Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbavu huwa zinaniuma kwa kumkumbuka mwalimu wangu wa Chemistry A-Level, kwani siku moja aliingia darasana na kuuliza DID YOU DONE YOUR WORK?
Kuhusu suala la kiswahili kutumika Tanzania kama lugha ya kielimu hilo bado ni kitendawili na wala halitatufikisha mbali.
Tate naneeeee.. huyu mama si Dokta? au ana udaktari wa kuzuga? sasa leo hii wanafunzi wa uchumi duniani wanatumia hali ya uchumi kama mfano halisi wa masomo yao, sisi wa kwetu wanakatazwa kutumia mifano ya EPA?
.....watu kama hawa ndio wanatuharibia nchi,bora wangefurahi maana atleast wanafunzi wanapewa hint za ubaya wa ufisadi na hatari yake...huyu mama pls shut up!
...Baada ya kusema hayo niwageukie Hakielimu kwani kuna watu na watu ndani ya taasisi hii na sio kwamba ni mtu mmoja na kuwa wale ambao wamekalia mno eneo moja kwa muda mrefu. Sawa elimu ni muhimu. Lakini mtoto wa Kitanzania hataishi kwa mkate wa elimu peke yake.
Tatizo la Hakielimu nadhani ni kukosa watu wabunifu wanaoweza pia kufikia maeneo mengine na kuyaacha yale ya zamani wakishawasha mwamko wa wananchi kiasi cha kutosha kwenye maeneo kamaa hayao.
Warudi kwenye maandiko ya Rudolf-Steiner na wata 'appreciate' maependekezo yaliyopo hapa chini:
Ninawashauri sasa waanze kampeni za:
. Viwanja vya watoto na kila kata,
. viwanja vya michezo kwa vijana kila kata,
. Deski kwa kila mtoto,
. Vitabu vya kiada na ziada kwa kila mtoto,
. wanafunzi kupewa homework kila siku kwenye masomo yote yanayofundishwa,
. shule za serikali kuiga mfumo wa elimu wa shule za private kwa mafanikio zaidi,
. bustani kila kata
. Kompyuta kama sehemu muhimu ya elimu kwa kila mtoto,
. mazingira bora kwa walimu, shule nzuri bila walimu wazuri ni kama gari bila peteroli,
. bustani kila shule,
. michezo na walimu bora wa michezo kwa kila shule,
. sanaa na muziki na walimu bora wa masomo hayo kwa kila shule,
. zahanati ndogo katika kila shule,
. mashindano na ushindani miongoni mwa shule kuongeza ubora wa kila kitu, kuanzia masomo, michezo, sanaa na usanii na kadhalika,
WAACHE UCHOYO watu wenye mawazo tupo; lakini mkitaka kula wenyewe mtaishia kuvimbiwa na kutapika kisaikolojia na kiitikeli!
Serikali yaionya Hakielimu
Halima Mlacha
Daily News; Wednesday,October 22, 2008 @20:19
Serikali imeionya Taasisi ya HakiElimu kuacha kutumia matangazo yake katika vyombo vya habari, kueneza chuki miongoni mwa watoto na vijana nchini na badala yake ingetumia nafasi iliyonayo katika kuwafundisha utawala bora.
Aidha, imewatahadharisha wote wanaoanzisha taasisi za elimu kwa minajili ya kupata fedha bila kuchangia lolote katika sekta ya elimu, ikiwa ni pamoja na shule zinazotoza wazazi fedha nyingi ambazo hazilingani na mazingira na kiwango cha elimu kinachotolewa.
...Alisema kutokana na matangazo na vitendo hivyo kwa sasa, hata watoto wa baadhi ya viongozi wamelazimika kuhamishwa katika shule za kawaida na kupelekwa shule nyingine kwa vile wanaitwa watoto wa mafisadi na wenzao.
...Alisema kama suala la tangazo la EPA limeleta athari hadi kufikia watoto wa viongozi kuhamishwa shule ni jambo hatari, hivyo aliahidi kulifikisha katika Bodi ya Mtandao huo ili walijadili na kulifikisha kwa taasisi hiyo ya HakiElimu.