Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Serikali ya Marekani hivi karibuni imetangaza mpango mpya wa ushuru dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi za nje. Kulingana na mpango huo, viwango vya ushuru vinaanzia asilimia 10 hadi 12.5, na kuhusisha karibu washirika wakuu wake wote wa kibiashara, ikiwa ni pamoja na China, Umoja wa Ulaya, Japani, Korea Kusini, Uswisi, Canada, Mexico, India, Indonesia, na Uingereza, huku baadhi ya nchi zikikabiliwa na ushuru wa ziada wa asilimia 10 licha ya ushuru uliopo.
Serikali ya Marekani inadai kwamba hatua hii inatokana na uchunguzi wa “wafanyakazi wa kulazimishwa” ulioanzishwa kufuatia Kifungu cha 301 cha Sheria ya Biashara ya mwaka 1974 ya nchi hiyo, ikisema hatua zilizopo zimeshindwa kuzuia kwa ufanisi bidhaa husika kuingia kwenye minyororo ya usambazaji nchini Marekani. Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Jamieson Greer amedai kwamba ushuru mpya “utasahihisha ukiukwaji wa haki za binadamu na vitendo vya upotoshaji wa biashara”.
Hata hivyo, hatua inayolenga masuala maalum ya haki za binadamu hatimaye imebadilika na kuwa seti ya ushuru mpana unaofunika nchi nyingi na bidhaa zote. Ni wazi kwamba sera hiyo hailingani na mantiki yake iliyotajwa. Lengo lake halisi ni kuhudumia sera ya rais wa nchi hiyo Donald Trump ya “Marekani Kwanza”, kutumia ushuru kulazimisha makubaliano ya washirika wa biashara, kuchochea uundaji upya wa viwanda, kurekebisha minyororo ya usambazaji ya kimataifa, na kuhamisha shinikizo la kiuchumi na kisiasa la ndani kwa nchi nyingine.
Ikilinganishwa na hasira kubwa iliyosababishwa na ushuru wa “Siku ya Ukombozi” wa mwaka jana, mara hii mwitikio kutoka nchi mbalimbali umekuwa mtulivu sana. Hii si kutojali, bali ni kupuuza, kwani nchi hizo zimezoea ushuru wa juu wa Marekani na mabadiliko yake ya mara kwa mara. Badala ya kujihusisha na vita na adui asiye na msimamo thabiti, ni bora kutafuta njia mbadala, ikiwa ni pamoja na kuharakisha utekelezaji wa RCEP, kuimarisha ushirikiano na nchi zinazoaminika, na kuendeleza mazungumzo ya biashara huria ya pande mbili.
Kwa China, duru hii mpya ya ushuru si ya kushangaza wala ya kutisha. China ina mnyororo kamili wa viwanda, soko kubwa mno la ndani, na ushirikiano wa uchumi na biashara na nchi nyingine duniani. Suluhisho halisi si kufuata vitendo vya Marekani, bali ni kuzingatia kujiendeleza yenyewe: kuharakisha kujitegemea kiteknolojia, kufungua mlango zaidi, na kuimarisha pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.
Kuanzia Sheria ya Dharura ya Kimataifa ya Mamlaka ya Kiuchumi, hadi Kifungu cha 122 cha Sheria ya Biashara ya mwaka 1974, na sasa Kifungu cha 301, msingi wa kisheria wa ushuru wa Marekani umebadilika mara kwa mara. Kwa bahati mbaya, baada ya miaka kadhaa, Marekani bado haielewi kwamba ushuru usio na sababu hauwezi kutatua mgogoro wake wa kifedha au kuokoa tasnia yake ya utengenezaji, bali utaharibu tu sifa yake na kuleta machafuko kwa biashara ya kimataifa.