HakiElimu vs Govt: The saga

Ndiyo shida iyo...mwalimu form four failure eti anawatayarisha wanafunzi wanaotegemea kuja kuliinua taifa hili maskini... hii ni akili ya abunuwasi
 
Mbavu huwa zinaniuma kwa kumkumbuka mwalimu wangu wa Chemistry A-Level, kwani siku moja aliingia darasana na kuuliza DID YOU DONE YOUR WORK?

Kuhusu suala la kiswahili kutumika Tanzania kama lugha ya kielimu hilo bado ni kitendawili na wala halitatufikisha mbali.
Shida niliyoiona mimi kwa kiingereza kuwa kigumu kwa sisi watanzania ni kutoaka na mazingira yanayowazunguka wanafunzi. Kwani ni muda mfupi ambao wanakuwa mashuleni na maara nyingi wanakuwa na katika jamii ambapo kiingereza ni venecular language, not sure kama nime-spell vizuri. Kwa hiyo utakuta wale wenye kipata kizuri na waliowapeleka watoto wao kwenye english media wanapaform vizuri kiingereza na hasa katika kuzungumza. Lakini ieleweke wazi kuwa kufahamu kiingereza si kufaulu masomo. Nina mfano ulio wazi kwa zangu wawili mmoja nilisoma naye shule moja na mwingine alisomea shule nyingine. Nikianza na huyu niliyesoma naye ni kwamba alikuwa na uweza mkubwa sana wa kuongea kiingereza tena ile slang. Na nilikuwa na-admire the way alivyokuwa akiongea kwa kimarekani na kwa kupatia hasa (mimi anayeongea sawa namjua ila mimi mwenyewe nahitaji kukosolewa). Ilipokuja kwenye mitihani yenyewe ni kwamba jamaa alipiga F (mkingule) hadi kwenye english subject huku sisi wa viingereza vya kuunga na super-glue tukiibuka na msonge.
na hata yule jamaa mwingine wa pili aliambulia D.

Kwa hiyo sidhani kama kiingereza ni kipimo cha IQ ya mtu isipokuwa ni vema kukifahamu kwa ajili ya mawasiliano.

Hot globali woming!!!
 
Sina hakika kama umesoma kilichoeleza hapo juu kwenye "Kiswahili, Norwegian or English as a Language of instruction?"
Kama hujafanya hivyo, isome tafadhali. Mimi baada ya kuisoma niko mguu mmoja nje mwingine ndani. Imenifungua macho sana hata hivyo, na nadhani watu wa Linguistic ndio wanaoweza kutupa mwongozo katika hili na sio wanasiasa.

Nakubaliana nawe kwamba kweli kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia bado ni kitendawili and again watu wa linguistic kwa hakika watakuwa na majibu kwa nini Tanzania tumepata kigugumizi kwenye hili. Kwamba hatutafika mbali kwa kufanya hivyo, hapo nasita kukubaliana na wewe.

.
 
Haika,

Mi nadhani bado jamii haijatulia na kuamua ni lugha gani hasa yaweza kutumika kufundishia na ndio maana si ajabu kukuta hata mwalimu nae hayo mayai yanampiga chenga.

Niliwahi kusikia kuwa watu wanapendekeza hata katika level ya University na high learning institutions wafundishe kwa kiswahili lakini yawezekana ugumu wanaokutana nao wanatulia wenyewe..But kwa mtazamo wangu ni kuwa hakuna maandalizi na nia thabiti ya kutumia kiswahili badala yake tunalazimisha kiingereza kilichopinda kama si kiswanglish...

Nchi kama china,urusi,japan na nyinginezo (mliosoma huko mtanisaidia) nina imani lugha inayotumika kufundishia kuanzia ngazi za chini za elimu hadi vyouni ni hizo lugha zao na wana maendeleo makubwa kuliko hata sisi tunaolazimisha lugha ya watawala wetu. Matokeo yake ndio hizo aibu...Lakini ni tangazo lenye ujumbe mzuri kwa wahusika..
 
Serikali yaionya Hakielimu
Halima Mlacha
Daily News; Wednesday,October 22, 2008 @20:19

Serikali imeionya Taasisi ya HakiElimu kuacha kutumia matangazo yake katika vyombo vya habari, kueneza chuki miongoni mwa watoto na vijana nchini na badala yake ingetumia nafasi iliyonayo katika kuwafundisha utawala bora.

