali kwa kushirikiana na wakuu wa vyama vya siasa vyote inategemewa sana kuweka mazungumzo ya wazi mara kwa mara kama njia ya kudumisha ushirikiano na kuondoa fikra za visasi kwa wafuasi wao kulifanya taifa husika kuwa kitu kimoja bila kujali utofauti wa vyama vya siasa.
Kwa kuyaona hayo na kuyaangazia madhara makubwa yanayotegemewa kutokea kutokana na kuwa na utawala usio wa haki usiofuata misingi ya kidemokrasia ni muda wa serikali zote za nchi husika kurasimisha mikakati endelevu ifuatayo itakayokwenda sawa na sheria zilizo wazi kuhakikisha uimara wa misingi/mikakati hiyo elekezi ya utawala.
Utaratibu sahihi wa kupendekeza viongozi wa ngazi zote.
Taifa au jamii yoyote yenye maadhimio makubwa kisiasa katika kukuza na kuendeleza misingi ya uchumi, afya na mazingira linatambua umuhimu wa kuteua viongozi wa ngazi yoyote kwa kuzingatia utayari, uadilifu na utashi wa hali ya juu katika kutoa maamuzi yenye matokeo chanya kwa taifa au sehemu husika kwa kiongozi yeyote mtarajiwa bila kujali ukubwa/ukongwe wa chama chake cha siasa kwa ushirikiano na tume ya uchaguzi.
Mikakati/utaratibu huo vikiaminika kuongeza umakini katika mifumo ya uteuzi wa viongozi wanao endana na utaratibu elekezi katika kulifikisha taifa katika matarajio yake.
Umuhimu wa elimu katika nafasi za uongozi.
Kwa miaka michache iliyopita limeibuka wimbi la uteuzi wa viongozi wa ngazi tofauti tofauti baadhi yao wakionekana kutokua na elimu inayowatosheleza kusimama kama viongozi wa sehemu husika,
Haimaanishi kuwa ufinyu wa elimu ya darasani humkosesha nafasi mtu yeyote kuwania uongozi fulani lakini umeonekana umuhimu mkubwa wa kuwa na elimu kwa viongozi wengi kwa taifa lenye kiu/matarajio ya mafanikio makubwa katika sekta mama ~Biashara,Uchumi na Afya ikiaminika kuwa kiongozi yeyote asiefahamu japo kwa uchache kuhusu uchumi kipaumbele chake kikubwa hakita husisha mikakati yoyote kulifikisha taifa katika uchumi wanao tamani hivyo hivyo kwa afya, elimu na biashara.
Kwa kushirikiana na mamlaka inayosimamia uchaguzi mkuu wa taifa lolote kuna haja ya serikali kuipa elimu kipaumbele katika uteuzi wa viongozi wa ngazi zote ikiaminika kuwa kwa taifa lolote lenye maadhimio makubwa katika uchumi,sayansi na teknolojia linahitaji kiongozi atakae toa kipaumbele kikubwa katika kufanikisha ukomavu wa mifumo hiyo inayo changia sehemu kubwa ya pato la taifa.

Upvote
1