Hakimu mkazi au resident magistrate ni nani?

Hakimu mkazi au resident magistrate ni nani?

Hakuna kitu kama mahakama ya mkoa kwenye mfumo wa sheria zetu. Mfumo wa mahakama unaanzia 1. Mahakama ya Mwanzo. 2. Mahakama ya Wilaya. 3.Mahakama ya Hakimu Mkazi. 4.Mahakama Kuu, na 4. Mahakama ya Rufaa.
Sasa unachopinga ni nini hiyo ya Hakimu mkazi si ndio level ya Mkoa?
 
Hata haihitaji kusomea sheria. Sisi tulifundishwa Form Two habari za mihimili ya dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.
Mfumo wa mahakama Tanzania wa Tanzania Bara unaanzia Mahakama ya Mwanzo. Hii ni mahakama ya ngazi ya chini. Inaweza kughukulika na mashauri ya kisheria kwenye kata au tarafa. Mashauri ambayo thamani yake haizidi elfu 50.(Japo busara pia inatumika). Hakimu wake anaitwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo au PCM kwa maana ya Primary Court Magistrate.
Mahakama inayofuata ni Mahakama ya Wilaya. Hii mahakama unspoken rufaa kutoka mahakama za mwanzo ndani ya Wilaya husika. Pia hupokea mashauri ambayo yanathamani zaidi ya shilingi elfu hamsini yasiyozidi laki mbili na nusu. Hakimu wake anaitwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya lazima awe walau na degree ya Sheria.
Mahakama ya Hakimu Mkazi inafuatia. Hii mahakama imepewa hadhi juu kidogo ya Mhakama ya Wilaya na inaweza kuthikiliza kesi ambazo thamani yake inazidi kidogo kiwango cha zile za wilaya. Hushughulikia mashauri ya ndani ya mkoa au Kanda. Hakimu wake anaitwa Hakimu Mkazi (idadi yao inategemea na mahitaji). Mara nyingi inaongezewa jina la mahali ilipo.
Mahakama inayofuata ni Mahakama Kuu. Hii inapokea rufaa kutoka Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Hakimu Mkazi. Pia hushughulikia mashauri ya jinai kubwa kama mauaji au kesi ambazo thamani yake ni kuanzia laki tano (busara). Mahakama kuu ni moja japo inafanya kazi kwa kanda. Hivyo haijalishi kosa lilopotendeka ila popote ndani ya Tanzania Bara shauri linaweza kufunguliwa. Kiongozi wa Mahakama hii anaitwa Jaji na anateuliwa na Rais.
Mahakama ya juu kabisa ni Mahakama ya Rufaa kwa Tanzania Bara. Kiongozi wa Mahakama hii ni Jaji Mkuu. Nayo inashughulikia rufaa kutoka Mahakama Kuu.
Huo ndiyo mfumo wa Mahakama ya Tanzania Bara. Kwa upande wa Zanzibar wao mfumo ni Tofauti kidogo japo. Hiyo ni knowledge ya Form Two.
Umeeleza mfumo wa kimahakama ila hujajibu swali
 
Hili swali linapaswa kujibiwa na mtu yeyote aliyesoma Civics Form Two na kuendelea. Kabla yakukujibu naomba kujua wewe umefikia level ipi ya elimu? Kama umevuka form two basi kuna shida kwenye mfumo wa elimu yetu.
Shida iko kichwani kwa mleta mada sio mfumo wa elimu yetu
 
Resident magistrate? Hapa hakuna elimu ya Civics wala ya sheria inayohitajika kujibu hili swali.
Ni kiingereza tu.
Mimi nadhani ni kutokana na kuwa huko nyuma kutokana na upungufu wa majaji wa mahakama kuu na ile ya rufaa majaji walilazimika kuzunguka mkoa mmoja hadi mwingine kwenda kutoa hukumu.. Yani unakuta jaji anatoka Mbeya kwena Iringa, Mwanza kwenda Shinyanga ili kutoa hukumu hivyo kuwafanya majaji wawe 'non resident magistrates'. Sasa kutokana na mashitaka kuwa mengi na kuchelewa kutolewa hukumu mahakama ikaamua ianzishe mahakama yenye uwezo wa kushughulikia baadhi ya mashauri ambayo sio lazima yashughulikiwe na majaji ndio wakaamua kuwe na hakimu wa kudumu wa eneo husika atayesikilisha mashauri madogo madogo na yale makubwa yangemsubiri jaji, Huyo hakimu wa kukaa eneo hilo nadhani ndio wakaamua wampe jina la resident magistrates yanii hakimu anakaa eneo lake la kazi hivyo kuwa hakimu mkazi.
We umejibu swali vizuri,engine wanatuletea ngonjera tu na swali la making hawajibu,
 
