Hakikisha unafanya kwa ukubwa Biashara yako wakati unaanza

Hakuna jambo gumu katika biashara kama mwanzo, biashara nyingi hufa mwanzoni si kwasababu hamna wateja ila ni kutokana na ufinyu wa mtaji na na kwa wenye mitaji kutojua nini cha kuuza na kipi kianze kipi kifate.

Leo nataka nimsaidie mawazo mtu mwenye mtaji anaetaka kuanza kufanya biashara ila hajui aianze anze vipi, Kuwa na idea ya biashara sio issue sasa hivi issue ni namna ya kuingiza hiyo idea yako kwenye vitendo hapo ndio patamu.

Iko hivi hizi idea sio kwamba ni perfect 100 percent ila napenda kuwapa mbinu na njia nilizotumia na kuona mafanikio yake (kuna baadhi ya wana JF they know me nnje ya JF) kuwa katika hii njia hakuna biashara nitaifungua popote kwasasa iniangushe (nikishasema YES kwenye biashara flani) hii ndio njia yangu pendwa ya namna huwa naanza biashara yoyote ile.

Kwenye biashara hakunaga mtaji unaotosha hata kama biashara iwe ina mtaji mdogo kiasi gani nakuhakikishia hakuna biashara utaingia ikajikamilisha, Kwanini? kwasababu biashara si yako ni ya wateja

Je, unajua wateja wote hii dunia wanataka nini kwenye hiyo biashara yako? jibu ni NO hivyo basi itoshe kuweka akilini kwamba huwezi kuwa namtaji ukatosheleza mahtaji ya mteja.

Ukishajua hilo sasa unaanzaje?

Yawezekana upo mahali umeshawaza biashara unayotaka kufungua ni Kuuza Genge Ndio kuuza genge ni biashara nzuri sana,genge maana yake ni kuuza vitu kama nyanya,karot, na vikorombwezo vingine kibao...

Mkononi una 100k yani LAKI 1, umeshaandaa kibanda chako umebaki mkononi na laki kamili Unajiuliza kesho sokoni ukanunue nini uache nni! huelewi

Acha nikwambie, nimesema "hakikisha unaianza biashara yako kwa Ukubwa bila kujalisha ni biashara gani" Mkononi una Laki moja, badala ya kwenda kununua nyanya tenga, vitunguu vya 10k,hoho za 20k, kabichi za 10k,nk nk yani unagusa gusa kila mahali kidogo kidogo (makosa makubwa hayo) Kubali kuanzia chini.

Nenda sokoni,umeshajua Hamna mboga itapikwa bila nynya,HAKUNA maana yake ni kwamba kwenye mboga nyanya ni kama beki anaecheza kulia na kushoto Nyanya ndio kila kitu kwenye biashara ya GENGE, nani anauza genge hauzi nyanya, HAKUNA.

Umeshalijua hilo na mkononi una Laki,ingia sokoni Tenga 1 ni 15k (mfano) chukua matenga yako manne kwa 60k changanya za kuiva tenga 1 mbichi tenga 3, = 60k unabaki na 40k usafiri weka 10k unabaki na 30k hii 30k nunua visado vyakupimia nyanya zako ujazo tofauti, beba mzigo wako hadi kibandani kwako.

Mwaga mezani nyanya zako zipange zipangike,una nyanya nyingi maana yake bei yako itakua chini kuliko wenzio wenye vitenga vimoja vimoja,Anza genge lako na NYANYA tu uza nyanya wateja wa wenzako watakua wanakuja nunua nyanya kwako, hamnaga mteja asiependa sehemu yenye mzigo wa kutosha na nyongeza,utauza sana nyanya zako, baadae mtaji ukikua utaongeza Vitunguuu Utaratbu ni ule ule Una ki 50,000 yote kanunulie vitunguuuu Leta gengeni kwako anza endelea na kazi...Tukutane december uone hilo genge litakavyokua.

