VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Spika Dr. Tulia Ackson Mwansasu, msomi wa kiwango cha Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town, Afrika ya Kusini sasa anadhalilishwa na kutwezwa na siasa. Msomi huyu na Mhadhiri wa zamani wa UDSM (mwanangu ambaye kwasasa naye ni Mhadhiri hapo alifundishwa naye) sasa ni dhahiri anazidiwa nguvu na siasa.
Siasa za kisasa zinataka matumizi sahihi ya fani, ujuzi na uzoefu juu ya mambo ambayo mwanasiasa anajihusisha nayo. Hata kwenye michakato ya kuwapata viongozi kwenye mihimili na kwingineko, mambo hayo huzingatiwa. Bunge ni chombo cha kutunga sheria na kuisimamia Serikali. Kinapaswa kuongozwa na mwerevu wa, pamoja na mambo mengine, sheria.
Pamoja na kwamba kwasasa amehama kwenye tasnia ya sheria (alikofika ngazi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali) na kuhamia siasani, Dr. Tulia anapaswa kuwa mfano mwema. Anapaswa kuwaonesha watanzania kuwa taaluma yake ya sheria inatusaidia sote kupitia nafasi ya Uspika aliyonayo. Bado anapaswa kuzungumza kama mwanasheria-kuzungumza facts zaidi ya porojo na hoja kuliko vihoja.
Jambo hili la Mkataba wa DP World ni la kisheria. Sote tulimtegemea tangu Bungeni kulizungumza na kuliongoza kisheria kwa maslahi mapana ya Tanzania yetu. Lakini, siasa ikamzidi nguvu. Akafanya alivyoagizwa kichama na kiserikali badala ya kadiri ya taaluma yake. Bado, huko Mbeya, anaendelea kuliletea porojo, dhihaka na kebehi jambo hili na wale wanaolizungumzia. Siasa inamdhalilisha na kumtweza.
Katika mifumo ya kiintelijensia na kiutawala, sisi wabobevu wa mambo ya kiuongozi huwa tunaamini kuwa yeyote anayepewa chochote asichostahili au bila kutegemea, huyo huwa mnyenyekevu hadi kuwa mbovu. Anayestahili akipata husimama imara. Kukosa sifa huleta woga. Huleta kutojiamini. Hukufanya kuangalia pande zote kila mara. Huleta 'utumwa' wa kifikra.
Rais Samia, maoni yako ni yapi kuhusiana na Mkataba wa DP World?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam