Hakika aliyeiroga Yanga ana la kujibu kwa Mungu

martial jb

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
863
Reaction score
1,462
Habari waungwana

NDIO AMEONDOLEWA TENA!!! Huyu si mwingine ni dar young africans, hakika hata kipenzi chetu Mwl. JK NYERERE anaweza kushtushwa na taarifa hizi huko alipo, huku akijiuliza "wanashida gani hasa!!??"
Hali kadhalika swali la wengi ni kwa nini kila siku aondoshwe yeye!!? Je, ana laana fulani inayomtafuna? Je hana kiwango!? Je, karogwa kwa kuwekewa zindiko na kunuiziwa kutotoboa kimataifa!!?? Mwisho wa siku klabu hiyo inakosa majibu.

Wakati huo majirani zao wanazidi kujenga heshima kimataifa na umaarufu na kujengeka kibiashara, leo hii michuano ya kimataifa imepelekea Simba kufahamika duniani, kuwa na wafuasi wengi mitandaoni, kufanya mauzo ya jezi nyingi nje ya nchi, kutengeneza mashabiki wengi nje ya NCHI. Na kuipa heshima NCHI.

Masikini muda huo wenzao Yanga wanafurahia mafanikio yao ya ndani na ya muda mfupi kwa viongozi wao wasio na tija na malengo.Kwani leo hii hata Twitter haifahamu kuwa YANGA ni klabu ya soka!! What a shame!!

Kuna jamaa yangu alienda misri akaulizia kuhusu SIMBA SC, hakuamini kwani watu wengi walionyesha kuipenda na kuifahamu vizuri ikiwemo na wachezaji wake, cha kusikitisha wengi wao walimshangaa alipoulizia kuhusu YANGA.

Kiukweli nawapa pole sana Yanga kwa hili janga linalowasibu masikini, nahisi sasa ni muda sahihi wa wao kufanya mabadiliko ya klabu yao kwani hawajachelewa

Na hakika nimeamini mkubwa ni mkubwa siku zote na rekodi zina nafasi yake kwenye mpira, kwani kuvunja rekodi si kitu rahisi. Yanga hana rekodi ligi ya mabingwa Africa na hilo ameendelea kudhihirisha

Kama kurogwa, basi aliyemroga Yanga ana kesi ya kujibu kwa Mungu, na kama wana laana na michuano ya kimataifa basi nawaamuru haraka watubu laana yao kwani itaendelea kuwatafuna.

Namaliza uzi kwa kusema siku zote mzoea vya udalali vya duka haviwezi, na ngoma ikilia sana ujue yaelekea kupasuka
 
Kuna takwimu zinasema

Muda ambao viongoz wa yanga waliotumia kuongea na waandish wa habar n mwingi kuliko muda wa wachezaj kufanya mazoez

Hii n timu iliyowekeza kwa waandish wa habari na s uwanjani

Cafcl hakuna bahasha kule uwezo wako uwanjan tu

Nadhan labda akili zitawakaa mashabik wa yanga na kugundu jins walivyochezewa na viongoz wao



Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
uzuri wa mpira hauchezwi vichakani kama unyago
 
Kweli kabisa....
Wanaongea sana....
Watu wa domodomo tu....
Manara tuuuuuuu basi.....

Ova
 
Mipira ya kuchezeshwa dk 70 na wachezaji Wana anguka kama Wana degedege. Soka la Afini ngumu kupiga hatua.
Mkuu redio hata wewe unaiponda yanga!!?? Kweli mfadhili mbuzi [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Well said
 
Yanga siwadai wamepambana sometimes mpira bahati na bahati haikuwa kwao.

Kama yanga wataingia makundi shirikisho waende kutafuta beki 4 na 5 waache ujinga mwamunyeto sio beki wa kucheza Yanga!!!
 
Mkuu redio hata wewe unaiponda yanga!!?? Kweli mfadhili mbuzi [emoji16][emoji16][emoji16]
Mimi Sina Cha kuwadai wachezaji wa Yanga, wamecheza Kwa uwezo wao ila refa amefanya kazi kubwa sana kuharibu mechi, nashukuru wachezaji walikua watulivu licha ya vituko vingi na mpira kuchezeshwa Kwa dk70 tu.

Maana Kila baada ya dk 4 mchezaji wa Al Hilal ana anguka, mpaka akitolewa akatibiwe amesha kula dk 2-3 na refa hachukui hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…