Yawezekana ni MAMA NTILIE unataka kuanza biashara ya Chakula

Mkononi umefanya kila kitu umebaki na 50,000 usipasuke kichwa eti nipike ugali nusu,wali kilo,pilau nusu,nk nk Acha kugusa gusa

Hakuna msosi unaolika kwa mama ntilie kama UGALI sasa una 50,000 chakufanya Tupia 50,000 yote kwenye Ugali nenda fata unga kilo zako 4 mboga weka za kutosha dagaa,kachumbari,mboga za majani,marage,mlenda kidogo Kisha Pika kila kitu in a professional way kuanzia ugali wako,mboga zako, mpka katika upakuaji sahani zako ziwe safi...

mteja akija akiulizia wali mwambie Umeisha,ulipika kidogo ila kuna UGALI MBOGA SABA anakwambia nipakulie ugali (kanasa huyo) hakikisha hukosei mpakulie vizuri panga mboga kama unampakulia mumeo home,peleka mezani mnawishe mteja, Biashara haina uchawi umemaliza hiyo Akila akimaliza asipoongeza niite CONTROLA nimekaa pale.

Ugali utaisha wote,kusanya wateja kwa bidhaa yako moja wakishakolea waulize jamani Kesho nataka wapikia Wali au Pilau vipiiii nipikee,Pokea maoni Acha kukurupuka kujipikia tu chakula huli wewe wanakula wateja Kusanya data kabla hujaingia Jikoni. Tukutane december tuone kama utakua unauza ugali tu.

Kuna mwingine anatamani kufanya biashara ya UWAKALA anahangaikaa anapata laini zote kuu 3 tigo voda airtel, mtaji wake 500k Acha nikwambie angalia mkoa au eneo ulilopo wateja wengi wapo mtandao upi,kama ni TIGO

Weka Voda na Airtel pembeni Float yote jaza na Tigo cheza na tigo toa weka na tigo kamisheni ukipokea ongeza mtaji na TIGO usikubali kuwakosa wateja wa TIGO brand ofisi yako na mabango yamtandao unaopga nao kazi tuuu usiweke tangazo la mtandao mwingine (nina maana yangu nikisema hivi) Anza kwa ukubwa huo huo na mtandao wako mmoja ukiwa na float ya kutosha,Mtaji ukiongezeka ONGEZA mtandao mwingine,hvyo hvyo Mpaka december tutambiana habari ilivyo.

Biashara ya Gas

Kampuni ni nyingi mitaji ni midogo jitahidi uanze kwa ukubwa tunaousemea hapa angalia una kiasi gani badala yakuanza na gas kampuni zote anza na 1 baada ya nyingine taratbu taratbu hadi utafikia lengo lako la kuuza gas aina zote kampuni zote.

Mifano ni Mingi lakini nimetolea hiyo michache,Hakikisha hugusi gusi kila kitu kuna faida nyingi kuanza kwa ukubwa na kutogusa gusa.

Unapoanza biashara hakikisha hutilii huruma na fanya kitu watu wajue uko serious na unachokifanya sio kufanya kwa kujjaribu jaribu maana wanaofanya kwa kugusa gusa ni wanaojaribu incase hiki hakijanunuliwa kinunuliwe hiki,sasa biashara haitaki majaribio biashara inataka ufanye, IFE uinuke Ufanye tena hamna kujaribu jaribu.

Eti unaanza mama ntilie leo unapika wali nusu ugali kilo wateja wa 5 tu washamaliza msosi woteee,Anza na kitu kimoja kwa ukubwa. Kila biashara ianzwe kwa ukubwa na itakulipa kwa ukubwa huo huo ulio amua kuanzza nao.

Watakwambia weka na hiki na kile pokea ushauri wao lakini mimi nakuambia Anza na Kimoja Kwa ukubwa kisha vingine vitafata.

CONTROLA 2023
Asante kwa wazo zuri la biashars mkuu. Je, kwa mimi ninayetaka kuanzisha biashara ya kilimo nianze na ekari ngapi mkuu?
 