Hili swali linapaswa kujibiwa na mtu yeyote aliyesoma Civics Form Two na kuendelea. Kabla yakukujibu naomba kujua wewe umefikia level ipi ya elimu? Kama umevuka form two basi kuna shida kwenye mfumo wa elimu yetu.
Huko sijafika mkuu niliishia kwa ras simba
 
Hakuna kitu kama mahakama ya mkoa kwenye mfumo wa sheria zetu. Mfumo wa mahakama unaanzia 1. Mahakama ya Mwanzo. 2. Mahakama ya Wilaya. 3.Mahakama ya Hakimu Mkazi. 4.Mahakama Kuu, na 4. Mahakama ya Rufaa.
Kumbe
 
Yule hakimu wake anaishi ndani ya jengo hilo la mahakama,
ndo maana inaitwa mahakama ya makazi kisutu,
yaani mahakama ya hakimu mkaaji wa mule mule ndani ya mahakama ya kisutu
Hahah,elungata
 
Yule hakimu wake anaishi ndani ya jengo hilo la mahakama,
ndo maana inaitwa mahakama ya makazi kisutu,
yaani mahakama ya hakimu mkaaji wa mule mule ndani ya mahakama ya kisutu
Kwa hivyo ni kama bwana yule aliyeng'ang'ania ndani ofisin, buguruni?
 
Mahakimu wa Kisutu ndio Mahakimu wenye Kesi za Maana, na Escrow, ma EPA, Ma Richmond na watakatisha Fedha wote wanshtakiwa Kisutu!

Hakimu wa Kagera au Sumbawanga ataishia kusikiliza kesi za Imani za kishirikina na Migogoro ya Kijinga jinga
Khaaaa..mkuu mbona umeenda mbali sana
 
iko hivi hizi mahakama zimepangwa kulingana na makosa na uwezo wa mahakimu katika kuamua kesi na ukubwa wa kesi mfano

1)Mahakama ya Mwanzo.
Hapa huamuliwa kesi za madai tu huwezi kukuta jaji katika mahakama hizi na mala nyingi mahakimu wake ni wenye elimu kiwango cha diploma mpaka degree moja una wakuta hapa

2. Mahakama ya Wilaya

Hapa uamuliwa makosa ya jinai na makosa ya madai ambayo yalitolewa mamuzi katika mahakama ya mwanzo lakini mamuzi hayo yakakatiwa rufaa hivyo kesi hiyo huamishiwa mahakama ya wilaya katika mahakama hii ndio utakuta majaji

3.Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Mahakama hii huhusisha makosa ya jinai tu kwaiyo kesi zilizopo hapa ni za makosa ya jinai tu na uamuliwa na majaji tu pia hushugulikia na zile kesi ambazo zimekatwa rufaa katika mahakama ya wilaya

Pia kumbuka si kila mkoa kuna mahakama ya hakimu mkazi

Kwa mtiririko wa maelezo haya nadhani utakuwa umepata mwanga kuwa
Mahakama Kuu, na Mahakama ya Rufaa zinajishugulisha na nini
Jibu swali la msingi,acha kupuyanga
 
Resident magistrate? Hapa hakuna elimu ya Civics wala ya sheria inayohitajika kujibu hili swali.
Ni kiingereza tu.
Mimi nadhani ni kutokana na kuwa huko nyuma kutokana na upungufu wa majaji wa mahakama kuu na ile ya rufaa majaji walilazimika kuzunguka mkoa mmoja hadi mwingine kwenda kutoa hukumu.. Yani unakuta jaji anatoka Mbeya kwena Iringa, Mwanza kwenda Shinyanga ili kutoa hukumu hivyo kuwafanya majaji wawe 'non resident magistrates'. Sasa kutokana na mashitaka kuwa mengi na kuchelewa kutolewa hukumu mahakama ikaamua ianzishe mahakama yenye uwezo wa kushughulikia baadhi ya mashauri ambayo sio lazima yashughulikiwe na majaji ndio wakaamua kuwe na hakimu wa kudumu wa eneo husika atayesikilisha mashauri madogo madogo na yale makubwa yangemsubiri jaji, Huyo hakimu wa kukaa eneo hilo nadhani ndio wakaamua wampe jina la resident magistrates yanii hakimu anakaa eneo lake la kazi hivyo kuwa hakimu mkazi.
Kidoogo nimekuelewa elewa mkuu
 
Mi nilpata A civics form 2 na 4 lakini sijui kwanini inaitwa hivyo sababu nilkuwa napenda masomo ya sayans hasa pcm..ukisema hivyo inamaana hata mimi nikimfata lawyer nikamuuliza kwanini gari ikifunga breki unasukumwa mbele akishindwa nimwambie kuna tatizo kwenye elimu yetu...jibu kama unajua kwanini hakimu mkazi kisutu?
Asante kwa swali nzuri ulompa
 
Back
Top Bottom