Watu wasahaulifu sana. Wamesahau jinsi kwa misimu zaidi ya mitatu sasa Simba imecheza mechi za ushindani mkubwa dhidi ya timu za Morocco, ikiwemo zile za Raja ambazo timu zote mbili zilibuni mbinu ya kutumiana vijembe mitandaoni kama mbinu ya kuongeza mwamko wa utalii nchini.
Watu wanasahau Simba kamtoa kigogo wa Africa Wydad hatua ya makundi msimu huu tu ulioisha ambayo kama huko Serikalini kungekuwa na watu wanaojua mbinu hasa za kukuza utalii hizi zote ni njia za kupita. Siasa imeingia, leo Yanga ndiyo wanaonekana vinara wa kukuza utalii. Ufahamu wetu wa utalii bado uko hatua ya chekechea hasa kwa kuwa siasa zimetutawala sana.
Hivi kati ya Simba na Yanga nani anaheshimika zaidi huko Morocco? Tukiweka siasa pembeni, kama tunatafuta engagement ya utalii kupitia michezo, option ipi ni bora zaidi?