Aidha, imewatahadharisha wote wanaoanzisha taasisi za elimu kwa minajili ya kupata fedha bila kuchangia lolote katika sekta ya elimu, ikiwa ni pamoja na shule zinazotoza wazazi fedha nyingi ambazo hazilingani na mazingira na kiwango cha elimu kinachotolewa.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii katika ofisi za Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Lucy Nkya, alisema HakiElimu pamoja na kuonywa na kusimamishwa hivi karibuni kutokana na utendaji wake, bado imeendelea kutoa matangazo ambayo yanaeneza chuki kwa vijana.

“Hili tangazo tena linalorushwa hata televisheni ya TBC1 la watoto wa sekondari wanazungumzia EPA, wanafanyiwa hesabu na kisha wanaambiwa waseme hizi hela zingefanyia hili na lile, kumbukeni samaki mkunje angali mbichi, huku ni kueneza chuki kwa watoto hawa,” alisema Dk. Nkya.

Alisema taasisi hiyo ya HakiElimu inakosea kutumia matangazo hayo kwa upande mmoja tu wa kukosoa. “Mimi nimesomea saikolojia, huu mtindo wa kukosoa serikali kwa namna hii, kunawajengea vijana wetu chuki, badala ya kuwafundisha utawala bora, sasa watoto wanafikiri serikali yote ni mafisadi,” alisema.

Alisema kutokana na matangazo na vitendo hivyo kwa sasa, hata watoto wa baadhi ya viongozi wamelazimika kuhamishwa katika shule za kawaida na kupelekwa shule nyingine kwa vile wanaitwa watoto wa mafisadi na wenzao.

Aliitaka taasisi ya TEN/MET kufikisha ujumbe kwa HakiElimu kuwa wanayo nafasi nzuri kuelimisha jamii juu ya masuala ya sekta ya elimu na si kueneza chuki pekee, kwani serikali itafika mahala italazimika kutumia meno yake.

“Msiisingizie serikali haina demokrasia pindi itakapotumia meno yake, haitokuwa kibogoyo tena,” alionya. Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, alitaka kufahamu uwezo wa kiutendaji wa mtandao huo wa elimu kwa kuwa haujitangazi, kwani pamoja na yeye kuwa Waziri wa Elimu ndio anausikia.

Kwa upande wake, Mratibu wa TEN/MET, Joseph Kisanji, alikiri kuwa mtandao huo umejificha na kwamba wanajitahidi kwa sasa kuutangaza kwa kutumia mtindo wao bila kuiga HakiElimu.

Alisema awali wakati HakiElimu ilipokabiliwa na serikali, takribani asasi nyingi za elimu ziliwatetea ukiwamo mtandao huo. “Hata hivyo, kuna mipaka yake katika kutumia media (vyombo vya habari) kwani zina nguvu na tuliwaambia wenzetu juu ya hilo ila hatuna maamuzi, kazi yetu ni kushauri,” alisema.

Alisema kama suala la tangazo la EPA limeleta athari hadi kufikia watoto wa viongozi kuhamishwa shule ni jambo hatari, hivyo aliahidi kulifikisha katika Bodi ya Mtandao huo ili walijadili na kulifikisha kwa taasisi hiyo ya HakiElimu.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TEN/MET, Antoine Gizenga, alisema watalivalia njuga suala la HakiElimu kwani mtandao wao unaitazama taasisi hiyo kama asasi inayosaidia kuibua yaliyojificha.

Mwaka jana, Ofisi ya Waziri Mkuu ilipiga marufuku machapisho na matangazo yanayotolewa na HakiElimu kupitia vyombo vya habari na kutishia kulichukulia hatua kali za kisheria iwapo itakiuka amri hiyo.
 
Tate naneeeee.. huyu mama si Dokta? au ana udaktari wa kuzuga? sasa leo hii wanafunzi wa uchumi duniani wanatumia hali ya uchumi kama mfano halisi wa masomo yao, sisi wa kwetu wanakatazwa kutumia mifano ya EPA?
 
Daktari wa binadam..si falsafa! Ndiyo maana anaona watoto wanaathirika kisaikolojia.
 
