Hakimu mkazi au resident magistrate ni nani?

Resident magistrate siyo mmoja mkuu,maelezo yoote uko sawia ila la hakimu kukaa hapo,hapana.Kila hakimu ana mahakama yake ya kazi ya kudumu kwa kipindi fulani.
 
Yule hakimu wake anaishi ndani ya jengo hilo la mahakama,
ndo maana inaitwa mahakama ya makazi kisutu,
yaani mahakama ya hakimu mkaaji wa mule mule ndani ya mahakama ya kisutu
 
Ya mafisad???
 
Mkuu pecuniary jurisdiction imeshaongezwa thamani,,angalia upya.
 
Hakuna kitu kama mahakama ya mkoa kwenye mfumo wa sheria zetu. Mfumo wa mahakama unaanzia 1. Mahakama ya Mwanzo. 2. Mahakama ya Wilaya. 3.Mahakama ya Hakimu Mkazi. 4.Mahakama Kuu, na 4. Mahakama ya Rufaa.

Ni Mahakama ya Rufani, Rufaa ndiyo kitendo chenyewe sawa sawa?
 
Mkuu acha dharau.
Hili swali linapaswa kujibiwa na mtu yeyote aliyesoma Civics Form Two na kuendelea. Kabla yakukujibu naomba kujua wewe umefikia level ipi ya elimu? Kama umevuka form two basi kuna shida kwenye mfumo wa elimu yetu.
Hili jibu lako ni la swali gani?



Soma hapa unaweza kujifunza jinsi ya kujibu swali kama lilivyouliza.
 
Nimekupata vyema mkuu naomba niswalishe nami kidogo juu ya
kazi za hawa ni zipi mahakamani?
1.KARANI
2.WAKILI
3.PP

Natamani sana kujua kazi zao na pia elimu zao.

Karibu mkuu..
 
iko hivi hizi mahakama zimepangwa kulingana na makosa na uwezo wa mahakimu katika kuamua kesi na ukubwa wa kesi mfano

1)Mahakama ya Mwanzo.
Hapa huamuliwa kesi za madai tu huwezi kukuta jaji katika mahakama hizi na mala nyingi mahakimu wake ni wenye elimu kiwango cha diploma mpaka degree moja una wakuta hapa

2. Mahakama ya Wilaya

Hapa uamuliwa makosa ya jinai na makosa ya madai ambayo yalitolewa mamuzi katika mahakama ya mwanzo lakini mamuzi hayo yakakatiwa rufaa hivyo kesi hiyo huamishiwa mahakama ya wilaya katika mahakama hii ndio utakuta majaji

3.Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Mahakama hii huhusisha makosa ya jinai tu kwaiyo kesi zilizopo hapa ni za makosa ya jinai tu na uamuliwa na majaji tu pia hushugulikia na zile kesi ambazo zimekatwa rufaa katika mahakama ya wilaya

Pia kumbuka si kila mkoa kuna mahakama ya hakimu mkazi

Kwa mtiririko wa maelezo haya nadhani utakuwa umepata mwanga kuwa
Mahakama Kuu, na Mahakama ya Rufaa zinajishugulisha na nini
 
Mkuu acha dharau.

Hili jibu lako ni la swali gani?




Soma hapa unaweza kujifunza jinsi ya kujibu swali kama lilivyouliza.
Ndo maana niliuliza level ya elimu. Kiwango cha elimu kinamwezesha mhusika kung'amua kwa urahisi taarifa anazopata. Kama hujaelewa hayo maelezo basi bahati mbaya, ni hakuna namna.
 
Yule hakimu wake anaishi ndani ya jengo hilo la mahakama,
ndo maana inaitwa mahakama ya makazi kisutu,
yaani mahakama ya hakimu mkaaji wa mule mule ndani ya mahakama ya kisutu
Mmmh Aisee..
 
Nimekupata vyema mkuu naomba niswalishe nami kidogo juu ya
kazi za hawa ni zipi mahakamani?
1.KARANI
2.WAKILI
3.PP

Natamani sana kujua kazi zao na pia elimu zao.

Karibu mkuu..
Wakili ni ntaalamu wa sheria ambaye kazi yake ni kutetea mtuhumiwa au kusimamia upande wa mlalamikaji.Elimu ya wakili ni kuanzia degree ya sheria na kuendelea na anakuwa na leseni ya uwakili na muhuri.Hata hivyo mawakili hawaruhusiwi mahakama za mwanzo.
 
Kumbe unadhani
 
Pp au Dpp ni mwendesha mashtaka anatajwa na ibara ya 59 B ya katiba ya jamuhuri.
 
Kwa hakimu mkazi kuhusu kesi kuendeshwa na majaji tuu ni uongo.Andy Lyamuya alikuwa jaji lini? Mahskimu hspa huitwa wakazi na mkuu wao ni principal resident magistrate yaani hakimu mkazi kiongozi.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kwanza fahamu kuwa neno Kisutu yaweza kuwa ni eneo au mtaa au mahali ilipojengwa mahakama.
Pili elewa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi ni level ya mahakama katika mfumo au muundo wa mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo huanza na mabaraza ya usuluhishi yaitwayo ward tribunals, baada ya hapo hufuata mahakama ya mwanzo ambazo husimamiwa na mahakimu wa mahakama ya mwanzo.
Pili ni mahakama ya wilaya ambayo husimamiwa na mahakimu wa wilaya chini ya usimamizi wa Hakimu Mkazi.
Tatu ni mahakama ya Hakimu Mkazi yenye wajibu wa kupokea rufaa toka mahakama, za chini na kesi nyingine zinazoletwa kwake moja kwa moja. Hapa ndipo ufahamu ya kuwa Kisutu ni jina la mahakama kama ilivyo sehemu nyingine zenye mahakama ya Hakimu Mkazi.
Nne ni mahakama kuu ambazo ziko kikanda na zina division au vitengo mbalimbali kama biashara, ardhi, kazi n.k. Mahakama hizi husimamiwa na majaji na husikiliza kesi nzito kama treason, murder na hupokea rufaa toka mahakama za chini.
Tano na mwisho ni mahakama ya Rufani inayosimamiwa na jaji mkuu na majaji wateule.

Hivyo pamoja na michango ya wengine nadhani umeelewa.
 
Kwa sababu. Mahakimu wengi Ni wanawake. Kama ujui lugha achana na jf
 
Hili swali linapaswa kujibiwa na mtu yeyote aliyesoma Civics Form Two na kuendelea. Kabla yakukujibu naomba kujua wewe umefikia level ipi ya elimu? Kama umevuka form two basi kuna shida kwenye mfumo wa elimu yetu.
Hata darasa la tano wanafundisha aina za Mahakama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…