Hakika uanasiasa unamdhalilisha na kumuanika Spika Tulia A. Mwansasu

Hakika uanasiasa unamdhalilisha na kumuanika Spika Tulia A. Mwansasu

20230714_183713.jpg
20230714_183713.jpg

Sina Mengi Sana
 
Spika Dr. Tulia Ackson Mwansasu, msomi wa kiwango cha Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town, Afrika ya Kusini sasa anadhalilishwa na kutwezwa na siasa. Msomi huyu na Mhadhiri wa zamani wa UDSM (mwanangu ambaye kwasasa naye ni Mhadhiri hapo alifundishwa naye) sasa ni dhahiri anazidiwa nguvu na siasa.

Siasa za kisasa zinataka matumizi sahihi ya fani, ujuzi na uzoefu juu ya mambo ambayo mwanasiasa anajihusisha nayo. Hata kwenye michakato ya kuwapata viongozi kwenye mihimili na kwingineko, mambo hayo huzingatiwa. Bunge ni chombo cha kutunga sheria na kuisimamia Serikali. Kinapaswa kuongozwa na mwerevu wa, pamoja na mambo mengine, sheria.

Pamoja na kwamba kwasasa amehama kwenye tasnia ya sheria (alikofika ngazi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali) na kuhamia siasani, Dr. Tulia anapaswa kuwa mfano mwema. Anapaswa kuwaonesha watanzania kuwa taaluma yake ya sheria inatusaidia sote kupitia nafasi ya Uspika aliyonayo. Bado anapaswa kuzungumza kama mwanasheria-kuzungumza facts zaidi ya porojo na hoja kuliko vihoja.

Jambo hili la Mkataba wa DP World ni la kisheria. Sote tulimtegemea tangu Bungeni kulizungumza na kuliongoza kisheria kwa maslahi mapana ya Tanzania yetu. Lakini, siasa ikamzidi nguvu. Akafanya alivyoagizwa kichama na kiserikali badala ya kadiri ya taaluma yake. Bado, huko Mbeya, anaendelea kuliletea porojo, dhihaka na kebehi jambo hili na wale wanaolizungumzia. Siasa inamdhalilisha na kumtweza.

Katika mifumo ya kiintelijensia na kiutawala, sisi wabobevu wa mambo ya kiuongozi huwa tunaamini kuwa yeyote anayepewa chochote asichostahili au bila kutegemea, huyo huwa mnyenyekevu hadi kuwa mbovu. Anayestahili akipata husimama imara. Kukosa sifa huleta woga. Huleta kutojiamini. Hukufanya kuangalia pande zote kila mara. Huleta 'utumwa' wa kifikra.

Rais Samia, maoni yako ni yapi kuhusiana na Mkataba wa DP World?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Uko sahihi. Nimesikia kwa masikio yangu mawili akitukana (bila shaka) akina Prof. Shivji, Tibaijuka, etc; akina Dr. Slaa, Nshala, etc; wanasheria wenzie akina Mwabukusi, Madeleka, etc; Wazee akina Warioba, Butiku, etc; kwamba, ni WAPUMBAVU. Duuh, pesa na madaraka; eeh Mungu tusaidie!
 
Elimu haijawahi kuwabadilisha watu wa pande izo. Mtu hata awe na digrii mia, bado vile vitabia vya kinyakyusa vinakuwepo.
Unakumbuka jinsi Daktari Mwakyembe msomi mwenye digrii nne alivyomchamba na kumsagia kunguni waziri mkuu wa kipindi kile Eddo Ngoyai Lowasa. Bila hata ya kumsitiri kwa kumuacha na kipensi, mzee wa watu alivuliwa nguo zote mbele ya kadamnasi, katikati ya vikao vya bunge.
Msomi mwakyembe alikuwa anachamba kuliko wale wanawake wa kiswahili wa Buza na Mbagala! Unakumbuka!
wewe wa pande gani? unatukana watu! ubaguzi ni ujinga wa hali ya juu. Usi generalize watu wote wa pande hizo unazozichukia kwamba kila mtu yuko hivyo huo ni upuuzi wa hali ya juu sana, umenikera kwelikweli. Wabunge walikuwa wanaungamkono wote ni pande hizo?? Ubaguzi na dharau ni ugonjwa mbaya sana
 
Kwamba Mwakyembe kuanika ukweli ilikuwa kosa na 'vitabia vya kinyakyusa'? Na huyu spika kukumbatia ujinga pia ni kosa? Pick a lane!

Lowasa alikuwa mwana mtandao wa mafisadi. Alishiriki kikamilifu kwenye uhuni wote wa 2005.
Huyo Mzee anaemsifia ndiyo walioharibu nchi hii na mtandao wao, jamaa nimedharau sana ametoka kwenye hoja anashambulia Kabila, inaelekea ni mtu mwenye uwezo mdogo sana wakufikili!
 
Hakuna sehemu inayoharibu taaluma ya mtu kama ccm.
Kuna Phd nyingi sana katika taifa hili ambapo kama zingekuwa zinapewa nafasi na uhuru taifa lingekuwa na hatua walao nyingi mbele.
Ndio maana kuna jamaa mmoja aliiterm abbreviation ya PhD kama permanent head destruction
 
Yani mpaka mwenyewe najiuliza siasa ina nini ndani yake?
Maana kawakusanya watu ambao hawaelewi kitu anasema anatoa elimu kuhusu mkataba, afu wao wanasema tuko nae bega kwa bega hata kwenye misiba, ametukopesha peas, Bajaji, nk
Afu yeye ameona kamaliza
Tulia ametulizwa akili
 
wewe wa pande gani? unatukana watu! ubaguzi ni ujinga wa hali ya juu. Usi generalize watu wote wa pande hizo unazozichukia kwamba kila mtu yuko hivyo huo ni upuuzi wa hali ya juu sana, umenikera kwelikweli. Wabunge walikuwa wanaungamkono wote ni pande hizo?? Ubaguzi na dharau ni ugonjwa mbaya sana
Pole...
 
Elimu haijawahi kuwabadilisha watu wa pande izo. Mtu hata awe na digrii mia, bado vile vitabia vya kinyakyusa vinakuwepo.
Unakumbuka jinsi Daktari Mwakyembe msomi mwenye digrii nne alivyomchamba na kumsagia kunguni waziri mkuu wa kipindi kile Eddo Ngoyai Lowasa. Bila hata ya kumsitiri kwa kumuacha na kipensi, mzee wa watu alivuliwa nguo zote mbele ya kadamnasi, katikati ya vikao vya bunge.
Msomi mwakyembe alikuwa anachamba kuliko wale wanawake wa kiswahili wa Buza na Mbagala! Unakumbuka!
Badala ya kuleta hoja unaleta ukabila
 
Back
Top Bottom