Hi idea Ni nzuri

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Hata siku 1 biashara haitokufia mkononi kama ukiweza Apply hii idea, Ndio mana nawambia watu

mimi biashara kunishinda itasubiri sana maana sio mtu wa kusubiri biashara inishinde nianze nyingine

mpya,Naanza biashara mpya hapo hapo kwenye biashara iliyopo Hata kama nauza bucha la nyama

kubadilishia gia hewani bucha nikaligeuza super market ni dakika sifuri tu Nyama zinaisha nabaki na super market...

Kuna mteja unaenda dukani kwake unaona kabisa huyu anamalizia KODI asepe,duka jeupe pee Unamuuliza bei

ya bidhaa anakutajia BEI kama vile duka lake limejikamilisha yani,Haogopi kudodewa yeye yupo na bei zake sawa

na wenzake ambao maduka yao yamejikamilisha mpaka na ma AC ndani,Unamsikitikia kisha unamwambia ASANTE unaondoka hununui kitu.

Anakuja anaachia FREM ana bidhaa kibao zimebaki anatafuta wakumuuzia,anakuja kuuza kwa nusu ya bei aliyonunulia... wakati alikua na uwezo wakurudisha hela yake akawa amepata hasara 1 tu ya (Muda) .

Biashara kufa mikononi mwako ni uzembe na kutokua na akili ya kuwaza zaidi ya hapo ulipo na zaidi ya hicho unachofanya sasa hivi.
 
Asante kwa wazo zuri la biashars mkuu. Je, kwa mimi ninayetaka kuanzisha biashara ya kilimo nianze na ekari ngapi mkuu?
Kilimo cha kutegemea Mvua za Muuumba Sina hata la kuweza kukushauri Mkuu

Kama unafanya kilimo cha umwagiliaji atleast tunaweza ongea LUGHA 1,nakubali

biashara ni (Betting) lakini biashara ya kilimo cha kutegemea Mvua za Msimu kwangu

mimi naona ni kama Kucheza BIKO mshiko nnje nnje (cheza sasa hiyo biko uone huo mshiko nnje nnje)
 
Nataka kulima kilimo cha kumwagilia mkuu. Nianzeje?
 
Hakuna jambo gumu katika biashara kama mwanzo, biashara nyingi hufa mwanzoni si kwasababu hamna wateja ila ni kutokana na ufinyu wa mtaji na na kwa wenye mitaji kutojua nini cha kuuza na kipi kianze kipi kifate.

Leo nataka nimsaidie mawazo mtu mwenye mtaji anaetaka kuanza kufanya biashara ila hajui aianze anze vipi, Kuwa na idea ya biashara sio issue sasa hivi issue ni namna ya kuingiza hiyo idea yako kwenye vitendo hapo ndio patamu.

Iko hivi hizi idea sio kwamba ni perfect 100 percent ila napenda kuwapa mbinu na njia nilizotumia na kuona mafanikio yake (kuna baadhi ya wana JF they know me nnje ya JF) kuwa katika hii njia hakuna biashara nitaifungua popote kwasasa iniangushe (nikishasema YES kwenye biashara flani) hii ndio njia yangu pendwa ya namna huwa naanza biashara yoyote ile.

Kwenye biashara hakunaga mtaji unaotosha hata kama biashara iwe ina mtaji mdogo kiasi gani nakuhakikishia hakuna biashara utaingia ikajikamilisha, Kwanini? kwasababu biashara si yako ni ya wateja

Je, unajua wateja wote hii dunia wanataka nini kwenye hiyo biashara yako? jibu ni NO hivyo basi itoshe kuweka akilini kwamba huwezi kuwa namtaji ukatosheleza mahtaji ya mteja.

Ukishajua hilo sasa unaanzaje?

Yawezekana upo mahali umeshawaza biashara unayotaka kufungua ni Kuuza Genge Ndio kuuza genge ni biashara nzuri sana,genge maana yake ni kuuza vitu kama nyanya,karot, na vikorombwezo vingine kibao...

