Nilipomaliza kidato cha sita, nilienda kwa binamu yangu mkoa wa Mara . Nikapata maambukizi ya staphylococcus. Nilijua ni bacterial infection kwakuwa baada ya kutibu mara kadhaa bila mafanikio, ilibidi kufanya kipimo cha culture.
Aisee ugonjwa ulinitesa , maana Kila nikimaliza dozi siponi. Yaani mayibabu yenyewe yalikuwa ya kusuasua kwakuwa nilikuwa nategemea fedha ya matibabu kutoka kwa binamu.
Baada ya kusubiri kwa muda huku nikiendelea kuugua, hatimaye Bina akanipa tsh2000/- nikatibwe. Kwa miaka Ile ilikuwa hela nyingi. Nimefika hospitali ya mkoa, nikajiandikisha , hatimaye nikaingia kwa daktari. Nikamweleza jinsi nimekuwa na maumivu kwenye njia ya mkojo kwa muda mrefu, na dawa nilizokwishakutumia. Ajabu, akaniambia ili aniandikie dawa, nitampa 2000/-.Nikawa nimemwelewa kuwa anataka rushwa. Nikakubali lakini nikapania moyoni kuwa nitamkomesha. Akaniandikia Vipimo, nikaenda maabara, baada ya mchakato kuisha nikarudi chumbani kwa daktari.
Akaniandikia dawa pale na kunielekeza kuwa niende nikazinunue. Nikambadilikia , nikamwambia wee jamaa nimeshakulipa Kila kitu hapa siondoki bila dawa. Akashangaa maana niliongea kwa sauti ili hata walio nje wasikie . Akaona hili ni Soo . Akachomoa Ile buku mbili akanipa, nikachukua cheti nikatoka nje. Nikapitia dirisha la dawa nikanunua nirudi home. Bahati nzuri nilipona.