Uchaguzi 2020 Hakika Dkt. Magufuli haamini macho yake. Alifikiri A, imekuwa B!

Pamoja na kuubana vilivyo upinzani kwa miaka yake mitano madarakani, haamini kuuona ukiwa na nguvu kwa namna hii hadi kuomba msaada wa wastaafu. Pamoja na kuuaminisha umma, tangu kuingia kwake madarani, kuwa anapendwa, anakubalika, anaheshimika na anaaminika kuliko yeyote yule kwenye uongozi, Dr. Magufuli haamini kuona wananchi 'wakitamani' kumuondoa madarakani kwa kura zao Oktoba 28.

Pamoja na 'mikwara' yake kwa makada wa CCM walioachwa pembeni wakati wa kura za maoni kuwa ni LAZIMA wawaunge mkono wagombea waliopitishwa na CCM yetu, Dr. Magufuli haamini macho yake anaposhuhudia sura za kukasirika na ghadhabu za makada hao. Makada wa maelfu nchi nzima wamejipanga kuwapigia kura wapinzani kwakuwa walioletewa hawakuwachagua.

Pamoja na kutumia jukwaa la Urais kwa miaka mitano kujinadi, kujiaminisha na kujitamba mbele ya watanzania, Dr. Magufuli hayaamini macho yake anapoona watanzania hawamulewi kwenye kampeni zake na hata hawasisimuliwi na ahadi zake tena. Wamejaa uchungu mioyoni mwao; wamepoteza matumaini kuliko kuyapata. Watanzania wanataka kuanza upya. Wanataka mabadiliko. Wanashindwa kumuelewa Dr. Magufuli.

Hakika, Dr. Magufuli haamini anachokiona. Ametarajia A, anaona B. Wako wapi wale waliokuwa wakimshabikia miaka yote mitano? Wako wapi waunga mkono juhudi? Ni wazi, tafakari atakayoifanya Chato kuanzia jana hadi tarehe 14/9/2020 itajikita katika kujiuliza: amewakosea nini watanzania hadi wampe 'surprise'hii ya kiuchaguzi? Atakapoanza na Kagera, ajirekebishe na ikibidi aombe radhi kwa kuteleza kwake kwa hili na lile.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kahama, Shinyanga)
Mkuu tukutane Chila
 
Fahari ya nyumbu ni kufarijiana hata wakiwa mbele ya mdomo wa Simba.

Hongera chadema
Kama anakubalika kwakuwa anajenga barabara
DIAMOND
Zuchu na msaga sumu wanaenda kufanya nn kwenye mikutano take?
Alidhani kupora KOROSHO kutamuacha salama?
 
Hajaja
Pamoja na kuubana vilivyo upinzani kwa miaka yake mitano madarakani, haamini kuuona ukiwa na nguvu kwa namna hii hadi kuomba msaada wa wastaafu. Pamoja na kuuaminisha umma, tangu kuingia kwake madarani, kuwa anapendwa, anakubalika, anaheshimika na anaaminika kuliko yeyote yule kwenye uongozi, Dr. Magufuli haamini kuona wananchi 'wakitamani' kumuondoa madarakani kwa kura zao Oktoba 28.

Pamoja na 'mikwara' yake kwa makada wa CCM walioachwa pembeni wakati wa kura za maoni kuwa ni LAZIMA wawaunge mkono wagombea waliopitishwa na CCM yetu, Dr. Magufuli haamini macho yake anaposhuhudia sura za kukasirika na ghadhabu za makada hao. Makada wa maelfu nchi nzima wamejipanga kuwapigia kura wapinzani kwakuwa walioletewa hawakuwachagua.

Pamoja na kutumia jukwaa la Urais kwa miaka mitano kujinadi, kujiaminisha na kujitamba mbele ya watanzania, Dr. Magufuli hayaamini macho yake anapoona watanzania hawamulewi kwenye kampeni zake na hata hawasisimuliwi na ahadi zake tena. Wamejaa uchungu mioyoni mwao; wamepoteza matumaini kuliko kuyapata. Watanzania wanataka kuanza upya. Wanataka mabadiliko. Wanashindwa kumuelewa Dr. Magufuli.