Mkononi una 100k yani LAKI 1, umeshaandaa kibanda chako umebaki mkononi na laki kamili Unajiuliza kesho sokoni ukanunue nini uache nni! huelewi

Acha nikwambie, nimesema "hakikisha unaianza biashara yako kwa Ukubwa bila kujalisha ni biashara gani" Mkononi una Laki moja, badala ya kwenda kununua nyanya tenga, vitunguu vya 10k,hoho za 20k, kabichi za 10k,nk nk yani unagusa gusa kila mahali kidogo kidogo (makosa makubwa hayo) Kubali kuanzia chini.

Nenda sokoni,umeshajua Hamna mboga itapikwa bila nynya,HAKUNA maana yake ni kwamba kwenye mboga nyanya ni kama beki anaecheza kulia na kushoto Nyanya ndio kila kitu kwenye biashara ya GENGE, nani anauza genge hauzi nyanya, HAKUNA.

Umeshalijua hilo na mkononi una Laki,ingia sokoni Tenga 1 ni 15k (mfano) chukua matenga yako manne kwa 60k changanya za kuiva tenga 1 mbichi tenga 3, = 60k unabaki na 40k usafiri weka 10k unabaki na 30k hii 30k nunua visado vyakupimia nyanya zako ujazo tofauti, beba mzigo wako hadi kibandani kwako.

Mwaga mezani nyanya zako zipange zipangike,una nyanya nyingi maana yake bei yako itakua chini kuliko wenzio wenye vitenga vimoja vimoja,Anza genge lako na NYANYA tu uza nyanya wateja wa wenzako watakua wanakuja nunua nyanya kwako, hamnaga mteja asiependa sehemu yenye mzigo wa kutosha na nyongeza,utauza sana nyanya zako, baadae mtaji ukikua utaongeza Vitunguuu Utaratbu ni ule ule Una ki 50,000 yote kanunulie vitunguuuu Leta gengeni kwako anza endelea na kazi...Tukutane december uone hilo genge litakavyokua.

Yawezekana ni MAMA NTILIE unataka kuanza biashara ya Chakula

Mkononi umefanya kila kitu umebaki na 50,000 usipasuke kichwa eti nipike ugali nusu,wali kilo,pilau nusu,nk nk Acha kugusa gusa

Hakuna msosi unaolika kwa mama ntilie kama UGALI sasa una 50,000 chakufanya Tupia 50,000 yote kwenye Ugali nenda fata unga kilo zako 4 mboga weka za kutosha dagaa,kachumbari,mboga za majani,marage,mlenda kidogo Kisha Pika kila kitu in a professional way kuanzia ugali wako,mboga zako, mpka katika upakuaji sahani zako ziwe safi...

mteja akija akiulizia wali mwambie Umeisha,ulipika kidogo ila kuna UGALI MBOGA SABA anakwambia nipakulie ugali (kanasa huyo) hakikisha hukosei mpakulie vizuri panga mboga kama unampakulia mumeo home,peleka mezani mnawishe mteja, Biashara haina uchawi umemaliza hiyo Akila akimaliza asipoongeza niite CONTROLA nimekaa pale.

Ugali utaisha wote,kusanya wateja kwa bidhaa yako moja wakishakolea waulize jamani Kesho nataka wapikia Wali au Pilau vipiiii nipikee,Pokea maoni Acha kukurupuka kujipikia tu chakula huli wewe wanakula wateja Kusanya data kabla hujaingia Jikoni. Tukutane december tuone kama utakua unauza ugali tu.

Kuna mwingine anatamani kufanya biashara ya UWAKALA anahangaikaa anapata laini zote kuu 3 tigo voda airtel, mtaji wake 500k Acha nikwambie angalia mkoa au eneo ulilopo wateja wengi wapo mtandao upi,kama ni TIGO

Weka Voda na Airtel pembeni Float yote jaza na Tigo cheza na tigo toa weka na tigo kamisheni ukipokea ongeza mtaji na TIGO usikubali kuwakosa wateja wa TIGO brand ofisi yako na mabango yamtandao unaopga nao kazi tuuu usiweke tangazo la mtandao mwingine (nina maana yangu nikisema hivi) Anza kwa ukubwa huo huo na mtandao wako mmoja ukiwa na float ya kutosha,Mtaji ukiongezeka ONGEZA mtandao mwingine,hvyo hvyo Mpaka december tutambiana habari ilivyo.