.....watu kama hawa ndio wanatuharibia nchi,bora wangefurahi maana atleast wanafunzi wanapewa hint za ubaya wa ufisadi na hatari yake...huyu mama pls shut up!
 
Huyu ni daktari wa binadamu....ambaye hiyo siakolojia anayosema amesomea wakati hatujamuuliza ni saikology ya wakojwa wakiwa wanaelezea matatizo yao...wakiwa wanaumwa.....si wazima

Na si watu wazima wenye afya ya akili timamu...sasa watoe mfano gani..hata wakisema mwingine mtasema nao unapotosha..ni lini serikari itakubali kuambiwa ukweli...Hao wa EPA.Ndio wamechukua fedha zetu..ambazo zinalingana na mfano unaotolewa na watoto hao.finito.
 
Yaani kuwafanya watoto wafikiri na kuhusisha matatizo yao na ufisadii imekuwa dhambi? Lakini labda anatimiza wajibu wake, msimlaumu sana. Sasa mlitaka afanyeje, awasifie kina Slaa? Ish!

asante.
 
Nadhani ni dactari ambaye hajaelimika. Ukitaka moshi usionekane zima moto siyo kuufunika moshi - utaonekana tu. we daktari tulitegemea ungefanya bidii kuzuia ufusadi na kukamata hao mafisadi wa EPA waliohujumu uchumi wetu!
hivi ni lipi linalokuuma; haki elimu kutusaidia kuwaambia ukweli watoto wetu kinacho sababisha mazingira mabaya ya elimu yao au uchumi wetu unavyoliwa na mafisadi. Au na wewe ni fisadi pia?! Historia itakuja kukuhukumu - rest assured.
 
AJABU kubwa hapa Afrika ni pale wale waliopewa kazi fulani wakashindwa na bado wanashindwa kuifanya kama inavyotakiwa akatokea mtu wa kuwasahihisha na kuwaongoza waifanye barabara basi inakuwa nongwa. Eti mbabaishaji anataka aonekana anaijua kazi yake na hana haja ya kufundishwa kitu na mtu. Huu ndio upumbaravu wa hali ya juu kabisa duniani. Mtu au watu wa namna hii wameishiwa mawazo na fikira na ni vyema wananchi wote wakajua hili.

HakiElimu kila mtu anatambua kwamba wamefanya kazi nzuri katika miaka hii michache ya kuwepo kwao na bado watu wanataraji wawafungue macho juu ya mengi mengine ambayo yanawezekana kufanyika lakini viongozi na hasa wabunge waliopo wanalifanya hili kama vile ni binti sultani kutaka apewe mwezi. Hakielimu endeleeni na sisi hatuna la kuwalipa ila atawalipa Mwenye uwezo naye sio mwingine ila Muumba ardhi na mbingu.

Baada ya kusema hayo niwageukie Hakielimu kwani kuna watu na watu ndani ya taasisi hii na sio kwamba ni mtu mmoja na kuwa wale ambao wamekalia mno eneo moja kwa muda mrefu. Sawa elimu ni muhimu. Lakini mtoto wa Kitanzania hataishi kwa mkate wa elimu peke yake.

Tatizo la Hakielimu nadhani ni kukosa watu wabunifu wanaoweza pia kufikia maeneo mengine na kuyaacha yale ya zamani wakishawasha mwamko wa wananchi kiasi cha kutosha kwenye maeneo kamaa hayao.

Warudi kwenye maandiko ya Rudolf-Steiner na wata 'appreciate' maependekezo yaliyopo hapa chini:

Ninawashauri sasa waanze kampeni za:
. Viwanja vya watoto na kila kata,
. viwanja vya michezo kwa vijana kila kata,
. Deski kwa kila mtoto,
. Vitabu vya kiada na ziada kwa kila mtoto,
. wanafunzi kupewa homework kila siku kwenye masomo yote yanayofundishwa,
. shule za serikali kuiga mfumo wa elimu wa shule za private kwa mafanikio zaidi,
. bustani kila kata
. Kompyuta kama sehemu muhimu ya elimu kwa kila mtoto,
. mazingira bora kwa walimu, shule nzuri bila walimu wazuri ni kama gari bila peteroli,
. bustani kila shule,
. michezo na walimu bora wa michezo kwa kila shule,
. sanaa na muziki na walimu bora wa masomo hayo kwa kila shule,
. zahanati ndogo katika kila shule,
. mashindano na ushindani miongoni mwa shule kuongeza ubora wa kila kitu, kuanzia masomo, michezo, sanaa na usanii na kadhalika,

WAACHE UCHOYO watu wenye mawazo tupo; lakini mkitaka kula wenyewe mtaishia kuvimbiwa na kutapika kisaikolojia na kiitikeli!
 