Hakika, Dr. Magufuli haamini anachokiona. Ametarajia A, anaona B. Wako wapi wale waliokuwa wakimshabikia miaka yote mitano? Wako wapi waunga mkono juhudi? Ni wazi, tafakari atakayoifanya Chato kuanzia jana hadi tarehe 14/9/2020 itajikita katika kujiuliza: amewakosea nini watanzania hadi wampe 'surprise'hii ya kiuchaguzi? Atakapoanza na Kagera, ajirekebishe na ikibidi aombe radhi kwa kuteleza kwake kwa hili na lile.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kahama, Shinyanga)
Hajajaaliwa uwezo wa kujinyenyekeza na kukiri kukosea,amejaa kiburi na visasi visivyokuwa na umuhimu wowote.Ndiyo maana anabakia kushangaa kuona Watanzania siyo watu wa kushabikia matendo ya kunyanyasa na kuonea wananchi wenzao.Wanaomwelewa huyu Mzee ni kina Samia,Majaliwa,Pinda,Polepole,Lusinde,Musukuma,Makonda a.k.a Bashite,Gambo,Mnyeti na wanaofanania nao.
Mzee Tupatupa,heshima kwa uchambuzi murua.Upo bado upande wa hawa watesi wetu?Kama siyo,i'm so sorry.But if you are against them,please let others know the truth.Let you personally make sure you convince as many voters against this insanity as possible.I'm sure we can,our powers are greater than theirs!
 
Pale kibaha Leo Lisu amemwaga sumu ya aina yake yaani wale wooote waliovunjiwa nyumba zao kulipwa na serikali ya Chadema. Hapo sikilizia mziki wake.
 
Kwaiyo Lissu ndio atakununulia Nguo?
Jitume tafuta pesa kwa Akili na jasho lako, Watu wananunua ndinga mpya kila siku wewe unafikiria Lissu atakupa nafuu ya Maisha.
Wewe huna hoja, Viongozi wa wanaoingia madarakani wana mchango mkubwa katika maisha yako ya kila siku, kataa kubali huo ndio ukweli usijotoe ufahamu mkuu.
 
Matikiti maji yanauzwa 2000 kwa moja nenda kalime kama hutopata hela,wewe unabeti alafu utegemee kupata hela.
Na wewe ndio wale wanaolima matikiti kwenye magroup ya. Wasapu?

Acheni kudanganya wenzenu, mnauza unga kuumiza watoto wa watu halafu unawadanganya wenzako kilimo cha matikiti kinalupa, jaribu wewe uwone mziki wake.
 
Kama unataka Mali utaipata shambani kama unataka maneno mfuate tobolisu.
 
Magufuli ameturudisha nyuma sana kwa kuvunja Sheria
Miradi mingi haijafuata utaratibu
Unanunua ndege kwa cash bila utaratibu wakati mazao ya wakulima unakopa hii imekaaje
Ndege zikianza kutoa profit ndo ttaanza kulipa cash na nyongez kwa manufaa ya mkulima.
 
Jaman aliye karibu na baba mwambie; Mbona hatujazisikia sera zetu? Kile kitabu cha page 300 kakimaliza hadi akimbilie za Lisu? Amwachie Polepole huyo dogoo Lisu yeye azame tu kwenye kile kitabu chetu cha page 300. Sera yetu, Yatoshaa. Tunamrudisha tena 5yrs more kwa kile kitabu chetu tu.
 
Mkuu umehama lini to CCM?

Haya sasa ni matusi! Mimi na CCM wapi na wapi!! Bora niwe mwanachama wa Chauma, ila siyo CCM. Sema tu nina desturi ya kukiunga mkono chama chochote chenye ndoto ya kuiondoa ccm madarakani.

Kiufupi tu mimi ni Mtanzania Mzalendo na Mpenda mabadiliko, nisiye na chama.
 
Haya bhana! labda nimekufananisha!!
 
Back
Top Bottom