Biashara ya Gas

Kampuni ni nyingi mitaji ni midogo jitahidi uanze kwa ukubwa tunaousemea hapa angalia una kiasi gani badala yakuanza na gas kampuni zote anza na 1 baada ya nyingine taratbu taratbu hadi utafikia lengo lako la kuuza gas aina zote kampuni zote.

Mifano ni Mingi lakini nimetolea hiyo michache,Hakikisha hugusi gusi kila kitu kuna faida nyingi kuanza kwa ukubwa na kutogusa gusa.

Unapoanza biashara hakikisha hutilii huruma na fanya kitu watu wajue uko serious na unachokifanya sio kufanya kwa kujjaribu jaribu maana wanaofanya kwa kugusa gusa ni wanaojaribu incase hiki hakijanunuliwa kinunuliwe hiki,sasa biashara haitaki majaribio biashara inataka ufanye, IFE uinuke Ufanye tena hamna kujaribu jaribu.

Eti unaanza mama ntilie leo unapika wali nusu ugali kilo wateja wa 5 tu washamaliza msosi woteee,Anza na kitu kimoja kwa ukubwa. Kila biashara ianzwe kwa ukubwa na itakulipa kwa ukubwa huo huo ulio amua kuanzza nao.

Watakwambia weka na hiki na kile pokea ushauri wao lakini mimi nakuambia Anza na Kimoja Kwa ukubwa kisha vingine vitafata.

CONTROLA 2023
Boss shukrani sana naomba unipe na mfano wa stationery CONTROLA
 
Boss madini mazuri sana kwakweli....vip kuna mweny idea ya bajaji kuendesha mwenyew
 
Ibaki hvyo tu kuwa ukitaka kuona hell za bajaji au kiriku endesha mwenyewee ,haswa bajaji uatafika mbali na ndani ya mwak utakuwa umesha Jenga kina da mkuu
 
Huu ni ukweli mtupu Hii ya ugali mboga saba mkuu nimeishuhudia Kuna mama ntilie mmoja anaishi nayo hii na raia wanamgombea htari sio uchawi
 
Hata siku 1 biashara haitokufia mkononi kama ukiweza Apply hii idea, Ndio mana nawambia watu

mimi biashara kunishinda itasubiri sana maana sio mtu wa kusubiri biashara inishinde nianze nyingine

mpya,Naanza biashara mpya hapo hapo kwenye biashara iliyopo Hata kama nauza bucha la nyama

kubadilishia gia hewani bucha nikaligeuza super market ni dakika sifuri tu Nyama zinaisha nabaki na super market...

Kuna mteja unaenda dukani kwake unaona kabisa huyu anamalizia KODI asepe,duka jeupe pee Unamuuliza bei

ya bidhaa anakutajia BEI kama vile duka lake limejikamilisha yani,Haogopi kudodewa yeye yupo na bei zake sawa

na wenzake ambao maduka yao yamejikamilisha mpaka na ma AC ndani,Unamsikitikia kisha unamwambia ASANTE unaondoka hununui kitu.

Anakuja anaachia FREM ana bidhaa kibao zimebaki anatafuta wakumuuzia,anakuja kuuza kwa nusu ya bei aliyonunulia... wakati alikua na uwezo wakurudisha hela yake akawa amepata hasara 1 tu ya (Muda) .

Biashara kufa mikononi mwako ni uzembe na kutokua na akili ya kuwaza zaidi ya hapo ulipo na zaidi ya hicho unachofanya sasa hivi.
Kubadilisha gear angani
 
Asantee sana kiongoz Ila samahani naomba unisaidie kitu Nina mtaji Ila sijui nifanye biashara gani?
 
Mimi nimepanga kuanziasha biashara ya mafuta ya kupikia alizeti nakuwa nalangua mashineni wanapokamua kisha niuze naomba unipatie mbinu zaidi ili niweze mamimi kusimama kwenye biashara hii na kuifurahia mr. Controla
 
Back
Top Bottom