Koba, nilipo sikia habari hii kwenye headline asubuhi nilidhani mimi ndo nachanganyikiwa!

Ki msingi nilidhani sasa hivi wizara ya elimu ingepaswa kubuni hata topiki kwenye masomo ya wananfunzi kuwafunza watoto wetu wakue wakijua wizi/ rushwa vilivyo vitu vibaya sana ili kwa baadae tupate taifa linalo chukia wizi/rushwa,

Sasa huyu mama anacho jaribu kusema mbona ni kinyume? Haki elimu wana saidia sana kuwaonesha watoto athari za wazi zinazo tokana na wizi wa EPA? badala ashukuru wana saidia sana kuwaonyesha watoto kwamba ni jambo baya yeye anaona ule upande mmoja tu kwamba mafisadi wameguswa??

We mama. acha kulewa madaraka, 'watchout'! Taifa lina angamia hili kwa upuuzi wa namna hii wa kutaka kuliita kolea kijiko kikubwa!

Tunahitaji mafundisho mengi kama haya kwa watoto wetu kwa ajili ya kuandaa taifa linalochukia wizi na udharimu huko mbeleni!

mafano: Nilishangaa nchi moja ugaibuni yaani mtu anfurahia kulipa kodi! nikakumbuka sie bongo wengi hukimbilia kusema nipe kwa bei hiyo sihitaji risiti ( manake bila kodi), nilipo jaribu wadadisi wakanieleza kwamba wanafundishwa toka wadogo kwamba lazima walipe kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa lao!

Sasa leo hii sisi hatutaki kuwafundisha watoto wetu ukweli ili tujenge taifa linalo chukia maovu? DR. Nkya, hebu angalia upande wa pili wa shilingi mama...
 
Ama kweli mama amefika! Kha! Unajua tatizo la hawa viongozi wetu wanafurahi sana kuongoza watu wasio na taarifa! Kama mtu kafanya makosa na yupo Serikalini anachotakiwa kufanya ni kuondoka kuwaacha wasafi waongoze hili jahazi! hakuna chuki yoyote itajengwa kwa Serikali km watoto watafahamu. Hapa ni maadili mema yatajengwa na watoto wataelewa nini maana ya uwajibikaji..hilo ndilo naliona kwenye matangazo hayo. In fact with this kauli za kuropoka za watu kama Dr ndizo zinaweza kufanya wanafunzi waone uongo na uelewa finyu wa walio madarakani. Dr....you are pathetic! I am sorry
 
Iga, what are you talking about? Have you even been to their website? What about their publications, have you seen or read one? The least you can do is read their articles.

.
 
Makubwa haya!
Yaani wenzetu hiki ndicho kinachowaumiza,

.
 
"Alisema kutokana na matangazo na vitendo hivyo kwa sasa, hata watoto wa baadhi ya viongozi wamelazimika kuhamishwa katika shule za kawaida na kupelekwa shule nyingine kwa vile wanaitwa watoto wa mafisadi na wenzao."

Wamehamishwa kutoka shule za kawaida! Hizi ni zipi???? wamepelekwa shule nyingine...LOL!!! watoto wa walala hoi wanalazimika kuacha shule kwa vile hakuna waalimu kwenye shule za Lowassa na pia hawawezi kununua uniform! sio kuhama shule!! hawa wanahama kwa vile wameitwa watoto wa mafisadi. There are Tanzanians and Watanzania! Ama kweli! The gap between is wide to see it as a gap!
 
Last edited:
hii kauli ya lucy nkya ni yake au ni serikali kuhusu haki elimu?
 
hawa watu jamani... hivi hata huu ukeli mdogo wanaombiwa hawautaki kuusikiliza,, hawataki kuona.. hivi tunakwenda wapi?????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…